Mimi ni Aquaculturist, nitumie kwa mradi wowote wa ufugaji samaki

Madear

Member
Feb 13, 2020
45
107
Habari za wakati huu Wakuu.

Kwanza kabisa nianze kwa kutoa pole kwa changamoto mbalimbali za kimaisha mnazozikabili. Mimi ni kijana wa kitanzania mwenye umri wa miaka 23, kitaaluma ni mtaalamu wa ufugaji samaki (Aquaculturelist). Ngazi ya elimu Diploma in aquaculture technology.

Pamoja na kuwa ufugaji samaki ni taaluma yangu lakini pia ufugaji wa samaki ni Kama dini yangu, mimi ni muhumini mzuri sana wa ufugaji samaki na samaki kwa ujumla, toka nikiwamdogo nimekua nikimuona Baba yangu akifanya kazi zinazohusiana na samaki (katika viwanda vya Mara fish & Primecatch industry) hapo ndipo passion na interest yangu juu ya samaki ilipoanzia na ndio ilipelekea kuchagua kusoma course ya Aquaculture, ninauwezo mzuri sana wa kusimamia na kufanya shughuli zote za ufugaji samaki (aquaculture activities) kuanzia site selection, cage & pond construction, fish seed production, best fish seed selection, larviculture, artificial propagation and fish feed formulation in general. Ninawelewa mpana, ujuzi wa kutosha, moyo wa kujituma katika kazi na pia ninakiu cha hali ya juu cha kutumia knowledge na ujuzi nilionao kwa maendeleo ya ufugaji samaki kibiashara.

Naomba nitumie nafasi hii kukuomba ewe Mjasiriamali, mdau wa aquculture au mtu yeyote unaeweza kunipaconnection au kunishika mkono kwa namna moja au nyingine, unisaidie nipate mdau mwenye mawazo ya kufuga samaki wa maji baridi kibiashara au nipate nafasi kwenye mradi wowote wa ufugaji samaki.

Mawasiliano; 0758779170.

Screenshot_20210520-071312.png
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom