Mizengo Pinda aenda kutibiwa UK

Tumesikia kwamba mh. Pinda -Waziri mkuu wa Tz,kaondoka leo kwenda kutibiwa UK kwa wiki moja.
Nadhani ziara ndefu na wingi wa kazi umemchosha sana,kwani hata mwendo miguu inaonekana sio sahihi kabisa,kwani asitibiwe Muhimbili tu.Wanadai kaenda na mkewe tu,kitu ambacho sio rahisi laziza wasaidizi wawepo.Anyway tunamtakia matibabu mazuri waziri mkuu wetu.

I hope haendi kutibiwa St Thomas Hosp in greater London.

Kambarage, Adul wakil. walipitia hapo!!!!!!!!!!!
Dr Omar was there, in less than a month.....
 
Eti kutibiwa UK. Hizo hela nasema siku zote: wangeamua kuziwekeza katika hospitali moja huko Tanzania.

Upuuzi mtupu. Kwanza sisi wananchi ndio waajiri wake, je tumempa lini ruhusa hiyo ya kutumia fedha zetu?

Halafu mtu mwenyewe tunafahamu anaumwa nini, sana sana akija huku ataambiwa apumzike, anywe maji na atumie supplements. HYPOCRITE!!
 
wanajamvi jana niliona katika taarifa ya habari TBC, Waziri Mkuu Pinda ameondoka jana kwenda London kwa ajili ya Uchunguzi wa Kiafya. nini kinamsumbua Mtoto wa Mkulima huyu kiafya mpaka aende London??.au ni issues nyingine!!!!! wenye news mwageni hapa
 
watu mnalalamika sana,hata mimi ningekuwa PM ningeenda kutibiwa uk,kwani ndio jadi yetu,ya kugawana riziki,kumbuka huko ulaya haendi peke yake,kuna wife/house ndogo,kuna Daktari wake atamsindikiza,kuna wapambe,etc,na pia ni opportunity ya kupumzika baada ya kutoka SUMBAWANGA -mpanda ktk kazi nzito za kijadi.
cha msingi ni kuangalia hizo gharama kwa mwaka ni kiasi gani,tuanze na JK,PINDA,Mawaziri, then tufanye hesabu zingetumika ktk kujenga zahanati ngapi,shule,polis post,etc.
:angry:
 
WAZIRI MKUU wa Tanzania, Mizengo Pinda jana ameondoka nchini kuelekea nchini Marekani kwa ajili ya kwenda kuchunguza afya yake kwa ujumla.
Waziri huyo aliondoka jana akiongozana na mke wake akielekea nchini humo ambapo aliagwa na mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam .

Waziri Mkuu huyo anatarajiwa kurudi nchini baada ya wiki moja baada ya kukamilisha zoezi hilo la kuangalia afya yake kukamilika.

NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.
 
Poa mkubwa ila hii thread ililetwa jana tukaijadili. Mwache mtoto wa mkulima akatibiwe kidogo manake yeye huwa ni ndani tu na vumbi lake!
 
wanajamvi jana niliona katika taarifa ya habari TBC, Waziri Mkuu Pinda ameondoka jana kwenda London kwa ajili ya Uchunguzi wa Kiafya. nini kinamsumbua Mtoto wa Mkulima huyu kiafya mpaka aende London??.au ni issues nyingine!!!!! wenye news mwageni hapa

kuchekiwa afya pamoja na mambo mengine kam kutengeneza mazingira ya kuwa na account za tusenti twao. mkuu wao alikuwa west indies kwenye tubembea na huko kuna tu-benki twakufichiwa vijisent.
 
Siku zote huwa watanzania tunafungwa kamba. Mara kuchekiwa afya, mara sijui nini, kumbe wana mambo yao. Siku moja yote hayo yatawekwa hadharani na watu makini.
 
ivi haya mwisho wake ni lini???
ivi kama tuna uwezo wa kujenga daraja la UMOJA na kuchangia billions kwa masherehe-sherehe tu
kweli inashindikana iyo pesa yote tujenge kituo cha afya cha nguvu apa bongo na kuweka watalaamu wetu na technicians,,,hawa watu wachekiwe afya hapa bongo?
sasa msululu wa allowances za safari na pesa za kujikimu zote izi...$##&&**$#

aisee
 
Waziri Mkuu Pinda ameondoka jana kwenda London kwa ajili ya Uchunguzi wa Kiafya. nini kinamsumbua Mtoto wa Mkulima huyu kiafya mpaka aende London??.au ni issues nyingine!!!!! wenye news mwageni hapa
.
PM Pinda, ni mtoto wa mkulima kiukweli, haumwi chochote, ila anakwenda kutimiza tuu matakwa ya moja ya stahili zake.

