Mitazamo na tathmini ya Uchaguzi 2015

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
15,409
31,394
Baada ya 'kiza' cha siku kadhaa katika mtandao, tutakuwa na mabandiko yakiangalia uchaguzi uliomalizika
Kwa kutambua hatma ya taifa letu ni yetu sote. Mtazamo wetu upo wazi kujadiliwa kwa maono na maoni mbali mbali

Njia nzuri kama taifa ni kujadiliana, na taifa lenye mijadala lina 'afya' kuliko lile linalotenda kizani
Kwamba, eti kuzungumzia mustakabali wa taifa ni makosa , uhalali ni kupiga makofi na kumeza bila kutafuna

Hatuwezi kuwa jamii iliyokamilika kama tutaendelea na utamaduni wa kufanya mambo gizani, kubinya uhuru wa kujieleza, kunyima fursa ya wananchi kujadiliana kwa amani na viongozi kusikia wananchi wanajadiliana nini

UTANGULIZI

Tumewahi kuzungumzia maana ya uchaguzi. Kwa uchache, ni hatua za kuchagua au kuchaguliwa kushika madaraka ya uongozi iwe katika serikali, taasisi ,jamii n.k.

Tumefanya uchaguzi wa serikali kuu na za mitaa kwa pamoja mwaka huu

Tumechagua wanasiasa watakaounda serikali au uwakilishi bungeni

Matokeo yametangazwa na tume ya uchaguzi na mshindi kupatikana

Jambo moja la kukumbuka, uchaguzi ni mtiririko wa hatua na wala si kupiga kura tu

Kura ni hatua ya kileleni kabla ya kukamilisha uchaguzi kwa hatua ya mwisho ya kutangaza matokeo

Kuanzia kuitishwa uchaguzi, kampeni hadi kupiga kura na kutangaza matokeo, vyote hivyo hufanya uchaguzi ukamilike

Na ili uchaguzi ukamilike ni lazima uwe huru na wa haki (Free and fair) katika hatua zote

Lakini pia,uchaguzi kuwa wa huru na haki (free and fair) haimaanisha uchaguzi huo umetoa mshindi halali

Ili uchaguzi uwe huru na haki, inapaswa kuwepo vionjo (elements), baadhi vikiwa vifuatavyo

1. Integrity ikimaanisha ubora wa kuaminika uliojengwa katika misingi ya maadili ya kiwango cha juu

2. Credible - Unaoweza kuaminika na wenye nguvu ya kushawishi kwamba ulifanyika kama ilivyo namba 1 hapo juu

3 Legitimate- Kwamba upo katika misingi ya kisheria au kanuni kwavile umepata integrity na ni credible

Siku zote wanasiasa wamekimbilia kauli rahisi ya 'uchaguzi ulikuwa huru na haki' je, uchaguzi huo ulikuwa na integrity, ni credible au legitimate? Haya hutayasikia hasa kwa viongozi wa nchi masikini kama zetu

Hivyo, tunatakiwa tujiulize, baada ya miaka 50 ya kujitawala, je uchaguzi 2015 ulikuwa free and fair, ulikuwa na integrity, credibility au legitimacy?

Tutaanza na sehemu ya 1 kati ya V.

Wakati ukifika tutajadiiliana, tunaomba subra kidogo

Inaendelea.......sehemu ya I
 
Sehemu ya I

TUME YA UCHAGUZI (NEC)

Hiki ni chombo kinacho ratibu na kusimamia shughuli zote za uchaguzi mkuu nchini kwa mujibu wa sheria

Ili kutekeleza majukumu yake, tume itashirikiana na vyombo vingine kama wadau

Sifa muhimu ya tume huru ya uchaguzi ni kusimamia sheria, kanuni na taratibu bila kufungwa au kufungamana

Nchi nyingine, tume ya uchaguzi hupatikana kwa utaratibu utakaoilinda dhidi ya vishawishi au kuingiliwa(independent)

Ili Tume iwe na sifa za kuaminika, wajumbe hupatikana kutoka katika jamii,kwa sifa za uaminifu, ukweli na uzalendo

Aghalabu, tume za wenzetu hushirikisha viongozi wa kiroho kupata integrity and credibility

Moja ya taratibu za kuifanya tume iwe huru ni namna ya kupata wajumbe na wanavyoweza kupoteza sifa

Kwamba upo utaratibu wa kisheria usioweza kuingiliwa na mtu au kikundi cha watu

Kwa utaratibu wetu Tanzania, tume inachaguliwa na Rais

Na kwa utaratibu wa kisiasa, Rais anatokana na vyama vya siasa.

Rais anaweza kuwa mgombea wa chama cha siasa au kuwa na nyadhifa akiwa na mamlaka ya kuteua Tume

Inatokea, Rais anakuwa kiongozi wa serikali wakati akiwa mgombea wa chama

Kwamba, sura moja ni ya ugombea, sura ya pili yeye ndiye mteuzi wa wale watakaosimamia uchaguzi anapogombe

Na zipo nyakati Rais akiwa mdau wa siasa anakuwa na mgombea ambaye ni mwanachama wa chama chake

Hivyo, Rais anakuwa na majukumu mawili, kwanza kusimamia shughuli za serikali ikiwemo uteuzi wa itakayosimamia uchaguzi unaomhusu mdau katika chama chake anachokiongoza kutafuta ridhaa ya kuongoza

Kwa lugha nyingine, Rais amepewa nguvu na ushawishi mkubwa katika utendaji na majukumu ya kila siku ya Tume

Inaweza isisemwe na wala haijaandikwa popote,akili za kawaida za mwanadamu zinaweza kumfikisha kuamini hivyo

Mwananchi ataamini Tume ipo kisheria tu bila kuwa na imani nayo

Tujiulize kidogo, tume yetu ya uchaguzi ni huru? Inakidhi vigezo vya Tume huru ya uchaguzi?

Inaendelea sehemu ya II
 
Mkuu Nguruvi,

Naomba niwie radhi kwa kuchangia kabla hujamaliza hoja zako. Nilipoona tu kichwa cha bandiko hili kuna kitu kikaregister kichwani mwangu - "Marudio". Nimesoma sehemu ya utangulizi na sehemu ya kwanza nimeona kweli kile nilichowaza ndio kweli 'kinaoneka' kinakuja kwenye mtiririko huu.

