Mistari ya antivirus ndani ya maisha club kesho tar.29-01-2012.

Mchaka Mchaka

JF-Expert Member
Jul 20, 2010
4,516
1,404
Januari 29, 2012, Sugu atawaongoza wanaharakati kibao katika shoo babkubwa itakayofanyika kwenye Klabu ya New Maisha, Oysterbay, Dar es Salaam.
Sugu ameandika kwenye ukurasa wake wa Facebook: “Watu wote waje waone mi-swagga ya Vinega. Tutapiga shoo babkubwa. Kama kawaida yetu huwa hatufanyi tusichoweza. Tukisema tunafanya, ujue tunaweza kufanya na tunafanya.”
Mratibu wa shoo hiyo, Fred Mariki ‘Mkoloni’ amesema kuwa katika shoo hiyo, itakuwa muafaka kusikiliza mawe yaliyomo kwenye mixtape za Anti Virus volume I na II.
Alisema, shoo hiyo ni mwanzo tu, kwani nyingine nyingi zitafuata kwa sababu wamepewa shavu la miezi sita kwenye klabu hiyo.
Aliongeza kwamba kwa kuanzia, Januari 29, watafanya shoo baadhi ya Vinega wakiongozwa na Sugu, kisha mwezi ujao, watapiga kazi wengine.
Aliendelea kusema kuwa Januari 29, mbali na Sugu, wengine watakaoshika mic ni Mapacha, Anselm Ngaiza ‘Soggy Dog’, Suma G, Daniel Kamili ‘Dani Msimamo’, Happy Thadei ‘Sister P’, DJ Snox wa Mabaga Fresh na Mkoloni mwenyewe.
Alisema kuwa ndani ya Club Maisha, itakuwa muafaka kumwaga mistari ya Anti Virus mwanzo mwisho na Vinega wote wamejipanga kwa ajili ya kazi hiyo.
 
kama kawaida yao VINEGA hakuna kuremba kazi kama kawa si wadau tupo pamoja
ONE LOVE.....'.,'
No apology.
 
Back
Top Bottom