Makala maalum ya vinega

mpenda pombe

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
1,385
681
oma Makala ya mdau wa harakati za Anti-Virus iliyotumwa kwa KaribuNdani leo Alhamis saa 19:30.

ovement ya Anti-Virus ilianzishwa kimya kimya na Mapacha Wa Maujanja Saplayaz baada ya kulalamikia unyonyaji uliopitiliza katika kituo kimoja cha redio jijini Dar es Salaam. Wakiwa wawili tu Magenge ya Mwenge waliweza kuwahamasisha wadau wa muziki na punde harakati zao zikaanza kushika kasi na jina la Anti-Virus kuzaliwa rasmi. Kupigana kwao na misimamo yao kupinga unyonyaji ilipelekea kuwavutia wasanii wengine nguli akiwemo Mheshimiwa Joseph Mbilinyi aka Sugu ambaye kwa kiasi kikubwa alikuja kuzikuza sana harakati hizi za Anti-Virus. Kuingia kwa Sugu katika movement kulikusaidia kuwaleta wasanii wengine wengi ambao wengine pengine walikuwa wakiogopa kutokana na vitisho vya kubaniwa nyimbo zao na kunyimwa show au pengine hawakuona kama kuna chochote kitakachobadilika.

Baada ya Anti-Virus Vol One kutoka na wasanii kadhaa kuingia kwenye harakati, Volume Two ya mixtape ya harakati ikaanza kuandaliwa. Ndani ya volume two wasanii kibao waliingiza sauti akiwemo Sugu, Rama Dee, Magenge wenyewe, Peen Lawyer, Adili, Soggy, Suma G na production ilisimamiwa na Kijana Chapakazi studio chini ya mzalishaji mkongwe Profesa Ludigo na bwana mdogo producer Safi Gushu. Listening session ya Anti-Virus Vol 2 ilihudhuriwa na wasanii kibao na wadau kadhaa. Baada ya hapo Vinega wakapata sapoti ya kuueleza umma hadharani juu ya madai yao ya unyanyasi na unyonyaji dhidi ya kituo kimoja ambacho hawakusita kukitaja wazi kwenye mixtape.

Hayo yalikuwa mafanikio ya aina yake. Vinega wakiwa na sapoti kubwa ya wananchi walifanya onesho la kipekee katika viwanja vya Ustawi wa Jamii mwaka 2011. Ingawa waliwekewa mizengwe kadha wa kadha ikiwemo Adili Hisabati kutaka kukamatwa kwa kisingizio cha kumtishia DMX (nguli wa Hipphop Marekani ) kiasi cha kushindwa kuja Bongo. Pamoja na yote Anti-Virus ilisonga mbele kwa mafanikio. Walisambaza ujumbe kila kona ya nchi kwa kutumia mitandao ya jamii pamoja na live performances

Mafanikio ya Anti-Virus Movement. Hadhi kwa wasanii wote na heshima kwa redio zilizotoa sapoti kwa harakati. Kila mtu anajua kuwa Anti-Virus Movement imeleta hadhi kwa wasanii.Juma Nature ambaye hakushiriki show ya Anti-Virus na kushiriki shoo nyingine iliyofanyika siku hiyohiyo, alidai kuwa alilipwa milioni moja kiasi ambacho hakuwahi kupewa siku za nyuma. Afande Sele, ambaye kwa wengi walitegemea angekuwa mwanaharakati madhubuti lakini haikuwa hivyo, naye alisema alilipwa Laki nane kiasi ambacho ni kikubwa hivyo asingeweza kukiacha. Hayo ni mafanikio ambayo Sugu aliweka wazi ndio kisa cha kuwepo kwa Anti-Virus. Ushindi kwa Vinega ni kuona wasanii wanapata malipo mazuri haijalishi wako ndani au nje ya movement. Kikubwa ni kuboreka kwa maslahi na kuondoa unyanyasaji katika industry.