Upinzani umeingia kwenye uchaguzi wa 5 dhidi ya serikali ya CCM. Mara 5 na serikali ile ile ya CCM. Na katika mara hii ya 5 wame "bahatika" kupata uzoefu kutoka ndani ya CCM. Katiba, Tume ya Uchaguzi na sheria za uchaguzi sio mpya ni zile zile. Kama ungekuwa unaweza kusafiri kurudisha muda nyuma, baada ya kila uchaguzi kati ya hizi tano ukafanya tathimini kama unayotaka kufanya sasa hivi nina uhakika kwa asilimia kubwa sana utarudi ma majumuisho yale yale kwa kila uchaguzi.

Nikuombe radhi tena kwa sababu nimechangia bila kuona majumuisho yako uliyotaka kuyaonesha kwenye huu uchambuzi wako lakini kama nilivyosema nadhani nimeshausoma huu uchambuzi kwenye historia za miaka iliyopita. I have seen this movie too times, nikiona tu unavyoanza najua inavyo isha. Kipya ambacho unaweza kukiongeza ni kuonesha specifics za uchaguzi huu lakini najua hizo nazo hazitasaidia wewe usifike kwenye hitimisho lile.

Kifupi ni kuwa;
CCM haikuwa na ajenda ya katiba mpya, ila kwa "werevu" waliiba na kuihodhi kama yao kitu ambacho kiliwapa uwezo wa kudictate mlolongo mzima. Nakukumbuka Mwanakijiji kwenye makala zake zote kipindi kile alipinga ule mchakato jinsi ulivyoanzishwa na kuhodhiwa na CCM ila nakiri na mimi nilikuwa mmoja wa walimuona anaweka vikwazo tu wakati watu wanataka katiba mpya. Anyway, wakahodhi mchakato mzima na matokeo yake katiba iliyotakiwa haikupatikana. Bunge la kitiba likarudi na a modestly improved katiba ya sasa with no major changes ambayo hata hiyo nayo hata haikupita. Uchaguzi ukafika tukaingia kwenye mchakato na muundo ule ule kwa maaana ya katiba ile ile, muundo ule ule wa tume ya uchaguzi na sheria zile zile za uchaguzi. And guess what? well, we all know the rest..

Ndio maana nasema hii tathmini kama nishaisoma (niwie radhi tena).

My prayers to Zanzibar, i hope they come to their senses there (in time) and announce Seif Sharif Hamad and we get over this uchaguzi thing!
 
Mkuu Galaxy3 hapo juu, unaweza kuwa sahihi au la. Mtiririko wa matukio unafafana, ili njia zinatofautiana
Tathmini hii haitaangalliasi uchaguzi tu bali hali ya kisiasa nchini. Watu waegemee nini

Ni tofauti
 
SEHEMU YA II

Mara zote wabunge waliokwmisha suala la tume huru ya uchaguzi ni CCM
Walifanya hivyo wakijua muundo wa sasa ambapo wana serikali, ingekuwa vema tume ibaki ilivyo

Wapinzani pamoja na jitihada zao, wakakubali kwenda katika uchaguzi bila kujifunza kutoka chaguzi za nyuma

Hili ni kosa, kwasababu tayari walikuwa na nguvu kubwa kutoka katika jamii iliyotaka kuona haki ikitendwa

Uchaguzi ukatangazwa na kampeni kuanza. Kkumekuwepo na hali zilizotia shaka juu ya integrity na credibility ya ya uchaguzi.

Mathalan lilipotokea tatizo upande mmoja tume ilikemea, kwa upande mwingine tume ilikaa kimya

Hali ikapelekea baadhi ya vyama kuanza kutangaza matokeo na asilimia za ushindi.

Kisheria hilo ni kosa, na hatujui kwanini Tume ya uchaguzi haikuliona kama kosa?

Fursa za kampeni kwa kutumia vyombo vya habari zilitia shaka sana.

Kwamba, mamlaka husika zenye udau na tume ya uchaguzi zilikaa kimya pale upendeleo ulipoonekana wazi

Matumizi mabaya ya vyombo vya umma ilikuwa kawaida

Hali iliyozidisha mashaka ni pale zilizpokuwepo habari za kuashiri hujuma kama uwepo wa kura na maboksi feki

Inawezekana ilikuwa ni uvumi, Tume ilikuwa na wajibu wa kuwaondoa wananchi wasi wasi, mengi yalipita kimya kimya

Kwa mfano, mwenyekiti wa NCCR amedai kukamata masanduku feki na kuyafikisha Polisi

Siku iliyofuata ushahidi ukwa umepotea kwa mujibu wake.

Hilo ni jambo zito katika kuaminika kwa uchaguzi. Tulitegemea Tume ilitolee kauli!

Kutangazwa kwa matokeo

Hapa ndipo palipo na sintofahamu. Kazi ya tume kama ilivyosema ni kujumlisha kura.

Hilo si jambo la siri kwasababu tayari zilishapigwa na kutangazwa vituoni.

Hakukuwa na tatizo kwa vyama vya siasa kujiridhisha kwa matokeo yaliyotolewa. Inafanyika duniani kote.

Hoja hapa ni kuwa kujumlisha kura hakubadili matokeo wala kuiondolea Tume nguvu ya kutangaza matokeo hayo

Zaidi inajenga imani na utaratibu mzima. Nakala kutoka kwa mawala zipo, iweje kuwe na sita sita kutoka Tume

Utangazaji wa matokeo ungefanyika kwa wakati mmoja. Kwamba, Tume imekamilisha zoezi ambalo halikutarajiwa kuchukua muda kutokana na kuimarika kwa mawasiliano nchini.

Hata ilipobidi kutangaza, ilitakiwa kusiwe na hofu, shaka au walakini.

Matokeo yakatolewa kidogo kidogo( Rejea uzi huu) https://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=860405.... yakianzia pembezoni

Maeneo yote yalioonekana kuwa na hali 'isiyopendeza' yakawekwa viporo

Tulitegemea utaratibu huo wa reja reja uendelee hadi mwisho

MATOKEO
Ghafla Tume ikawa imekamilisha matokeo na kutangaza mshindi. Matokeo yaliyopatikana siku moja kwa ujumla!

Palipokuwa na matatizo , Tume haikuwa na nafasi ya kujibu, kufafanua au kueleza matatizo yaliyoletwa mbele na vyama.

