Elections 2010 Mizengo Kayanza Peter Pinda's Profile

Tukumbuke mkwere na kambi yake (mafisadi) hawachagui wazalendo halisi kuongoza nchi, Pinda amechaguliwa ili aendeleze "umesenja". Magufuli moto mwingine!
 
Akina EL na RA wanadai Pinda na mgogoro mbaya wa kiafya. Matarishi wao jana na juzi wameshinda kwenye mabaa mbalimbali hapa Dodoma wakidai "mgogoro" wa afya yake ni mkali sana.

Nina mashaka na afya za wakubwa wetu!
 
Ndio Mizengo Pinda a.k.a Uso wa Mamba....hamna kucheka nao safari hii....wakunjie sura hao mafisadi, tunakukubali kati ya wana CCM wote.
God Bless you
 
Ndio Mizengo Pinda a.k.a Uso wa Mamba....hamna kucheka nao safari hii....wakunjie sura hao mafisadi, tunakukubali kati ya wana CCM wote.
God Bless you

Umesahau huwa anamwaga chozi anapobanwa maswali?
 
Mzee Pinda kazi kwa kwenda mbele acha tu kuchekea au kulilia mafisadi. Mie naamini Mzee Pinda anaweza ila aache tu uoga na kulia hilo linamshusha chini. Akaze buti na napenda pale anapojibu maswali ya pao kwa papo ingawa hayana manufaa kwani hakuna ufuatiliaji wowote ule zaidi
 
Hiyo shule mbona ipo wazi coz Kapinda kasobea hapo kwenye hizo BETO(toilets)
 
Waziri Mkuu ni mteule wa Rais. Anayetaka kumchagua Pombe kuwa Waziri Mkuu agombee urais ili akipata amteua kuwa PM wake period.
 
Ni kweli kabisa ,Pinda ni ni msafi yeye kama yeye, likini ndugu zangu Afya yake ina matatizo makubwa na ni siku nyingi tena yeye na mwenzi wake, kwa hiyo wasiwasi wangu ni kwamba hawezi kujiamini ktk utendaji wake,wote tunajua ule ugonjwa ukishampata mtu huwa anajihisi mnyonge, na mara nyingi huwa wanakosa maamuzi kwa kuogopa kudharauliwa,MOLA tuonee huruma dawa zije mapema Makamanda wanaangamia
 
Umesahau huwa anamwaga chozi anapobanwa maswali?


Safari hii ni zamu ya mafisadi kumwaga machozi hasa Chenge..You know Pinda ni mpole na watu wapole mara nyingi huwa wanaonyesha hisia zao kwa kulia ili kuweka MSISITIZO waeleweke manake hawana maneno mengi ya kuongea... Go Pinda a.k.a Mamba face no kucheka.
 
Hivi huyu MKPP ana uhusiano gani na usalama wa taifa?
au alikua na uhusiano gani na hii taasisi?
na je uhusiano wake umeisha?
 
Safari hii ni zamu ya mafisadi kumwaga machozi hasa Chenge..You know Pinda ni mpole na watu wapole mara nyingi huwa wanaonyesha hisia zao kwa kulia ili kuweka MSISITIZO waeleweke manake hawana maneno mengi ya kuongea... Go Pinda a.k.a Mamba face no kucheka.

Wewe naona umekaa kifisadi! Umeshindwa kuelewa kwamba pinda yuko chini ya jk ambaye aliwapamba mno mafisadi wakati wa kampeni, huo uso wake wa mamba utasaidia nini?
 
Hivi mmesahau kwamba Kikwete anachagua usalama wa taifa tu kwenye baraza la mawaziri?
 
Ni kweli kabisa ,Pinda ni ni msafi yeye kama yeye, likini ndugu zangu Afya yake ina matatizo makubwa na ni siku nyingi tena yeye na mwenzi wake, kwa hiyo wasiwasi wangu ni kwamba hawezi kujiamini ktk utendaji wake,wote tunajua ule ugonjwa ukishampata mtu huwa anajihisi mnyonge, na mara nyingi huwa wanakosa maamuzi kwa kuogopa kudharauliwa,MOLA tuonee huruma dawa zije mapema Makamanda wanaangamia

Nafikiri si busara kumshambulia mzee Pinda juu ya afya yake. Hapa ongelea utendaji wake. Tunajua si fisadi na anapenda nchi yake. Ugomvi wetu ni kwa bwana aliyechukua nchi kwa mabavu. By the way wewe umepima au ni wale wale waliokunywa uji wa mgonjwa
 
Ndugu wana JF.

Nimepokea bila mshituko wala msisimko wowote kuwa Mizengo Pinda ameteuliwa kuwa PM.