Mafanikio ya Anti-Virus yaliendelea kuonekana hata baada ya show ya uzinduzi . Stamina akishiriki tamasha kubwa la Fiesta linaloandaliwa na Primetime kupitia kituo chake cha Clouds Fm, alidai kuwa sasa wasanii wanalipwa vizuri kwenye shoo hizo. Yeye mwenyewe anakiri kupokea kitika hadi cha milioni 1 kwa kwa kutoa huduma yake kwenye tamasha hilo. Kwa ufupi maisha ya wasanii yamebadilika in terms of performance fees wanazolipwa.

Tuzo za Kili. Ikumbukwe kuwa hizi tuzo zilizonekana kuwabagua wasanii baadhi hasa hawa waliokuja kujiunga na harakati. Hivyo kwa Rama Dee kushinda tuzo ile ilikuwa ni mafanikio makubwa kwa vinega na Anti-Virus Movement.

Upande Wa Redio Stations Anti-Virus imesababisha vituo kadhaa vya redio kupata umaarufu na kukubalika zaidi. Hapo awali isingekuwa rahisi kwa Show kama ya Azonto kujaza kiasi kile. Hapo kabla iliaminika kituo kimoja tu cha redio ndio kinaweza kuandaa shoo kubwa na kuleta wasanii wakubwa na kupata mafanikio. Kwa bahati nzuri sana, Anti-Virus ambayo hakuwa na msanii wa nje hata mmoja, na ambayo iliandaliwa kwa sapoti ya wananchi na vituo vichache vya televisheni na redio, ilifanikiwa sana na kujaza sana kiasi cha kuishinda hata shoo iliyofanyika siku hiyo hiyo ambapo kulikuwa na wasanii waalikwa toka Marekani huku mmoja akishindwa kutokea. Haya ni mafanikio, sasa watanzania hawaangalii chombo gani cha habari kimeandaa tamasha. Wanachojali watanzania ni burudani. Ndio maana tunaona hata Eric Shigongo anafanya matamasha na hakosi watu.

Dalili za Kufa kwa Anti-Virus Movement Vinega walishtushwa na kupatana kwa Sugu na Ruge kitu kilichotafrisiwa kama usaliti na unafiki katika movement. Sugu ambaye baadae aliwaomba msamaha vinega inasemekana alishinikizwa kufikia maamuzi yale. Hata hivyo, damage au uharibu alioufanya kamwe hakuwezekana kurekebishwa. Hapo dalili za kufa kwa Anti-Virus Movement zilianza kuzaliwa. Kulikuwa na kutofautiana miongoni mwa supporters wa movement hiyo. Public haijui lakini watu waliokuwa wakiisapoti hii movement walianza kuondoka kundini.

Hata hivyo, Sugu aliendelea kutetea haki za wasaniii na hilo linajionesha pindi Mapacha walipofunguliwa mashtaka na mmoja wa mahasimu wao. Sugu alipaza sauti kuwaponda aliopatana nao na kudai hakuna kilichotekelezwa katika makubaliano yale. Ilipotokea bifu jipya la Lady Jaydee na kituo hicho cha redio na kupelekea Anaconda movement kuzaliwa, Sugu aliwaita bungeni vinega wakiongozwa na Mkoloni na Rama Dee pamoja na Anaconda chini ya Lady Jaydee na Profesa Jay. Katika hotuba yake aliyoisoma bungeni mwaka wa fedha 2013/2014 Sugu alirudisha na kujenga imani kwa supporters wa Anti-Virus na Anaconda.

Hata hivyo, ni Anaconda waliopata nguvu zaidi kwa safari hiyo ya Dodoma ikiwa ni pamoja na kufanya show kubwa iliyojaza kiasi cha watu kuzuiliwa mlangoni. Show ilipewa jina la Miaka 13 ya Lady Jaydee na kama kawaida upande wa pili walijaribu kuvuruga hii show kwa kumpa MwanaFA aibu ya mwaka.