Ikiwa nakala za mawakala zipo, kipi kigumu kwa Tume kuoanisha taratkimu mbali mbali na zao ili kupata muafaka?

Hili la kuvuta muda na kisha kutangaza ghafla linaondoa kile kinachosemwa kuaminika kwa zoezi na wasimamiaji

Uchelewaji wa kutangaza matokeo ulikwenda sambamba na ule wa ZEC!

Kwanini kulikuwa na uharaka wa kutangaza matokeo baada ya kusuasua?

Inaendelea...
 
Sehemu ya III

MATOKEO

Zilikuwepo fununu za mgombea mmoja kwenda kupinga mahakamani matokeo ya Urais.

Kupinga matokeo si jambo lilozooeleka, na pengine lingeuweka uchaguzi katika mtihani mkubwa

Lingechelewesha zoezi la kumpata Rais lakini kikubwa ni huenda kungekuwa na ushahidi na htujui mahakama ingemuaje

Wakati huo huo ZEC walisubiri kisichojulikana tukizingatia udogo wa eneo na wapiga kura wake

Muda haukuoa nafasi kwa ZEC kuendelea na ukimya. Mh Jecha wa ZEC akafuta uchaguzi katika mazingira tata sana

Kilichoonekana ni uchaguzi wa JMT kuathirika kwa namna moja au nyingine na hali ya znz
Hayo mawili yakapelekea matokeo yatangazwe yote kwa ujumla na uharaka.

Matokeo yakaonyesha Magufuli akiwa mshindi kwa asilimia 58 kinyume na 68 zilizotolewa na CCM kutokana na takwimu ilizopata kutoka vituoni!

'Ushindi' huo katika mazingira tuliyoeleza una matatizo makubwa matatu

Kwanza, ushindi wa chini ya asilimia 60 (2/3) ya wananchi ni kidogo kuongoza taifa.

Kwa wenztu, hali hiyo hulazimu uchaguzi wa marudio.

Ndivyo ilivyokuwa miaka ya nyuma kabla Serikali za CCM kuundoa

Pili, ni ushindi huo wa ''uchaguzi huru na haki'', cha kujiuliza, process nzima ilikuwa na integrity, credibility na legitimacy?

Tatu, kuna tatizo la Watanzania kutoelewa kwanini wanapiga kura.
Kwa matokeo yaliyopo, inakuwaje mkoa wenye majimbo 9 kati yake 7 yaende upinzani na mgombea wa Urais ashinde kura za jumla?

Kwamba wanachagua sera, vyama au mtu?

Inakuwaje Mji au jiji likubali kuwa chini ya chama kimoja,lakini liongozwe na sera za chama kingine?

Nne, ushindi huo umezua mgogoro mkubwa wa katiba (Tutajadili mbeleni)

Matokeo yaliyotangazwa kukiwa na taharuki kule ZNZ yaemejenga ufa utakaoplekea taifa kugawanyika kuliko ilivyo sasa

Kwa mujibu wa Makamu wa Rais wa kwanza wa ZNZ, ZEC ni wakala wa NEC kule visiwani.

Kauli hiyo haijakanushwa na ZEC au NEC. Ikiwa ni hivyo, matokeo ya kura za Urais za ZNZ kwa JMT yamepatikanaje?

Tunasisitiz kwa mujibu wa Makamu wa Rais wa kwanza. Je, mchakato mzima bara na visiwani una integrity na credibility?

Tangazo la ZEC kwa mujibu wa Mwenyekiti na hatua za NEC kutangaza matokeo zinaiweka serikali katika wakati mgumu

Ima ikubaliane na matokeo na kupinga kauli za Mwenyekiti wa ZEC au Ikubaliane na ZEC na kufuta uchaguzi

Serikali ikikubali matokeo yatolewe, ramani ya utawala wa nchi itabadilika.

Ikikubali uchaguzi ufutwe,Rais wa JMT atakuwa amepatakina katika mazingira ya utatanishi, muungano ukiingia majaribuni

Inaendelea....
 


JE, BADO TZ NI ROLE MODEL?


Hali tete inaendelea visiwani wakati bara mshindi keshatangazwa.

Yapo maswali ya kujiuliza, Uuhaguzi huu kuanzia mwanzo hadi mwisho ulikuwa na haki?
Vyama na wagombea wote walipewa haki zako kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu?

Wapo watu wa ndani na nje wanaosema uchaguzi ulikuwa huru na wa haki.
Tunauliza tena,je una integrity na credibility? Uchaguzi unaweza kuwa huru si lazima uwe wa haki

Uchaguzi ulikuwa na msimmko ukiwa na matukio ya kisiasa yasiyokuwa ya kawaida, ukihamishawananchi kupiga kura kwa wingi

Hata hivyo, tukubaliane,uchaguzi umeacha makovu kwa taifa.

Umetuweka katika nafasi ambayo hatukuwa nayo siku nyuma katika uso wa kimataifa

Pamoja na matatizo ya chaguzi nyingi za nyuma, huu wa mwaka 2015 umeliacha Taifa katika nafasi zifuatazo

Kwanza, wapo wanahoji kama sisi ni role model ya demokrasia.

Pili, Uchaguzi umeliacha taifa limeduwaa. Shauku zimetoweka ghafla.

Yote hayo ni matokeo ya utaratibu mzima na wala si kwa walioshindwa au kushinda

Kwa mtazamo wa kawaida, taifa limeduwaa,hata mahasimu bado wanaonekana kushangaa kwa ujumla wake jambo lile lile moja. Kwamba wana kitu wanachokiona hakipo sawa ambacho ni utaratibu mzima wa uchaguzi, integrity na credibility yake

Kwa maneno mengine si wanaounga mkono CCM au Upinzani walioridhishwa na uchaguzi ulivyoendeshwa na kumalizwa

Hapa si suala la kupiga kura kwa uhuru na kutumia haki hiyo, bali integrity na credibility ya mchakato mzima

Tatu, uchaguzi umemwacha Rais mteule na kazi mgumu

Nne, uchaguzi umetia doa uzalendo, umepalilia hisia na kuharibu sana nguvu ya umoja na utaifa


BUNGE
litaendelea kutawaliwa na CCM. Spika atatoka CCM kuendeleza utaratibu wa miaka yote.
Kutakuwa wa mivutano na chuki, ubabe na kukosekana kwa mwafaka kwa mustakabali wa taifa

CCM watatumia wingi kufanya yao. Haionekani kusikilizwa wachache itafanikiwa.
Kura za ndiyooo zitatumika kuhalalisha kile kilichopo mezani hata kama hakina masilahi katika taifa

Kwa upande mwingine, iwapo kutakuwa na jambo linalohitaji 2/3 linaweza kuwepo tatizo.

