Twin Tower
JF-Expert Member
- Jan 13, 2023
- 2,133
- 2,986
Wakuu salam!
Hili jambo nimeshalilalamikia kipindi cha nyuma lakini naona sasa imekuwa kero.
Binafsi nilisajili namba ya airtel na kuiweka katika simu. Muda wote ipo kwenye simu ila nikaswitch single line use.
Nakuja kutaka kuitumia haisomi kwangu, najaribu kuipiga inatumiwa na mtu mwingine.
Leo pia namtafuta mtu sikuwa nimewasiliana nae muda mrefu anapokea mtu mwingine.
Huu nachukulia ni udhaifu mkubwa sana unaendekezwa hasa na TCRA katika kuwa simamia hizi kampuni za simu.
Kubadilisha kwa sababu yeyote ile bila ridhaa ya mwenye namba alieisajili ni uhuni tu.
Kama wanaona haitumiki wafanye jitihada za kushawishinwateja ama ziwe suspended kama wanadhani kuna shida yeyote ila sio kuhamisha matumizi kwa mtu mwingine.
Najua kuna wafanyakazi wa makampuni hayo humu achilia mbali TCRA fikishenu huu ujumbe.