Mimi ni muathirika wa UKIMWI

Aisee pole sana. ....mojawapo ya matokea ya ku jiweka wazi ndio kama hizo rejections.

Usikate tamaa muda bad unao na utabarikiwa mtu muelewa na mtakuwa na familia yenu.

Jitahidi kumsamehe na ujisamehe wewe pia, kwa maana ni jukumu lako kujilinda afya yako kwanza.

Ni muda sasa tujifunze kuacha kuwa nyanyapa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi na kuwaona kama wamemkosea Mungu au walikuwa na maienendo michafu kufika maambukizi.

Kila la kheri Protein
...................Samahani mkuu nikuulize jambo!

Ktk situation kama hii mimi kama mwanaume wewe kama mwanamke ikitukuta tufanyeje?well mimi siwezi kumpigia muhusika simu immediately kwamba bwana sitakuowa zaidi nitajitahidi kutafuta mazingira salama kwake kwa ajili ya kumwambia ila wewe unategemea na upo tayari kufanya nini?

Kuanzisha familia labda!?
 
Huu udhi umenikumbusha mbali sana. Kuna kipindi Lemutuz alikuwa anatumia ID inaitwa Field marshal nadhani. Basi akaamua kuja na ID mpya Akijiita Willium Malecela akajitambulisha mwenyewe. Uandishi wake ulimtambulisha na kila mtu alochangia alisema field Marshal mzee wa masauti kaamua kujivua fekelo.
Field Marshal kumbe ni le mtuzi naona kakimbia ID ya william malecelA
 
Nafikiri Mkuu Protein umefanya vyema kujua afya yako pia.... Kilicho muhimu jali afya yako kwasasa na pia jali afya ya uwapendao....

Mimi naamini kabisa maisha ni lazima yaendelee, ndoto na matarajio uliyokuwa nayo yanaweza kukamilika be strong kila kitu kitakuwa poua....
 
Jf the land of saints.. utafikiri kila mtu anatumia rubbers..

Pole mdada , kuna vitu katika maisha ukishakumbana navyo ni kama vimeingia jumla..hata ulie na ukeshe kwa kulia bado haitokussidia

Cha msingi usimlaumu jamaa ila jilaumu kwa kuwa dhaifu hadi kumuachia chance ya kukuambukiza hivyo, ondoa suala la kuwa makosa ni yake peke yake ..

Kingine isamehe nafsi yako kwa kukosea na itafute amani ndani yako.. Make peace with your past to have better hopes for the future.. Hiyo ni aina ya maisha yako mapya na huwezi kujua unayapitia hayo yote kwa sababu gani ??... kila kitu kina sababu aidha uijue au usiijue, uikubali au uikatae... ila mwisho wa siku kinachojalisha ni lazma maisha yaendelee

Jifunze kujipenda na kuwa na furaha kwa yale uliyoyabakiza na kupitia hapo utapata mtu mwema.. Amini na itakuwa
 
Pole ndugu yangu, kwenye ujana tunapitia mitihani sana ukinusurika unamshukuru Mungu, mana idadi kubwa kabla ya ndoa kwenye ku date huwa tunajisahau na kujikutana tumewaamini watu tunao date nao tunajiachia huku hata kupima hatujapima. Nakumbuka nilipopata mchumba anataka kunioa akaniambia cha kwanza kupima uuuwi nilienda kwanza mwenyewe but still niliyakimbia majibu, uzuri nilienda na rafiki yangu nikamuomba akanichukulie mana mimi nilishakimbia nikamuacha pale hospitali, aliponiambia nimeyachukua uko Negative nilihisi kama kiumbe kilichozaliwa upya, baada ya kama mwezi nikaend tena hospitali nyingine this time peke yangu, nikakutwa negative ndo nikapata sasa nguvu ya kwenda kupima na mchumba wangu
inaonyesha ni jinsi gani ngoma iko used
 
Mwaka jana 2018 nilikutana na mwanaume wa ndoto zangu. Mtanzania, mzuri mcheshi msomi. Maongezi yalinoga sana. Tulikwenda dinner, mara ya pili tulikwenda picnic park. Siku nilipomkaribisha dinner nyumbani baada ya glass ya wine nilifinguka .

Yule kaka alikuwa hakustuka. Baada ya kuondoka aliniambia kwenye simu kuwa hataweza kunioa hivyo asinipotezee muda.

Niliumia sana.
bora maana inaonekana jamaa anajujua mwenyewe
 
...................Samahani mkuu nikuulize jambo!

Ktk situation kama hii mimi kama mwanaume wewe kama mwanamke ikitukuta tufanyeje?well mimi siwezi kumpigia muhusika simu immediately kwamba bwana sitakuowa zaidi nitajitahidi kutafuta mazingira salama kwake kwa ajili ya kumwambia ila wewe unategemea na upo tayari kufanya nini?