Hivyo, hakuna matarajio yoyote tofauti. Sheria kama za uchaguzi na tume zitabaki kama zilivyo.
Zinaonekana kuwa 'nzuri' na wengi hawatakubali kitu tofauti. Hakuna mabadiliko yoyote

RAIS

Rais amechaguliwa na nusu ya Watanzania hata kama wapo wasioamini hivyo
Tume imetangaza kwa mujibu wa madaraka iliyopewa na katiba

Rais ataingia ofisini akiwa na Taifa lililoduwaa, chuki, hasira, vinyongo na kibaya zaidi lilogawanyika

Yote hayo ni zao la utaratibu unaonekana kutokubalika au aminika na wengi au wachache walio wengi

Tutajitia wajinga na wehu, tukijifariji uchaguzi umefikia kileleni kama ilivyotarajiwa na kwa umoja wetu

Tatizo si nani kashinda nani kashindwa bali utaratibu mzima wa uchaguzi kwa ngazi zote

Wale wanaonekana kuwa na furaha, bado furaha inaonekana kwa mshangao. Kwa ujumla ni taifa lililo katika ganzi

Lakini pia mchakato mzima umeibua mengine yaliyokuwa yamejificha na yatakayompa Rais wakati mgumu sana

Suala la ZNZ ni moja kati ya hayo

Itaendelea...
 
TARATIBU ZETU ZINA MATATIZO

Kufanya chaguzi tatu kwa wakati mmoja ni tatizo. Tunachokiona kwa mujibu wa matokeo ya tume kinahitaji fikra zaidi

Yapo maeneo diwani ni wa chama X, mbunge ni wa chama Y na Rais ni wa chama Z

Hapa panahitaji kuiuliza, hivi wananchi wanachagu sera za vyama au watu binafsi?

Kwa upande wa udiwani, inaweza kukubalika kwasababu ni serikali za miji na majiji na wananchi wanaweza kupanga mipango yao.

Kwa upande wa Ubunge na Urais lipo tatizo. Hivi wananchi wanawezaje kumchagua mbunge wa upinzani kwa kuamini sera za chama chake, wakamchagua Rais kutoka chama kingine akiwa na sera zake?

Rais atakaposema anasimamia sera za chama chake, nini nafasi ya mbunge katika kusimamia sera za chama chake?

Ndiyo maana tunauliza, je wananchi walijua wanachagua nini? Au kimetokea kitu gani hali ikawa hivyo?

UCHAGUZI WA JMT VS ZNZ

Kwamba, chaguzi hizi mbili zinaenda sambamba. Kule ZNZ, ZEC ndiyo wakala wa NEC.

Hakuna kiongozi yoyote kutoka serikalini au ZEC aliyekanusha hilo. Na haya yameongelewa na watu maarufu kama Prof Lipumba

Inapotokea tatizo kama lililopo, uchaguzi mzima unaingia dosari.

Kwa mfano, nani anaweza kutueleza kiongozi wa NEC kule ZNZ na majumuisho ya kura za Urais wa JMT zilifanyika vipi.

Tunauliza haya kwasababu ni haki yetu kujua na kuiona hali ya uchaguzi ikiwa na credibility na integrity.

Wananchi wasipofahamishwa, huja na tafasiri zao wenyewe, jambo la hatari kwani upotoshaji unaweza kutokea

Ni wajibu wa NEC kueleza bila kificho utaratibu wa uchaguzi na kura za Urais wa JMT kule ZNZ zinapatikana vipi

Katika mazingira yaliyopo ni utaratibu upi na kwa sheria zipi na taratibu gani kura za Rais wa JMT zimehesabiwa ZNZ

Hili ni jambo la muhimu sana, kinyume chake kunaweza kutokea wapotoshaji au upotoshaji na kuzua tatizo jingine

WAZANZIBAR KULALAMIKA

Wakati matatizo ya ZNZ yanaendelea na huenda suluhu ikapatikana, tatizo litarudi kuhusu namna Rais wa JMT alivyopatikana.

Wapo watakaosema huyo ni Rais wa Tanganyika, kwasababu rahisi tu, kuwa, utaratibu mzima hauonekani kueleweka.

Watakaokuwa na hisia hizo wataweza kujenga hoja nyingine kuhusu Muungano, hapo tatizo litazuka

Hilo litachagiza sana hoja ya serikali 3 kwasababu ile ile kuwa, kuwepo na mipaka ya madaraka na kwamba, Rais wa JMT awe na majukumu yake ili nchi mbili, Tanganyika na ZNZ ziweze kufanya mambo yao kutokana na mazingira yao

HOJA YA SERIKALI 3 INAPATA NGUVU SASA

CCM walipokataa serikali 3 hawakuweza kuona mbali. Hapa duru tumewahi kuhoji sana, hivi ikiwa vyama tofauti vitashinda bara na visiwani nini itakuwa hatma ya taifa?

Kwavile CCM imezoea kuongoza kwa hisia. ubabe na bila maono, hilo hawakuliona.

Leo tatizo la ZNZ linagusa Tanganyika. Kwamba, Rais anaweza kuongoza serikali ya 'umoja' wa kitaifa isiyo rasmi.
Na hasa ndicho kinapelekea CCM kugomea uchaguzi wa ZNZ

Hili ni tatizo waliloshindwa kuliona kwasababu ya kutosikiliza wananchi. Kiburi cha kuongoza

Msemaji wa CCM kwa ujumla, Bwana Mkamba alisema uchaguzi ulikuwa mzuri na kutoa tathmini ya wabunge watakaopata

Hivyo alikubali kabisa uchaguzi kule ZNZ ambako CCM ilishindana ulikuwa huru na wa haki.

Hakuna kumbu kumbu za kuonyesha kulalamikia matokeo

Leo CCM visiwani wanasema uchaguzi ulikuwa na matatizo.

