SoC02 Mitandao ya kijamii: Fursa za kimazingira na kijiografia kwa wanafunzi wa vyuo vikuuu, Gundua fursa zisizoonekana

Stories of Change - 2022 Competition
Jul 31, 2022
13
9
Mitandao ya kijamii ikiwemo jamii forums,twitter, linkedin, instagram, facebook n.k vimekuwa nyenzo mhimu katika kutoa habari za ki-eliumu, mazingira, afya, uchumi, kilimo, biashara, jamii, tamaduni, siasa na michezo.
hivyo hutoa nafasi ya kufuatilia mafunzo maalumu na kumuwezesha mfuatiliaji kupata maarifa na ujuzi mahususi.

Kwa kipindi cha miaka kumi na tano nyuma mpaka sasa kuna ongezeko kubwa la watumiaji wa simu janja . Pia, idadi kubwa ya wanafunzi wa elimu ya juu kwa sasa hapa nchini wanamiliki na kutumia simu janja, ambapo huwawezesha kujisajili katika mitandao ya kijamii kutegemeana na ufahamu wa matumizi au mapenzi ya kufuatilia machapisho na watu mahususi.

Kwa upande mwingine wanafunzi kutegemea na mahala au miji vilipo vyuo wanakosoma au maeneo wanakozaliwa huzungukwa na fursa za kimazingira na kijografia ambazo ni muhimu katika safari zao za kitaaluma, kitaalam na za kijasiliamali, fursa hizi ni pamoja na kuwepo kwa taasisi, makampuni na mashirika ya ndani ya nchi na ya kigeni yanayojihusisha na shughuli mbalimbali, shughuli za watu binafsi, za vikundi mbalimbali katika jamii, semina, makongamano, matamasha mbalimbali na mafunzo maalum yanayoendeshwa katika mazingira hayo. Kwakuwa idadi kubwa ya wanafunzi hutokei maeneo ya vijijini hivyo hukumbwa na matumizi yasiyo ya tija lakini hata wale wanaotokea mijini bado wanahitaji kupata elimu zaidi ya matumizi bora.

Rasilimali hizo hazijatumiwa kikamilifu na wanafunzi walio wengi mathalani kabla, baada ya kujiunga na baada ya kuhitimu masomo, rasilimali hizo zinaweza kutumika kupata ujuzi, maarifa na kama jukwaa la mijadala ya kubadilishana mawazo kuhusu changamoto za kitaifa ikiwemo ajira, usalama hafifu wa chakula, maji safi, mabadiliko ya tabia ya nchi, uchafuzi wa mazingira, demokrasia, usawa wa kijinsia, afya, uhuru wa habari, kujieleza na haki za ki-binadamu. Kwa nyongeza, rasilimali hizo ni mhimu katika kuukabili ulimwengu wenye fursa shindani.
Ufafanuzi wa wazo
1. Kivipi wanafunzi wawezeshwe kufahamu matumizi bora ya mitandao ya kijamii?

2 . Wanafunzi wanawezaje kutambua na kutumia fursa za kimazingira zinazowazunguka?
Wazo linalopendekezwa ni;
Wanafunzi Kufikia ujuzi na maarifa yanayopatikana katika mitandao ya kijamii na yanayotokana na fursa za ki-mazingira/giografia huska.

Wazo hili linahitajika katika jamii ya wanafunzi kwa sababu ya Uhitaji mkubwa wa maarifa na ujuzi mchanyiko katika soko la ajira/kujiari, pia wazo hili linawezekana kwa sabubu? 1. Wanafunzi wanao uwezo wa ufikiaji wa mitandao ya kijamii kwa kutumia simu janja zao 2. Wanafunzi wako kwenye tabaka la jamii ambalo lina utayari wa haraka wa kujifunza na kupata maarifa husika 3. Kuwepo kwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknologia 4. Kuwepo kwa Wizara ya Sanaa,habari na michezo 5. Kuwepo kwa shughuri mbali mbali zinazofanyika katika mazingira waliyopo wanafunzi

Malengo makuu ya wazo hili ni Wanafunzi wa vyuo vikuu kuweza;

1. Kuunda mitandao na miunganisho (Creating network and connections) kupitia;
  • Kufuatilia wasifu wa watu ambao ni waandamizi wenye ujuzi katika eneo husika na kuunganika nao
  • Kufuatilia wandamizi wa kitaaluma kama vile wenye shahada za uzamili na uzamivu katika vyuo vya ndani na nje ya nchi.
  • Kufuatilia wanataaluma kama vile Maprofesa na wahadhili katika vyuo au wanafanyakazi waandamizi katika taasisi na makampuni mbali mbali.

