ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,019
- 7,223
"Salaam kwa mkt wa CHADEMA MKOA WA MOROGORO.
Dada yangu habari za jumapili, kwanza nikukumbushe kwamba leo ni siku ya ibada kwa kuwa natumai wewe ni mkristo, tufanye siasa, lakini daima mungu mbele.
Nasikitika kutuma salamu hizi kwako, ambazo ni aibu kwako wewe kama mwenyekiti na pia chama chako kwa ujumla,
Ndg mwenyekiti, makada wa chama chako ndg Juma Tembo na mwanasheria asiyejitambua ndg Tarimo wakiwaongoza vijana wengine katika siku ya juz, majira ya mchana, mtaa wa mkwajuni, kata ya kichangani, wilaya ya moro mjini, makada hawa walileta vurugu za hatari na zisizo na msingi wowote MSIBANI kwa kugombea mwili wa marehemu Amina Juma ambaye mama yake mzazi bi Annastazia ni kada wa chama cha mapinduzi CCM.
Mmoja kati ya makada niliowataja hapo juu ambaye inasemekana ana mahusiano ya karibu na ya undani na bi Mchilo ambaye ni mama mdogo wa marehemu ndiye aliyekuwa kichochez kikubwa katika vurugu hizo za kijinga, ndg huyo kwakuwa alitoa hela ya mchele na nyama kwa ajili ya shughuli za mazishi, akichanganya na mahusiano yake ya karibu na familia ya marehemu alitumia nafasi hiyo kutaka kuugeuza msiba huo kama jukwaa la kisiasa na eneo la kisiasa la kufanya kampeni za CHADEMA.
Juma tembo na tarimo waliagiza magari meupe Pick up nne zilizoandikwa M4C, ambazo kwa wakati wote zilikuwa zikirandaranda msibani, kilichotokea...
1 wakati wa chakula makada hao waliwapanga vijana wa chadema kugawa chakula huku wakimuuliza kila anayekuja kuchukua chakula ajitambulishe kwamba yeye ni wa chama gani? Na akisema yeye ni wa CCM ananyimwa chakula, akisema chadema anapewa chakula kingi. Na akisema hana chama basi anaambiwa kuanzia leo ajiunge na CHADEMA.
2 matusi na kashfa nzito zilitolewa na makada wa chadema hadharani huku watu wakiwasikiliza, matusi na kashfa hizo ziliekezwa kwa diwan wa kata hiyo komandoo John Waziri(ccm) Mhe Aziz Abood mbunge wa kudumu milele jimbo la morogoro mjini(ccm) viongoz mbali mbali wa ccm, na serikali ngaz ya wilaya mkoa mpaka taifa.
3 makada wako walishinikiza, waligombea, walitukana na kulazimisha mwili wa mtoto huyo upandishwe kwenye moja ya magari yaliyoandikwa M4C.
Chama cha mapinduz ccm kilipata mafanikio makubwa katika msiba huo kwa kuweza kuzidhibiti vurugu hizo za chadema kikiongozwa na katibu wa ccm wa kata hiyo bi subira mashaka, vijana wa uvccm wakiongozwa na kamanda wa kata hiyo ndg Hamis Zikatimu, ambao kwa kiasi kikubwa walihakikisha mwili wa mtoto wa kada wa ccm bi Annastazia unapandishwa kwenye gari la ccm. Kama mwenyewe alivyotaka na kusema huku akilia kwamba "nataka maiti ya mwanangu ipandishwe kwenye gari la ccm)
Viongoz wa ccm wa kata hiyo walichukua hatua hiyo ya kuleta gari la ccm MAHINDRA kutoka ccm wilaya, baada ya kuona mlolongo wa magari ya chadema yakiwa yanazunguka hovyo hovyo msibani kinyume cha taratibu.
Hekima na busara za vijana wa ccm ndizo zilizo sababisha kutokumwagika damu msibani hapo kwani wananchi wengi walikuwa wameshachukizwa na vurugu hizo za Chadema. Tuliwasihi greengard wetu wawe wapole na watumie hekima zaid ili watofautiane kimaadili mbele ya jamii na vijana wa chadema. Vijana wa ccm walifanikiwa kwa hilo.
Ndg mwenyekiti, hivyobasi, naomba umkanye ndugu Juma Tembo ambaye mara zote amekuwa akikichafua chama chenu hapa morogoro kwa siasa zake za vurugu, akiwa mgombea wa ubunge jimbo la morogoro mashariki ambapo alishindwa vibaya na mgombea wa ccm ndg Innocent Kalogerez, Juma Tembo mwaka huo wa 010 alipata mkong'oto wa nguvu kutoka kwa greengard wa ccm ambapo ghafla akilitumia gari la chadema aliuingilia msafara wa ccm katikati ambao ulikuwa umetoka kwenye kampeni kata ya sultan, nikiwa ndani ya gari la greengard pamoja na katibu wa uvccm w beatrice tuliwaruhusu vijana wamtandike vizuri sana juma tembo, na vijana wakiongozwa na massawe walimpa discpline ya nguvu mpaka kakimbilia polisi ambapo alionekana mjinga kwa kuingilia msafara ambao haumuhusu.
Mwenyekiti waambie vijana wako kwamba, watambue
1 msibani sio eneo la kufanya siasa, ni eneo la majonz na linalowakutanisha watu wa iman tofaut, si vyema kugawa watu kwa misingi ya vyama na siasa.
2 kutukana viongoz wa nchi ni kuvunja sheria za nchi, ni upuuz, ni ushamba wa siasa, ni ujinga uliopitiliza na kutaka kuifanya nchi yetu isitawalike. Hatujengi, tunabomoa
3 Demokrasia isiyofuata sheria ni janga na maafa kwa taifa, marazote chama chenu kimekuwa ni chanzo cha vurugu, maandamano na mikutano isiyofuata taratibu, matusi na makelele yasiyo na maana, si vyema
Dada yangu mkt, waelimishe makada wako na umwambie Juma na wakili tarimo, iwe mwanzo na mwisho, wamevumiliwa sana, siku nyingine wakileta vurugu msibani kama vile, hakika vijana wetu watazirejesha nidhamu zao kwa vitendo. Juma anajua vizuri sana
Jumapili njema..."
By Mdau - Morogoro.
Familia zimegawanyika katika mazishi ya mtoto kutokana na itikadi za kisiasa. - YouTube
My take: Iwapo jitihada hizi zingeelekezwa kwenye upatikanaji wa maji safi au uboreshaji wa shule zetu na huduma za afya pamoja na miundombinu, tungekuwa mbali sana kimaendeleo. Badala yake watu wanashindana kununua chakula misibani na kupeperusha bendera zao kwenye magari ya kubeba jeneza!!!
Ni wapi tunakwenda?