Hapa taratibu tunazosema ni mbaya zinaonekana. Ni CCM ipi inayozungumza?

Ya Makamba Lumumba, au ya Kisiwandui ZNZ?



Inaendelea..
 
CCM ZANZBIBAR

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa ZEC tatizo ni ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi. CCM ZNZ wanataka uchaguzi wa marudio

Swali kwa CCM, wao wakiwa na serikali wanapaswa kutueleza, mamlaka ya mwenyekiti kutangaza kufutwa matokeo yanatoka katika kifungu gani cha sheria ambacho CCM wanakubaliana nacho?

Utaratibu wa tume kutoa uamuzi ulizingatia sheria iliyounda tume hiyo?

Ni kifungu gani kinachotoa nafasi kwa mwenyekiti na si tume kutenda jambo 'solo"?

Madai ya kukiukwa kwa uchaguzi yapo pale pale na ni haki ya CCM kama chama. Lakini, kwanza, wajitokeze na kufanunua madai ya kurudia uchaguzi na kutangazwa kufutwa uchaguzi wanayatoa wapi?

Ni lazima CCM waeleze kwanini wanakubaliana na mwenyekiti wa tume mmoja

Kinyume chake, CCM itakuwa imezaa tatizo. La kwanza, ni kutawala sehemu moja ya nchi, jambo litakalompa wakati mgumu Rais wa JMT, na pili ni kulazimisha kutawala jambo litakalozua mtafaruku kama ilivyokuwa huko nyuma

Hizo zote ni changamoto zinazomsubiri Rais aliyetangazwa wa JMT.

Tatizo kubwa zaidi si ugumu wa mtatizo, bali jinsi uchaguzi ulivyoendeshwa kukiwa na dalili zinazoashiria watu kutoridhika

MAGUFULI NA NUSU YA WAPIGA KURA

Ukiacha uatata kuwa ZNZ watahoji kuhusu upatikanaji wa Rais wa JMT, kuchaguliwa kwa nusu ya watu ni dalili ya taifa kugawanyika. Kiongozi anayeongoza taifa lililogawanyika ana wakati mgumu. Matatizo ya ZNZ ni tatizo jingine linalomsubiri

Utaratibu wa kurudiwa uchaguzi ili Rais apatikane kwa 2/3 sasa unaonekana wa maana kuliko wakati mwingine

Nguvu ya kiongozi kuongoza si kutokana na nguvu za dola, bali nguvu ya wananchi walioko nyuma yake

Kwa jinsi Taifa lilivyoduwaa na ganzi, ikitokea yale ya 1978 kule Uganda, Rais atakuwa na kazi ngumu.

Kazi ya kwanza ni kujenga umoja na kazi ya pili ni kurudisha uzalendo na kazi ya mwisho kujenga imani

Katika nyakati za dharura kama zile za 1978 na Nduli Amin, muda wa kufanya hayo haupo
 
HITIMISHO

Hakuna chochote kipya katika uchaguzi huu ambacho hakijajadiliwa.

Pengine kipya ni hali ya vyama vya upinzani kuendelea kukubali kuingia katika uchaguzi katika mazingira wanayoyajua

Si kuwa hawaungwi mkono, bali kama tuilivyowahi kuandika huko nyuma, kwa nchi yetu ushindi ni zaidi ya kura

Yapo mapungufu mengi kutoka upinzani. Wao waliamini ulinzi wa kura tu unatosha, hawakukumbuka kura zinavyohesabiwa, na uaminifu wa vyombo husika. Mwaka huu utaratibu ni tofauti na hili tuliwaeleza, hawakusikia

Kwa wananchi waliojitokeza kwa wingi, si busara kusema hamtapiga kura tena. Sauti zenu ni nusu ya uchaguzi

Kama Rais amechaguliwa na nusu basi nanyi mna sauti nusu na ni makosa kuziziba, kukata tamaa au kuendelea kuduwaa

Msidhani CCM imebadilika. Kitachobadilika ni sura tu na nyadhifa. Mfumo uliotumika kuiweka madarakani miaka nenda rudi utalindwa. Utaratibu unaotumika katika uchaguzi utaendelea.

CCM hawatakubali mabadiliko yoyote yatakayowaweka katika wakati mgumu.
Mwaka huu kuna funzo wamepata, lakini CCM ina kiburi, jeuri na dharau

Ni wajibu wa wananchi wote kwa ujumla kusima na kutaka mabadiliko bila vyama.

Mabadiliko yaanzie katika madai ya Katiba mpya itakayobadili hali iliyopo.

Wananchi wasidangaywa na ujenzi wa flyover na barabara. Ujenzi wa shule n.k. Huo ni wajibu wa serikali yoyote duniani.

Wananchi wanachotakiwa ni kudai muongozo mpya

Hivyo, hakuna namna isipokuwa dai la kwanza liwe kuandika utaratibu mpya.

Na hapa ni lazima wanaotangulia wawe wananchi wenyewe. Leo Taifa limeduwaa kila mmoja akijitazama bila kujua nini kimetokea, si kwa washindi hata walioshindwa.

Hivyo Rais ajaye akiingia ofisini, aelezwe k mgawanyiko wa taifa na dosari za uzalendo. Wananchi waitake katiba yao

Kazi hiyo isaidiwe na wabunge wa upinzani. Tayari tumneona viongozi wa CCM 'walivyoadhibiwa' katika sanduku la kura.

Yule kiongozi mzee aliyekuwa anaongoza harakati za kupinga katiba mpya, leo anakimbilia mahakamani.
Hivyo jukumu la vyama vya siasa mbali na CCM ni kuanza na namna ya kubadili utaratibu

Kazi hiyo inaungwa mkono na wananchi wengi kuliko ilivyokuwa huko nyuma. Na wakiangalia uchaguzi huu, nguvu ni zaidi

Wanasiasa wana platform ya kuzungumza, wanasehemu muhimu ya kushinikiza mabadiliko na si sura tunavyotarajia

Ili kufanikisha hillo, lazima pia kuwepo na mbadiliko katika uongozi mzima wa vyama vya wapinzani Bungeni.

