Ibrah
JF-Expert Member
- Mar 22, 2007
- 2,729
- 528
Nimepata taarifa kuwa Rais JK amewapandishia mishahara Askari wa vyombo vya Ulinzi na Usalama hadi asilimia 40 kwa cheo cha SSP (Polisi na Magereza)! Kwa wenye akili timamu tunajiuliza kwa nini Wanajeshi wamepandishiwa mishahara kwa kiasi hicho wakati huu? Je, serikali ya JK imepata wapi hizo fedha za nyongeza hiyo kubwa ya mishahara wakati alituhutubia Watanzania kuwa Serikali haina uwezo wa kuwaongezea mishahara Wafanyakazi wake na kwa hiyo hata kura zao kwenye Uchaguzi wa mwaka huu hazitaki?
Je, ni kwanini upandihsaji huu umefanyika kwa siri kiasi kwamba hata Askari wenyewe wameshangaa kujikuta mishahara imeongezwa?
Taaarifa hizi nimezipata kutoka kwa Askari wa Magereza na Polisi, sina uhakika JWTZ na Wafanyakazi wengine wa Seriakali wameongezewa au la, wameongezewa Mlioajiriwa Sirikalini mtujuze.
Yawezekana, hofu imemkumba Muungwana kwa Mpinzania wake Mkuu DK Slaa kuitumia kauli ya kutotaka kura za Wafanyakazi kwenye harakati za kuingia Ikulu.
Hatua hii yaweza kuzua mtafaruku zaidi kwani Wafanyakazi watatambua kuw Sirikali inao uwezo wa kuwalipa vizuri ila tu Wakulu wanataka waendelee kutanua peke yao. Lakini pia nyongeza hiyo ni hatari kwa Uchumi wa nchi kwa hali za Wtanzania zimekuwa mbaya maradufu kutukana na kuzidi kudorora kwa uchumi na kuzidi kwa mfumuko wa bei kwa kiasi cha kutisha katika kuliko nchi yoyote ya Afrika Mashariki.