Sababu hasa za Anti-Virus kupotea kama sio kufa kabisa Kuna vitu kadhaa vimechangia kufa au kupotea kwa Anti-Virus Movement. Hizo sababu ni pamoja na;

1. Kukosekana kwa Mpango Mkakati (Strategical Plan), Katiba, Article of Association au MOU kati yao kumeigharimu movement. Tatizo kubwa lililoifanya Anti-Virus kukosa uhai ni kujiendesha kienyeji. Vinega walipoingia vitani hawakuwa na sustainable plan (mpango endelevu), hawakuwa na makubaliano kati yao (Memorandum of Understanding-MOU), hawakuwa na tamko la umoja na pia hawakuwa hata na katiba ambayo ingewapa sehemu ya kurejea kila wanapokwama.

Matokeo yake walikuwa wanapigana vita pasipo kujua mwisho wake, au mipaka ya vita yao. Na ilipotokea ushindi umepatikana kwa kishindo wakashindwa kujiendeleza kibiashara. Duniani kote watu huangaika kupata platform (jukwaa). Vinega walifanikiwa kupata jukwaa ambalo kama wangelitumia vizuri wangepata mafanikio zaidi. Lakini cha ajabu walishindwa kufanya kazi ilihali walishajihakikishia support kwa media.

Rama Dee ndiye msanii pekee ndani ya Anti-Virus aliyeonekana kutumia vizuri fursa. Alifanikiwa kujitangaza zaidi kupitia Anti-Virus akafanya muziki mzuri na hatimae akapa tuzo. Inawezekana kabisa Rama alikuwa na plan A,B na pengine hadi C. Ndio maana mpaka leo hii Rama Dee ndiye aliyefanikiwa zaidi baada ya movement kati ya vinega wote.

Kukosekana kwa mipango madhubuti kuliwakosesha vinega fedha nyingi amba wangetumia kujiendesha. Hakuna harakati yoyote duniani isiyokuwa na faida. Wala usiende mbali, hebu waangalie Anaconda tu, pengine bila harakati yao show ya Miaka 13 ya Lady Jaydee isingefikia mafanikio yale. Vinega hawakutumia fursa waliyotengeneza wenyewe. Hawakujaribu hata kutafuta wataalamu wa biashara wawape Business Plans ambazo zingewafanya wazidi kusonga mbele.

2. Usela mwingi Baadhi ya Vinega usela ulizidi. Si vibaya kuwa masela kama hiyo ndo identity (utambulisho) ya harakati but lazima vitu vya msingi viamuliwe kwa busara na sio usela. Wakati wa maamuzi ya msingi sana, vinega walipendelea kukaa Bar na kunywa huku wakijadili. Kamwe pombe isingeleta mawazo ya kuboresha harakati.

3. Uongozi Ukiulizwa sasa hivi kiongozi wa vinega ni nani, bila shaka hutakuwa na jibu sahihi. Kukosekana kwa uongozi ni sababu mojawapo ya kupotea kwa harakati. Haikuwa rahisi kupata taarifa za harakati, hakuwa rahisi kuandaa vikao vya pamoja na ilikuwa shida kujua nani hasa ni memba wa kudumu wa Anti-Virus. Hakuna uongozi, hakuna taarifa.

4. Majukumu binafsi na Safari za Rama Dee na Peen Lawyer Lazima tukubali wachache walijua kutumia fursa iliyopatikana. Fursa hii ilipelekea vinega kadhaa kupata michongo mbalimbali. Mkoloni alikwara ajira yake ya kudumu Times FM kutokana na uwezo wake katika event planning and management. Mkoloni alikuwa mstari wa mbele sana kwenye harakati. Ubize wake umechangia kuififisha harakati, amebanwa na kazi na majukumu binafsi hivyo inamuwia vigumu kujigawa.

Rama Dee amehamia Australia na kurudi Bongo ni mara moja kwa mwaka na hukaa kwa muda mfupi. Kutokana na mchango mkubwa wa Rama Dee wa hali na mali, movement inakosa uimara. PeenLawyer ni kinega ambaye mchango wake ulikuwa haukwepeki, kwasasa anaishi Germany. Peen alikuwa kichwa cha Anti-Virus katika graphic na promotion. Ikumbukwe Anti-Virus Vol 1, kwa mara kwanza katika historia ya harakati, ilikuwa ikipatikana katika Swahili Original website pekee ambayo inamilikiwa na PeenLawyer.