Hatutegemei viongozi walioshindwa kupata suluhisho la kama tume ya uchaguzi, katiba n,k wanaweza kuja na jipya

Kunahitaji mabadiliko katika uongozi wa KUB ili ipatikane damu mpya itakayokuwa na mbinu mpya

Damu mpya itakayoongoza umma katika kutafuta kile wananchi wanachokitaka, si kwenda kwenye juisi za maembe Ikul

Wapinzani walidai mabadiliko, nao wanawajibu wa kusimamia walichokitaka. Mwaka huu KUB na timu nzima iwe mpya

Kwa Rais ajaye, Wananchi wa Tanzania hawataki kusikia idadi ya madaraja au ngisi baharini.

Wanataka utaratibu utakaoweza kuwaondoa katika hali duni iliyopo na kuwapa uhuru wa kuamua hatma ya taifa lao

Wananchi wanataka haki na usawa na hivyo havipatikani kwa kutumia maderaya na magari ya maji ya washa washa

Rais atambue kuna manung'uniko miongoni mwa jamii. Kwamba, haki inaonekana kuwa ni fadhila na wala si haki

Inapofikia vituo vya haki za binadamu navyo havipewi haki basi kuna tatizo kubwa la haki nchini

Rais atambue, taifa limegawanyika na uchaguzi umeacha makovu makubwa.

Hivyo, kazi yake si kupita mikutanoni na wana CCM wenzake wakibeza wenzao.

Watambue kuwa kuna manung'uniko makubwa ndani ya mioyo, nao pia waangalie wapi manung'uniko yanatokea. Wajiangalie kama kufika kwao hapo walipo kulikuwa ni rahisi

Ishara ya wananchi kumzomea mgombea wa Urais ni dalili nzuri kuwa, wananchi wamechoshwa na kiburi, ibabe, jeuri , ufisadi na kila aina ya uovu uliokuwepo na pengine uliopo.

Hivyo kazi muhimu ni kusikiliza wananchi si kuamua kwa niaba ya wananchi

Utaratibu wa kundi dogo ndani ya CCM kuamua hatma ya nchi umelifikisha taifa hapa.

Leo kuna matatizo ZNZ huku bara kuna manung'uniko hata kama hayasemwi.

Ni utaratibu wa CCM wa kuburuza watu na si CCM yote bali kikundi kilichopewa nguvu ndani ya CCM

Hatutegemei kubadilika chochote, muhimu ni kuelewa kuwa katika hali iliyopo, ni rahisi watu kutafuta sababu zao ili kuondoa hisia zao. Hata jambo dogo tu linaweza kuleta tafrani

Kazi ya Rais ajaye si kuangalia deni la taifa, posho za wabunge na uteuzi wa maswahiba waliosadia

Rais aliangalie Taifa kwa ujumla wake, ili ajiridhishe kuwa Watanzania wana furaha.

Ajiridhishe kuwa ganzi inayoonekana inatokana na Eli nino na si kitu kingine.

Rais aangalie umoja wa kitaifa, na ajiulize kama Taifa alilopokea ndilo lile aliloasisi Nyerere.

Ndio taifa lile lenye umoja, mshikamano, furaha hata penye dhiki, na uzalendo.

Ajiridhishe kuwa hayo yote yapo salama ndipo aanze kazi za kila siku

Kama hataridhika kwa nafsi yake, basi atambue lipo tatizo linalohitaji uharaka.

Tusemezane
 
TUNAJITAHMINI AU N BORA LIENDE,BORA KUMEKUCHA!I
Taifa linalojielewahufanya mambo kwa weledi. Hutathmini kila hatua ya jambo lililofanyika kwa uyakinifu

Uchaguziumekwisha, tunachokiona ni wasomi kuanza kutafuta nafasi za kisiasa.

Kamailivyokuwa wakati wa kampeni ambapo wasomi walishadidia takwimu zisizo namaelezo ndivyo ilivyo

Hatujiulizi kama tumefanya jambo sahihi na kwa usahihi wake. Kila mmoja anazungumziamshindi na mshindwa
Hatuzungumzii kama hatua za kupata mshindi na mshindwa zilikidhi haja na matarajio yetu.

Tunafikia hitimisho, fulani kashinda fulani kashindwa
Hakuna anayejiuliza kama taratibu zetu za kuweka serikali na bunge zilikuwa sahihi.

Tunaongelea matokeo badala ya hatua. Tunajifariji kama tumefanikiwa , bila kuona kule tulikoshindwa.

Tumebaki kuzungumzia ushindi si tathmini itakayotufikisha kwenye hitimisho la ushindi aukushindwa

Tumeso mamaoni ya msomi mmoja akitaka wagombea wakubali matokeo.

Msomi huyo hakutuezakwanini wakubali tu na kama wanacholalamikia ni sahihi au la


Msomi huyo anaungana na wengine waliokuwa bize kutuletea takwimu ziszoeleza kwanini fulani ashinde na kwanini mwingineashindwe.

Hawakuzungumzia mchakato mzima kama ulitoa fursa sawa kwa washindani

Wasomi wamebaki vijibwa' (puppet) wakitupiwa mifupa watasema chochote ilimradi tu waonyeshwe dinari

Wasomi wetu h awaongelei kwanini taifa limepigwa ganzi. Hawaelezi hatma ya umoja wetu kwakuangalia Zanzibar

Kesho Amir jeshi mkuu wa JMT anaapishwa, huku kipande anachotawala kikiwa na sintofahamu na taharuki

Hatari iliyopo mbele si ya ZNZ tu, ni ya umoja wa taifa . Leo ZNZkatika hali waliyo nayo wanajisikiaje Rais wa JMT akiapishwa?

Je, huu muungano utakuwa na matokeo gani hata baada ya vumbi kutulia kule visiwani

Watanzania hatuna utamaduni wa marejeo ‘post mortem' kubaini wapi tumefanya vema wapi tumeanguka.


Hata pale tulipoanguka tumejikita katika eneo tuliloangukia si pale tulipojikwaa. Ni taifa zima, wasomi na wasomewa!