Kimsingi Pinda ni muadilifu na ana haiba ya 'mtu mwenye kutenda haki'. Tatizo la Pinda ni moja tu: Ni muoga. Chaguo sahihi la mafisadi. Wanataka mtu anayeweza kulia na kutoa machozi kama mtoto mdogo bungeni. PM ambaye mafisadi wakimuamuru 'sema meremeta ni ishu ya JWTZ' akubali na aseme. Au fisadi akimtuma 'muambie Zitto Kabwe hatorudi Bungeni 2010' anasema kweli. Aibu ya TZ.

Tangu ateuliwe 2008, amedhihirisha kuwa ni muoga na kwa hiyo amewafanya WaTZ wakichukie chama chake kwa sababu siyo jasiri. Hawezi kuthubutu. Nathubutu kusema bora Lowasa kuliko Pinda. Ubaya wa Lowasa ni tabia yake ya kufanya ubia na wahujumu uchumi....Wahindi.

Kwa kifupi kuteuliwa kwa Pinda ni muendelezo wa kiduku.

Makinda TV.
Hii ni runinga. Tena runinga ya mbao. Kazi ya huyu maza ni kutafuta vifungu vya kulisha 'ban' wabunge watakao chokonoa maslahi ya waliomuweka. Aibu yetu. Aibu ya Tz.

Skizia baraza la mawaziri. Usishangae kuyakuta majina yafuatayo:

  • Makongolo Mahanga (PhD feki)
  • Zakhia Meghji (WaTz wamesahau madudu yake akiwa hazina)
  • Lawrence Masha (rafiki na kipenzi cha familia)
Kama kawaida. Mkwere anaendeleza harakati zake za usanii kwenye uongozi wa nchi. Katika Zama hizi ambapo Watanzania wanataka viongozi wanauthubutu.

Ndiyo maana mimi ni mfuasi wa Chadema kwa sababu viongozi wake wanathubutu.

Sasa tunaletewa mtu anayetumwa, tena na mafisadi, "kaseme hivi...". Kazi ipo.

Ndiyo maana nathubutu kuuliza, Pinda ni bora kuliko Dr. John Pombe Magufuli?

Nisaidieni.
Wewe ni mtundu, mtoto wa mjini na mtu mwenye hoja zenye ujazo, daima huwa najivunia kuwa na watu kama nyie ndani ya hili jamvi.
 
Ni ukweli mtupu kuwa bila kuwa na serikali adilifu kamwe hatutapata maendeleo ya kweli. Complacency ya serikali ya CCM naamini inasababu za kimfumo zaidi na wala sio credibility ya mtu mmoja mmoja. Japo mara chache hutokea binadamu wachache waliojaaliwa vision na commitment katika jamii zao kama kina Mwalimu Nyerere, Mandela na kadhalika, hatuwezi kuwategemea hao katika kuhakikisha tunayapata maendeleo tunayoyatamani siku zote. Dawa ni kujenga mfumo imara ambao ni mafisadi-proof.

Katika nchi za wenzetu kama China, Japan, Marekani etc viongozi wanaonyesha uadilifu wa kiwango hitajika na naamini sio kwa sababu wao ni wasafi sana mioyoni mwao bali wanalazimishwa na mifumo thabiti ambayo haiwaruhusu kuthubutu japo kufikiria tu kufisadi nchi zao. Kwa mfano tunaona jinsi Obama anavyopelekeshwa na Republicans na pia jinsi Bush alivyopelekeshwa na Democrats enzi zake. Lazima serikali iliyopo madarakani itajitahidi ku-perform tu maana ikicheza tu nje! China nao wana mfumo wa kivyao wa kupambana na complacency.

Mimi naona namna pekee kwetu Tanzania ni kuing'oa tu CCM ikae pembeni japo kwa miaka mitano na chama kingine kiunde serikali. Later wakirudi ulingoni watakuwa na adabu! Na pia hicho chama kingine kitashika adabu tu. Without this cycling ya kuendesha serikali kamwe hatutafika popote na tutabaki pointing fingers to each other bila ya manufaa yoyote!

Cha muhimu kuliko vyote kwa sasa ni sisi kujitahidi kuwaelimisha ndugu zetu hasa kule vijijini wajue kuwa upinzani sio kiama. Tukumbuke thamani ya kura ya mpiga kura wa kijijini ni sawa na ya mwana-JF yeyote humu!

Mwaka 2015 sio mbali jameni!
 
- Uteuzi wa Waziri Mkuu kuwa Mh. Pinda, ninaukubali sana kwa sababu ni kiongozi makini sana, ana uwezo mkubwa wa kufikiri, very humble man ni muelewa wa wakati na besides anajua kua kama Mawaziri wote wakuu waliopita kabla yake, anatakiwa kuonyesha utiifu zaidi kwa aliyemteua kufuatana na misngi ya katiba ya Jamhuri.

- Sisi hata Mungu anatuasa kuwaombea viongozi wetu wa taifa na hata wa local, na wabunge wote, tuwaombee sasa maana tunawahitaji sana kutumia hekima na busara kuliongoza taifa letu!



William.
 
Back
Top Bottom