2.Kuhudhuria kozi au mafunzo maalumu kwa njia ya mtandao
  • Mafunzo/kozi mbalimbali huchapishwa na kuendeshwa kupitia akaunti za mitandao na wavuti za vyuo vikuu ndani na nje ya nchi, taasisi mbalimbali, makampuni na watu binafsi
  • Mafunzo haya huweza kuendeshwa kwa mfumo wa mfululizo wa wavuti (webinar series), mikutano ya mtandaoni (online conferences), warsha au kozi za majira ya joto (summer course)
  • Kozi/ mafunzo huweza kutolewa kwa mda maalumu kama vile mara moja au mfuatano wa mada kwa kipindi fulani kutegemea waandaaji
  • Mwanafunzi anaweza kufuatilia matangazo ya mafunzo/kozi hizo, kujisajili na kushiliki
3. Kufikia fursa za kimazingira na kijiografia
  • Mazingira yayowazungunguka wanafunzi aidha wawapo vyuoni au maeneo wanakozaliwa/ishi huwa na shughuli za kitaasisi,makampuni,mashirika, watu binafsi na za kijamii.
  • Mwanafunzi anaweza kuainisha mazingira yake aliyopo akatambua shughuli zinazompendeza au masuala ambayo ni mtambuka kwa jamii.
  • Kushiliki katika masuala ya kijamii kunamfanya mwanafunzi kutambua changamoto zilizopo na kuchangia majibu.
  • Kwa kutambua shughuri zilizopo, mwanafunzi aweza kuandaa maombi ya kujifunza namna shughuri zinavyoendeshwa wakati akiwa katika likizo.
Faida kuu za matumizi bora ya mitandao ya kijamii na fursa za kimazingira na giografia kwa wanafunzi wa vyuo vikuu

  • Mwanafunzi atapata maarifa na ujuzi, ikiwemo ujuzi wa kuwasiliana na kuunda mtandao wa marafiki wa kimataifa au kikanda. Baadhi ya waandaaji wa mafunzo/kozi za mtandaoni hutowa vyeti vya ushiliki ambapo huboresha ukuaji wa kitaaluma, kibinafsi na wasifu wa mwanafunzi, mwanafunzi awapo chuoni na kutafuta kupitia google kujisajili katika tovuti za Coursera, Edx, Udemy, Khan academy, Itunesu free course, Mit opencourseware, Stanford online, Open culture online courses, n.k atapata nafasi ya kufuatilia mafunzo/kozi maalum kutegeamana na kada anayopendelea na anaweza kujiunga na kozi nyingi kadri awezavyo ili kupata maarifa,ujuzi na kukuza wasifu wake
  • Kushiliki shughuli katika mazingira huska itampatia mwanafunzi nafasi ya kupata uzoefu wa kazi/biashara, kuboresha ujuzi wa kitafiti, utatuzi wa changamoto na hatimae kuboresha wasifu wake ampapo itamrahisishia kukabili fursa za ndani na nje ya nchi zilizoko mbele yake.
Hitimisho

  • Wizara ya elimu, sayansi na teknologia, Wizara ya Utamaduni Sanaa, na michezo Pamoja na Wadau mbalimbali wa Elimu na Tehama wanapaswa kuboresha sera ya matumizi ya Tehama Nchini kwa wanafunzi kuanzia ngazi za awali, pia katika mitaala ya elimu liwepo somo ya Matumizi ya mitandao ya kijamii kuanzia vyuo vya kati mpaka vyuo vikuu.
  • Vyuo vikuu kwa kushirikina na serikali za wanafunzi vinapaswa kutoa elimu elekezi ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii, pia uongozi katika maeneo ambapo wanafunzi wanasoma au wanaishi unapashwa kuwapa nafasi ya kushiliki katika shughuli ili wajifunze
  • Serikali kuu inapashwa kuweka sera elekezi kwa mashirika ya umma na yasiyo ya umma kutoa nafasi za kujitolea kwa wanafunzi ili kujifunza. Endapo elimu bora ya matumizi ya mitandao na mazingira itatolewa itasaidia kujenga ujuzi kwa wanafunzi kushiriki kikamilifu kuchangia majibu ya changamoto za taifa na kushika fursa za ndani na nje ya nchi.
 
Back
Top Bottom