Tusemezane






















 
URAIS NI TAASISI

HIZI HAZIKUWA DALILI NJEMA ZA UMOJA WA TAIFA

Mara nyingi Mh amesikika akitumia neno 'mimi' katika kuonyesha kama Rais

Urais ni taasisi, kama mtakumbuka siku zote viongozi hutumia neno 'sisi'

Hapa nchini Mwl Nyerere alitumia maneno 'Tumefanya, tumefanikiwa n.k.' akionyesha kama taasisi moja ya nchi na si mtu

Siku za nyuma tulizoea kusikia viongozi wakisalimia kwa neno 'ndugu wananchi' . Siku hizi ni salama za kidini

Hili linabagua watu wengine ima wa dini zisizo kubwa au za asili au wasioamini kabisa

Tunayasema haya kwasababu kauli za 'Rais ni fulani' zinazidi kuondoa utengamano wa kitaifa hasa katika wakati huu taifa likiwa limegawanyika, umoja wetu kuwa majaribuni , kukiwa na mbegu za kubaguana kiaina n.k.

Ukiangalia leo, walihudhuria sherehe hizo walikuwa wana uniform za CCM.

Hili ni dosari kubwa sana kwani Rais anayetaka kujenga umoja wa kitaifa hawezi kuwa Rais wa kundi moja.

Katika hali ya upungufu uliopo mambo haya yanazidi kujenga ufa miongoni mwetu

Rais ameomba ushirikiano kwa wapinzani ili na kwamba uchaguzi umekwisha turudi katika umoja wetu

Hapa ni wazi Rais ameona tatizo hasa ganzi na jinsi Watanzania wasivyo na furaha
Suala si furaha ya nani kashinda nani kashindwa, bali mchakato mzima unaoonekana kuwa na maswali mengi

Haaraka inayoendelea huku ZNZ ikiwa na sintofahamu hailisaidii taifa.

Mwisho wa siku itakuza tatizo lililopo hasa baada ya hali kutengemaa kule visiwani.

Katika wakati huu, kulikuwa na sababu za kuharakisha haya tunayoyaona huku sehemu ya nchi ikiwa katika tension?

Ndiyo maana tunasisitiza kuwa tatizo linalomkabili Rais si uchumi bali umoja wa kitaifa.

Hili halionekani haraka, litaonekana kadri muda unavyosonga na litampa wakati asioutarajia

Kuongoza taifa likiwa na manung'uniko, likiwa halina furaha, likiwa limegawanyika ni jambo lisilo zuri

Tukiangalia hali ya furaha za wananchi, tunaona Rais amekabidhiwa nchi katika hali inayoonyesha kutokuwa na maridhiano

Leo wapinzani wana vikao vyao, Rais anaapishwa. Hapa kuna umoja wa taifa kweli?

Tunaona jinsi jitihada zinavyofanyika kumpamba Rais, lakini ukweli kuwa taifa linaonekana kuduwaa

Taratibu zilizotumika kuendesha mambo yetu, zina walakini, na walakini huo ni taifa kuduwaa, na umoja wetu kuwa majaribuni.

Si suala la nani kashinda nani kashindwa, ni suala la utaratibu uliotumika na kwamba kila mmoja aliridhika?

Tusemezane
 
Nguruvi3 baba sioni sababu kuwapa nguvu vyama vya UKAWA kusingizia upinzani,wamesusia,sema MUUNGANO wa UKAWA. alafu duniani kote vyama vingi vikishindwa bado, hali ni ile ile kutokubali kushindwa,na kususia sherehe, hao UKAWA walijiofanya Leo kukataa kwenda Uwanja wa uhuru,ni utoto na ulaghai, nataka nione wasuse wasiende bungeni,sababu bunge limeitishwa na Rais.. yule yule wasiomtambua,ndio kaitisha kikao cha bunge
 
Last edited by a moderator:
UMUHIMU WA KUUNGWA MKONO NA WANANCHI

Mwl Nyerere aliingia katika mapambano ya kisiasa akiwa hana uzoefu wa aina yoyote
Nguvu aliyokuwa nayo ni kuungwa mkono na jamii

Nguvu hiyo ilionekana katika nyakati tofati moja ikiwa ni vita dhidi ya Uganda.
Mwl aliungwa mkono kipindi cha vita na baada ya hapo, Kauli zake ziliaminika na kusikilizwa

Hata pale alipotangaza kutokubaliana na IMF wananchi walikuwa nyuma yake
Kuungwa mkono kulimsadia katika uongozi wake. Naye alikuwa msikivu pale wananchi walipopaza sauti

Katika maraisi walioingia madarakani kwa kuungwa mkono baada ya Mwl ni Kikwete
Miaka 5 ya mwanzo aliungwa mkono bila kuhoji au kususiwa

Kipindi cha pili uungwaji mkono uipungua kutoka asilimia 80 hadi 60 kwa namba zilizopo.
Hii ni baada ya wananchi kutoridhishwa na maamuzi na hatua anazochukua akiwa kiongozi

Nguvu ya JK katika jamii ikaondoka, akabaki na nguvu za kiutawala.
Wananchi hawakumsikiliza tena , akatumia nguvu ya bunge kukabiliana na nguvu ya umma .

Matumizi ya Bunge kuwa mhuri wa serikali yakawa ndio utaratibu wa kuongoza.
Kuunda tume na hata kumsukumia mizigo waziri mkuu

Nguvu zikatumika katika Bunge la Katiba, na nguvu ya umma ikawa kubwa. Katiba ikafa

Mambo yanayobaki kama legacy mbaya ya JK ni katiba . Mipango ikawa ya maguvu na mingi kushindwa

Matumizi ya bunge yakaingia nyongo, wananchi wakaichukia CCM kuanzia hapo.

Tuliona CCM ikiogopa kutumia jina hilo . katika uchaguzi. Ikawa Chagua Magufuli. CCM ilijua gharama za ubabe wa bunge ni kubwa.

Mawaziri waandamizi wakaadhibiwa kwa kura, Mmoja ni yule kinara wa sera za serikali anayelipa gharama kubwa

CCM imepoteza hata kwa takwimu zao. Wamepoteza wabunge na ushindi wao ndio huo huo na hivyohivyo

Rais Magufuli ameshuhudia chuki ya umma katika kampeni. Amezomewa, mikutano ya kubeba watu n.k

Inaendelea....
 
Inaendelea...


Hapo juu tumeonyesha jinsi bunge la CCM lilivyoadhibiwa kutokana na ubabe au shinikizo la serikali yake.

Mikoa na majimbo matiifu kwaCCM imeafanya ‘uasi'.