Kuanzisha familia labda!?

Bila samahani....mimi sio mkuu lakini.
Iwapo ikatokea mimi ndio muhusika...nitajaribu kukuelewesha kwa kina iwapo kama utakuwa tayari kuendelea na mimi.
Hayo mengine ya kuanzisha familia ni huko mbeleni sana...muhimu ni wewe kunikubali mimi katika hali yangu na kujifunza jinsi gani nitakulinda/utajilinda usipate maambukizi.
 
Mimi ni member mkongwe humu. Ninaishi Sweden na nina passport kwa sasa. Nilikutana na kijana Mtanzania aliyekuwa na viza ya uanafunzi 2007 kumbe slikuwa muathirika. Nilimlaribisha nyumbani kwa chakula bila kufahamu lengo lake.

Kawakua nilikuwa mpweke sana alijenga mazoea ya kuja kwangu hasa weekends. Alionyesha dalili zote za mapenzi, nilimuambia tukapime kwanza. Siku moja alijiforce kwangu na ukawa mwanzo wa mapenzi bila kupima.

Yule kijana alirudi Tanzania, niliendelea na maisha. Nilimsahau kabisa. Mwaka 2017 nilipata kazi wizara ya afya Sweden, occupation health walinipa form ya kujaza. Nilikwenda kwa daktari na kumwambia sitajali kama atatick box zote. Aliniuliza una uhakika unataka kupima HIV? Nikasema ndiyo.

Alinipa karatasi niende nayo lab. Baada ya wiki moja nilipigiwa simu nirudie vipimo. Sikuwa na wasiwasi. Baada ya wiki nilirudi kwa daktari. Aliniambia Protein una HIV. Nilidhami anaongelea mtu mwingine.

Alianza kunieleza kuwa matibabu sikuhizi yameboreshwa sana. Nenda kwenye kitengo.

Nimefika kwenye kitengo walikuwa wanafunga kwa chakula cha mchana. Ilibidi niende nyumbani. Nilisali sana kuomba huruma ya Mungu.

Saa nane nilirudi kwenye kitengo. Walichukua vipimo upya. Majibu kutoka HIV+. Nilipewa nurse alinipa counselling kuanzia saa tisa mchana mpaka 11:00 wakati wanafunga ofisi. Safari yangu kama muathirika ilianzia hapo.

Nyumbani kwetu hawafahamu zaidi ya kaka yangu ambae aliumia sana. Alisema tulikupeleka Ulaya upate maisha bora leo hii unapata HIV Ulaya?

Haya ndiyo maisha yangu mapya kama muathirika.


Baada ya maambukizi nilikaa miaka 10 bila kujijua. Nilikuja kumjua aliyeniambukiza baada ya kupata list ya wa Tanzania aliowaambukiza. Kuna uwezekano niliwaambukiza watu wawili au watatu kwani nilikuwa single nikijaribu bahati ya relationship.

Ondoa kwanza hiyo dhana kichwani. Ukimwi kila mtu anao. Na kama unamaanisha HIV hakuna kitu kama hicho. Ruhusu akili yako ifikiri nje ya box
 
Mkuu kwa kuwa wewe utakuwa na elimu na hii kitu usichoke kwa maswali yangu ndo kutoana tongo tongo kwenyewe huko.

Hizo receptors zinafanyaje kazi mkuu na prep inasaidiaje kutopata maambukizi kirahisi ,kama utakuwa na nafasi hebu fafanua kidogo.

Pili,mwanaume na mwanamke ni yupi aliye na nafasi kubwa ya kupata maambukizi wakati wa tendo lenyewe endapo mmoja wao atakuwa na maambukizi tayar?
ke ndo mwenye hatari ya kupata maambukizi .bt me akiwa hajafanyiwa tohara anakywa jwenye hatari pia...
 
Yaa kwa kujiamini kuwa niko Ulaya nilihakikisha wanapima kwanza. Ninakumbuka nilipima 2005 nikawa mzima. Basi kila aliyeniuliza nilisema ninepins.

Kuna siku nikiwa kwenye shrehe watu walimuongelea Zabron slivyoumwaga Ukimwi Stockholm ndipo masikio yalinifunguka.
Kweli unadiriki ku sex na mwanaume bila kupima ? Ilhali ww ulijua huna maambukizi ?
 
Mambo mazito haya mara ya mwisho nimepima sikumbuki na deilee siachi kula kavu anyway itakavyo kuwa iwe tu ndio fungu nililo lichagua
 
Hamnaga kitu huwa kinanikera kama hiki, yaani ufungue ID mpya sababu ya uzi tuu?! Ina maana angesema na ile ya zamani tusingeelewa au?!
Hahaaaahaaa!!!anaogopa mashambulizi watu watatumia ugonjwa wake ka silaha
 
Back
Top Bottom