Miongoni mwa stahili za wale viongozi watano wakuu pamoja na wasataafu wa nafasi hizo, ni pamoja na kuchekiwa afya zao nje ya nchi mara moja kila mwaka.
Huduma ambazo wakuu hawa wanapewa kama stahili zao, hawawezi kuzikwepa hata kama wako fit kabisa, lakini lazima wakachekiwe.
Miongoni mwa stahiki za waheshimiwa wabunge, ni pamoja na kupatiwa gari, dereva, ofisi, mwanhalizi wa ofisi na msaidizi. Fedha za huduma zote hizo, hulipwa kwa kila mbunge kwenye mshahara wake. Fanya utafiti utakuta wabunge wengi hawakai kwenye hizo ofisi zilizoandikwa Ofisi ya Mbunge, hivyo fungu la mwangalizi wa ofisi, wanatia ndani, wengi hawana wasaidizi, wanajisaidia wenyewe, fungu wanatia ndani, wengi hawana madereva, wanajiendesha wenyewe, fungu wanatia ndani, ila wabunge wao wakiugua, pia wanatibiwa nje ya nchi.

Mwachieni Pinda, mwana wa mkulima.
 
kwa nini wasicheki pale muhimbili..au hilo sio kituo cha afya?
 
kwa nini wasicheki pale muhimbili..au hilo sio kituo cha afya?
Stahili ni stahili na hivyo waliozibuni waliona inafaa, jee unajua kuwa kila rais akisafiri/akifanya ziara au kila alipo, yuko na timu ya watu 21?.
Unajua kuna mtu kazi yake kubeba sanduku lake la nguo?. Mbona wabebaji wa hoteli wapo?.
Unajua kuna mtu kazi yake kumshauri avae nini au kumsaidia kuvaa?. Kwani mwenyewe hawezi?.
Unajua kuna mtu kazi yake kuonja tuu chakula kabla yeye hajala?
Kuna mbeba speech, siku hizi pia anabeba laptop?.
Unajua kuna mpiga picha?
Unajua kuna mpiga video?
Unajua kuna mwandishi wa habari?
Unajua pia mkurugenzi wake wa Mawasiliano yupo wakati wote? etc etc.

Hivi wote hawa ni rais anayewahitaji ama ni sehemu ya stahili zake?.

Hata kama Mtoto wa mkulima Pinda, angependa achekiwe Muhimbili, stahili inasema atachekiwa nje ya nchi mara moja kila mwaka atake asitake!
Mwacheni jamani mtoto wa Mkulima!.
 
Huyu hana tofauti na Mkuu wa Kaya kusafiri nje!
Alikuwa Japan na Vietnam mwishoni mwa mwezi wa 3.

Tukumbuke alikuwa London vilevile mwezi wa 3 mwaka jana.
Chukua Chako Mapema.
 
wanajamvi jana niliona katika taarifa ya habari TBC, Waziri Mkuu Pinda ameondoka jana kwenda London kwa ajili ya Uchunguzi wa Kiafya. nini kinamsumbua Mtoto wa Mkulima huyu kiafya mpaka aende London??.au ni issues nyingine!!!!! wenye news mwageni hapa
wewe ndiye mwenye news, sasa unaomba zipi tena? tujuze basi...
 
Stahili ni stahili na hivyo waliozibuni waliona inafaa, jee unajua kuwa kila rais akisafiri/akifanya ziara au kila alipo, yuko na timu ya watu 21?.
Unajua kuna mtu kazi yake kubeba sanduku lake la nguo?. Mbona wabebaji wa hoteli wapo?.
Unajua kuna mtu kazi yake kumshauri avae nini au kumsaidia kuvaa?. Kwani mwenyewe hawezi?.
Unajua kuna mtu kazi yake kuonja tuu chakula kabla yeye hajala?
Kuna mbeba speech, siku hizi pia anabeba laptop?.
Unajua kuna mpiga picha?
Unajua kuna mpiga video?
Unajua kuna mwandishi wa habari?
Unajua pia mkurugenzi wake wa Mawasiliano yupo wakati wote? etc etc.

Hivi wote hawa ni rais anayewahitaji ama ni sehemu ya stahili zake?.

Hata kama Mtoto wa mkulima Pinda, angependa achekiwe Muhimbili, stahili inasema atachekiwa nje ya nchi mara moja kila mwaka atake asitake!
Mwacheni jamani mtoto wa Mkulima!.

Huwezi ku-compare hizo 'stahili' za rais na hii ya kwenda kutibiwa nje. On one side...hizo za rais ni neccessary...they come with the job. Ni kama kazi nyingine zinavyoweza kukulipia mwanao fees. Au mfano mwingine ni protection anayopewa balozi na watumishi wa ubalozi.
Ishu hapa ni matibabu kufanyika nje ya nchi! kama huoni hiyo ni ishu...basi! Kwani hayo matibabu yanaweza kutolewa huko nje tu? Hii ni sawa na kusema...mpiga video wa rais awe mzungu tu! The issue sio kuwa na mpiga video, the issue ni kwa nini awe mzungu! wengine hawafai? Hospitali zetu hazifai? And by the way...who makes these 'stahili'? I thought Pinda is a top dog...and if he cant change them...who can?
 
Back
Top Bottom