Hakuna alitegemea chama cha CUF kuwa na idadi ya wabunge iliyonayo ikipora CCM

Miji na majiji makubwa yataongozwa na wapinzani.
Kwa takwimu zilizopo za uchaguzi (ndizo zinzotakiwa kutumika kisheria) kuna maswali DktMagufuli anatakiwa kujiuliza.


Hivi inakuwaje apate kura za Urais apoteze mbunge katikajimbo hilo hilo?


Je, wananchi walimchagua kama mtu au mbeba sera wa CCM?

Kwanini ilikuwa chagua Magufuli na si CCM?

Je bado anadhaniCCM ina nguvu ya ushawishi kama ilivyokuwa siku za nyuma? Je, zomea zomeaimetokana na nini?


Zomea zomea kilikuwa kipimo kizuri cha jinsi gani wananchi walivyochoka.


Rais amekumbana nayo,na amekumbana na nguvu ya umma katika kampeni.

Kutawazwa kwake kuwa Rais hakufanani na mazoea yaWatanzania.

Nchi imegawanyika, na kuna manung'uniko yasiyo rasmi yanayoonekana.

Tunaijua Tanzania na ni rahisi kwetu kuona tatizo.

Umoja wa kitaifa haupo, na hilo litapelekea kupotea kwa uzalendo na kutoungwa mkono


Katika mazingira haya, Rais anapaswa aanze na kazi za kulileta taifa pamoja.

Kazi ya kurudisha umoja wa taifa, kuwasikiliza wananchi na kutenda haki.

Hilo ndilolitamsaidia kupata kuungwa mkono.

Kutegemea nguvu za vyombo vya dola au bunge kutamrudisha kule alipoachia mtangulizi wake


Kwa kuanzia, Rai yetu kwa Rais ni kuwa, uchaguzi umepita na ameshakuwa Rais.

Ndiye mwenye mamlaka makubwa kwa mujibu wa katiba yetu ya1977, katiba inayolalamikiwa

Ili kurudisha umoja wa kutaifa, ni vema angeondoa kesi za uchaguzi zilizopo mahakamani

Kuendelea kuwa na kesi, ni kuwakumbusha wananchi machungu ya sheria za kibabe zinazotumika kuwatia watu matatani.

Sheria zile zile zilizopitishwa na bunge la CCM ililoonekana kukataliwa na wananchi.

Tumesema, ikiwa kampeni ilikuwa ni ya mtu na si chama, lipotatizo.

Ikiwa mgombea anashinda Urais na ubunge au udiwani kwenda kwingine, lipo tatizo

Kufuatia hali ya ganzi iliyopo nchini, na matatizo yaliyojitokeza kwa baadhi ya taasisi, NGO na watu binafasi, njia bora ya kuliponya taifa kutokana na makovu ya uchaguzi ni kuanza upya

Kuanza upya ni pamoja na kuondoa kesi za uchaguzi.

Rais ameshapatikana kuendelea na malumbano ya uchaguzi iwe mitaani au katika vyombovya sheria ni kuendelea kulitia taifa ganzi na kuligawa zaidi.


Ni kupalilia chuki zilizotokana na uchaguzi ambazo zitazidi kulipooza taifa achilia mbali kuligawa

Tusemezane
 
Nguruvi3 baba sioni sababu kuwapa nguvu vyama vya UKAWA kusingizia upinzani,wamesusia,sema MUUNGANO wa UKAWA. alafu duniani kote vyama vingi vikishindwa bado, hali ni ile ile kutokubali kushindwa,na kususia sherehe, hao UKAWA walijiofanya Leo kukataa kwenda Uwanja wa uhuru,ni utoto na ulaghai, nataka nione wasuse wasiende bungeni,sababu bunge limeitishwa na Rais.. yule yule wasiomtambua,ndio kaitisha kikao cha bunge

Wapinzani wamesema hawamtambui Rais?
 
Hapa kuna video moja inayorueleza jinsi uchaguzi unavyofanyika ZNZ

Kwa ufupi, wznz wanapiga kura 5 kwa wakati mmoja

3 Zinawahusu wazanzibar ( Rais wa SMZ, Wwawakilishi na madiwani)

2 Zinahusu JMT (Rais wa JMT, wabunge kutoka ZNZ wanaoingia JMT)

Chumba cha kupigia kura ni kimoja, na wenye daftari za wapiga kura wa ZNZ ni ZEC, na kuna kidaftari cha wote (bara na visiwani)

Hapa ndipo mkanganyiko kama si mchanganyiko unapoingia

Hoja ya ZEC kufuta uchaguzi ni uwepo wa wapiga kura wengi kuliko ilivyotarajiwa

Kama walikuwa ni wale wa walioandikishwa na ZEC then, athari zake zitagusa NEC kwasababu ni hao hao wameshiriki uchaguzi wa JMT ikiwemo Rais na wabunge wao

sikiliza

http://mzalendo.net/habari/videomaada-moto-katiba-ya-zanzibar.html
 
Katika video hapo juu, wazungumzaji wameeleza hoja moja wengi hatuizingatii

Kwanza, wameuliza ni kifungu gani kinaipa tume ya uchaguzi nguvu za kufuta uchaguzi? Hili swali CCM hawana jibu

Kuna hoja ya wananchi kwanini JK alikaa kando na kuwaachia mkuu wa majeshi.

Tunajua katiba ya JMT inasema, Rais wa znz ni mjumbe wa baraza la mawaziri la JMT.

Sasa ikiwa Seif ni Rais, atalazimika kuingia katika baraza hilo lenye CCM.

Hapo ndipo ganzi inapoingia? Watawezaje kufanya mambo yao gizani?

Haya yote yameletwa kwa ubabe wa CCM. Waliamini kuwa wataendelea kutumia vyombo vya umma kutawala milele

Hawkujua ipo siku umma unaweza kuamua tofauti. Leo hii kuna tatizo kubwa sana kule visiwani linalogusa JMT

Tatizo linalotishia muungano kwasababu hali ilivyo Rais wa JMT amepataikana katika mazingira yaisyoeleweka na wananchi. Inakuwaje kuwepo na wapiga kura wengi ambao hawakuathiri uchaguzi wa JMT?

Na kama ni hivyo, uchaguzi ukifutwa kama wanavyodai huku bara utafutwa?

Kama sivyo, huyo mpinzani ataingiaje vikao vya juu vya serikali ya JMT ambayo ni ya CCM ?
 
Back
Top Bottom