Misri yapeleka Jeshi mpakani kukabiliana na uchokozi wa Israel

Webabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,183
10,917
Kimya kingi kina mshindo. Hatimae nchi ya Misri imeamua kuongeza askari wake maeneo ya mpaka wa Rafah na lango la Karem Shalom.

Uamuzi huo umekuja baada ya maonyo ya awali na kufuatia taarifa ya jeshi la Israel kwamba liko mbioni kupeleka askari wa miguu eneo la Rafah walipojikushanya wapalestina zaidi ya milioni 1 waliokimbizwa kutoka maeneo mengine ya jimbo la Gaza.

Kazi za mwanzo za jeshi la Misri itakuwa ni kuziba matundu ya kuta na seng'enge ambayo yalisababishwa na Israel miezi miwili iliyopita iliposhambulia sehemu hiyo kutokea angani.

Shambulio hili lililobomoa sehemu za makuta hayo lililfanyika wakati Israel ilipokuwa ikishinikiza kuwasukuma wapalestina waingie nchini Misri.

1707796509119.png

1707796555334.png

Egypt reinforces security presence along Gaza border

Israel anataka wafukuza wapalestina waondoke katika nchi yao ndo mana anaharibu mpaka wa misri ili wapalestina waondoke na wakiondoka hataki warudi.
Hata pale Misri si ni kama kwao, ni kwa ndugu zao wa kitabu na imaan. Inabidi Misri ifungue mpaka iwapokee na kuwahifadhi na dhiki inayowaandama.
 
Namna ya kumsaidia ndugu wa kitabu na imani ziko nyingi.Njia nzuri sio kuruhusu anyang'anywe alichonacho na wewe umbebe nyumbani kwako.
Ni bora umsaidie kupambana na jambazi na abaki hapo alipo.
 
Duuh. Jamaa hawataki Mpalestina hata mmoja akatize kuingia Misri
Tatizo miaka ya nyuma, Jordan, Lebanon, Syria, misri zilikubali kupokea wakimbizi wa kipalestina. Baada ya vita Israel ikawazuia hao wapalestina wasiludi ktk nchi zao na mpaka leo wapaledtina wanaishi katika nchi hizo kama wakimbizi.

Na hata ktk hii vita ya Gaza Israel ilitaka wapalestina waondoke Gaza na wasiweze kuludi tena. Sasa wameshitukiwa na plani yao ovu ila nyinyi manyumbu hamuelewi kitu ndio maana mmebaki kupayukapayuka tu
 
Namna ya kumsaidia ndugu wa kitabu na imani ziko nyingi.Njia nzuri sio kuruhusu anyang'anywe alichonacho na wewe umbebe nyumbani kwako.
Ni bora umsaidie kupambana na jambazi na abaki hapo alipo.
Kwa hiyo unakiri kwamba bila kujali jinsia, umri, wala afya, wapalestina wote ni wapambanaji na hivyo wanatakiwa kuendelea kubaki uwanja wa mapambano kupambana na Israel? Sasa mbona Israel ikawafyeka huwa mnasema inafyeka wanawake watoto, wazee na wagonjwa?
Kwa kauli yako hapa umeshakiri kwamba Israel yupo sawa sababu kila mpalestina ni ni mpiganaji.
Kingine Misri kamwe hawezi kupoteza resources zake kwenda kukabiliana na Israel, pale ameenda kudhibiti Wapalestina wasiingie upande wake na mpaka anasogeza majeshi Sinai ujue tayari wameshakubaliana na Usrael sababu hana mamlaka ya kusogeza majeshi Sinai bila kuwasiliana kwanza.
 
Na wewe unataka japo njama zimeshajulikana lakini bado hizo njama zisizuiwe badala yake apewe Israel anachokitaka.Hiyo sio akili nzuri.
Wapalestina ndio wote ni wapambanaji lakini wasio na silaha.Sasa unahalalisha kwa sababu ni wapambanaji wauliwe tu hata kama sheria za kivita za kimataifa zitakiukwa.
 
Screenshot_20240213-082527_Quora.jpg
 
Duuh. Jamaa hawataki Mpalestina hata mmoja akatize kuingia Misri
Wapalestina hafai kuishi nao mkuu;
1. Walikwenda Lebanon huko walikuja kuopindua serikali na kuanzisha jeshi lao (Hizbollah)
2. Walikwenda Jordan baada ya muda waliazisha jeshi vita ilikuwa kubwa hadi Jordan iliomba msaada wa Israel kuwamaliza!
3. Walikimbilia Misri kaskazini na baadae walianzisha vita dhidi ya Misri kwa muda sana! hawafai hawa watu!
Ni hataree weka mbali na watoto!
 
Acha uongo na kuwa na aibu. Toa ushaidi wa madai yako
 
Namna ya kumsaidia ndugu wa kitabu na imani ziko nyingi.Njia nzuri sio kuruhusu anyang'anywe alichonacho na wewe umbebe nyumbani kwako.
Ni bora umsaidie kupambana na jambazi na abaki hapo alipo.
Nenda Kawasaidie sasa kuliko kuning'iniza kaynday hapo kibarazani baada ya kuvimbiwa na tende.
 
Duuh. Jamaa hawataki Mpalestina hata mmoja akatize kuingia Misri
Sahihi wapalestina waliohojiwa wakasema hakuna Kwa kukimbilia Tena Misri imefunga mpaka wanaomba tu Allah awasaidie Kwa Hilo eneo la Raffah pamoja na Misri kujenga ukuta wenye nyaya za umeme kuzuia wapalestina kwenda Misri pia wameweka wanajeshi kuzunguka huo ukuta kuhakikisha hakuna mpalestina anavuka mpaka kuingia Misri Hilo Jeshi sio Kwa ajili ya kupigana na Israel ni kuzuia wapalestina wasivuke mpaka kwenda kwao

Wanaogopa Hamas wasiingie Misri wakiwa wamevaa hijabu wanaume nk
 
Back
Top Bottom