Adili Hisabati alikuwa kiungo muhimu kwa vinega, alishiriki kwenye production zote mbili. Ye mtengeneza za video jingles and pia rapa katika mix tape. But mchizi alihamishia makazi homeland Mbeya Green City. Kule aliendelea na harakati akiwa na Salu T lakini hiyo ilitosha kuua nguvu ya Anti-Virus.

5. Rumours Baadhi ya watu wanadhani hii movement ni ya Sugu hivyo vinega wanafanya kazi za mbunge huyo. Hiyo imewavuruga na kuwavunja moyo baadhi ya vinega. Kinachofahamika ni kwamba Sugu ni kinega muhimu wa harakati kutokana na nafasi yake kitaifa. Lakini haimaanishi yeye ndo kila kitu. Kuna watu walikuwa na mchango mkubwa sana kama Rama Dee, Adili Hisabati, Mkoloni na Profesa Ludigo.

Hitimisho Siwezi kusema kuwa harakati ndo zimeishia hapo kwasababu ya hizo sababu au kwasababu ya usaliti mwingine uliofanywa na Mapacha hapana. Harakati zitasimama tu baada ya kufanikiwa kumaliza kabisa unyonyaji na unyanyasaji. Ni kweli kabisa Mapacha ama Magenge wamekosea na kila mwanaharakati na kinega wa kweli amechukizwa kwa hilo. Lakini wao sio sababu ya kushindwa kwa harakati.
 
binafsi nilipata hasira sana... baada ya kirusi kuingia kwenye hii ANTIVIURUSI....

wasaniii hawana umoja hii ndio jibu fupi sana...

nilifuatilia hii movement.. ila mwisho wake duuuh...
sina mengi leo...
 
Umri umesonga, majukumu yameongezeka. Hawawez kuwa kwenye harakati ambazo haziwanufaishi zinawakosesha fursa tu.

Mkumbuke wengi hawajasoma pia lazima mjue tuko dunia ya ubepari.
 
Vinega wamesambaratika,wanashindwa hata na mwanamke Jide,kasimama mwenyewe mpaka sasa

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
kwa mara ya kwanza i lke what you wrote
Umri umesonga, majukumu yameongezeka. Hawawez kuwa kwenye harakati ambazo haziwanufaishi zinawakosesha fursa tu.

Mkumbuke wengi hawajasoma pia lazima mjue tuko dunia ya ubepari.
 
Hawa Vinega hovyo kabisa sasa wana baki kulia hata jide kawashinda.

Bora wameomba msamaha pengine walikuwa na hali mbaya.
 
binafsi nilipata hasira sana... baada ya kirusi kuingia kwenye hii ANTIVIURUSI....

wasaniii hawana umoja hii ndio jibu fupi sana...

nilifuatilia hii movement.. ila mwisho wake duuuh...
sina mengi leo...
Hakika
 
Umeandika vizuri sana... hongera hapo baadhi ya watu waliodhani ni uhuni wameelewa kidogo....salute..
 
Walikua hawajui wanatafuta Nini

Pia waulize mapacha THT walienda kufanya Nini ?..na wameambiwa Nini ? ...
 
Wasanii wengi wanaojiita wanahiphop ni aggressive sana..
Na matusi kwao ndo medium of communication!
Waendelee na hizo harakati zao wauziane copy chumbani,zikienda mbali sana nyumba ya jirani!
 
Wasanii wengi wanaojiita wanahiphop ni aggressive sana..
Na matusi kwao ndo medium of communication!
Waendelee na hizo harakati zao wauziane copy chumbani,zikienda mbali sana nyumba ya jirani!

Kula tano....ila ushauri huu kawape pale KIRINGENI
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom