SoC01 Mimba za utotoni ni "kaburi" la ustawi wa Watoto wa Kike nchini

Stories of Change - 2021 Competition

Uchumi wa Mifugo

JF-Expert Member
May 20, 2021
345
576
Amina (siyo jina halisi)mwanafunzi wa kidato cha tatu katika mojawapo ya shule za sekondari wilayani Kibaha mkoa wa Pwani kila siku anaamka saa 11 ili awahi kwenda shule,shule iliyopo umbali wa kilometa sita kutoka nyumbani kwao.Kila siku anaenda na kurudi kwa miguu, nyumbani hapati kifungua kinywa wala hapati hata mia moja ya kununulia kipande cha muhogo.Nililazimika kufanya mahojiano na Amina baada ya kusikia mazungumzo kati yake na Sofia. Amina alimuomba Sofia kipande cha muhogo wa kukaanga ili atulize njaa kali iliyokuwa inamkabili muda wa mapumziko ya saa nne,badala ya kumpa muhogo Sofia alimjibu kwa kebehi"wewe si unamkataa Roja".Roja kijana dereva bodaboda amekuwa akimshawishi mara kwa mara Amina wawe wapenzi na kwenye mapenzi hayo angekuwa anapewa shilingi 1000 kila siku na kubebwa kwenye pikipiki wakati wa kurudi nyumbani kwao.

Lakini Amina amekuwa akikataa kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi akihofia ndoto zake za kuja kuwa nesi zitapotea kama zilivyopotea ndoto za rafiki yake na jirani yake Asha aliyekuwa anasoma naye darasa moja. Asha alipewa mimba mwaka 2019 na Hamis,kijana anayefanya biashara ya kuuza vitu vya urembo.Asha alipata mimba akiwa kidato cha kwanza na alifukuzwa shule hata kabla ya kufanya mitihani yake ya kumaliza kidato cha kwanza.Hakukuwa na kesi kwa sababu wazazi wa Hamisi na wa Asha walikaa kikao na kukubaliana Hamisi alipe fidia ya 180,000 ambazo alikabidhiwa baba yake Asha.Amina na Asha wote walimpenda nesi Rehema anayefanya kazi kwenye zahanati iliyopo karibu na kijiji chao, walimpenda Rehema kwa sababu ya unadhifu wake na tabasamu lake anapokuwa anahudumia wagonjwa,waliona hata wao wanaweza kuja kuwa manesi kama Rehema lakini kwa Asha ndoto hiyo imepotea imebaki kwa Amina ambaye naye anakutana na vikwazo lukuki.

Asha ni mmoja kati ya maelfu ya wanafunzi wa kike nchini Tanzania ambao ndoto zao za kufanikiwa kielimu na kuja kufanya kazi wanazozipenda zimekufa kwa sababu ya kupata ujauzito wakiwa shuleni.

Pamoja na kuwepo sheria kali ya makosa ya kujamiiana ya mwaka 1998 lakini bado vitendo vya ubakaji vinaendelea kushika kasi.Shirika la utangazaji la Uingereza lilitangaza kuwa kesi zaidi ya 600 za udhalilishaji watoto zilifunguliwa kwenye vituo vya Polisi Zanzibar kwa mwaka 2020 pekee huku ikiaminika kuwa kuna vitendo vingine vingi vya udhalilishaji vinafanyika na kumalizikia nyumbani bila kufika Polisi.Taarifa ya kituo cha sheria na haki za binadamu kuhusu mwenendo wa haki za binadamu ya mwaka 2020 inaonyesha kuwepo ongezeko la matukio ya udhalilishaji 5802 kwa mwaka 2015 mpaka matukio 7837 kwa mwaka 2020.

Taarifa nyingine ya kusikitisha ni ile iliyotolewa wilayani Kibondo mkoa wa Kigoma julai 18,2021 wakati Naibu waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto mheshimiwa Mwanaidi Ali Khamis alipokuwa akikagua na kujionea utoaji wa huduma za ustawi wa jamii na masuala ya maendeleo ya jamiii kuwa wasichana 981 walipewa ujauzito kuanzia januari hadi juni 2021.Yaani kwa miezi sita tu wasichana 981 walipata ujauzito ndani ya wilaya moja!

Pamoja na kuwepo mipango na sera nzuri za Serikali kuhusu ustawi wa watoto wa kike lakini kundi hili linaachwa nyuma,watoto wengi wa kike wanaoanza kidato cha kwanza hawafiki kidato cha nne na wengine wanapata ujauzito wakiwa shule za msingi.

Kuna sababu nyingi zinazopelekea mimba za utotoni baadhi ni hizi zifuatazo;
Umbali kutoka nyumbani hadi shuleni
,njiani wanakutana na vishawishi vingi kutoka kwa madereva pikipiki wanao washawishi kuwapakia bure pia wanapata ushawishi kutoka kwa vijana wengine na watu wazima wanaowashawishi kwa kuwapa hela na ghiliba nyingine.

Baadhi ya wazazi kutokutekeleza wajibu wao pia ni sababu nyingine ya wanafunzi kupata ujauzito.Sera ya elimu bila malipo imechangia ongezeko la mimba kwa sababu wazazi hawafuatilii maendeleo ya shule ya watoto wao kwa sababu hawagharamii elimu,wanaona hawana hasara.Pia hawafuatilii mienendo ya watoto wao,hawajui mabadiliko ya tabia ya watoto wao na hata wakijua hawawakatazi au kuwaongoza kwenye njia sahihi.

Kukosekana kwa chakula shuleni ni sababu nyingine ya kuongezeka mimba za utotoni.Ni rahisi kwa mwanafunzi mwenye njaa anayetoka nyumbani saa 11 asubuhi bila kupata kifungua kinywa na hapewi hela ya chakula kushawishika kuingia kwenye tamaa ya kupewa fedha na wanaume.Mtu mwenye njaa anaweza kufanya chochote.

Kuishi kwenye vyumba vya kupanga karibu na shule nayo ni sababu ya kuongezeka kwa mimba za utotoni kwa sababu wanafunzi wanakuwa huru sana,hawana wa kuwasimamia.Wanaweza kuingiza mtu yoyote na kwa wakati wowote kwenye vyumba vyao.

Pia baadhi ya wazazi wamekuwa wakiwashawishi watoto wao wapate ujauzito ili wafukuzwe shule na kisha waolewe ili wapate hela ya mahari.

Sababu nyingine ni kutokuwepo ufuatiliaji wa makosa ya kujamiiana,kesi nyingi za ubakaji zinamalizikia nyumbani.Hali hii inawafanya baadhi ya wanaume waone si jambo kubwa kumpa mimba mwanafunzi kwa sababu kesi yake itaisha kirahisi kwa kutoa fidia kidogo.

Pia fikra za wazazi kwamba kuliko kumfunga baba wa mtoto na kupelekea mtoto kukosa matunzo ni bora kusiwe na kesi ili baba wa mtoto abaki kwa ajili ya kumtunza mtoto wake inachangia sana kuongezeka mimba za utotoni.

Nini kifanyike?
Yajengwe mabweni ya wasichana katika shule za sekondari na wapewe umuhimu wale wanaotoka mbali na shule
.Mabweni yatasaidia wanafunzi kwa sababu hawatakuwa wanatembea umbali mrefu kwenda shule pia hawatakuwa wanaishi kwenye vyumba vya kupanga.Mabweni yatasaidia pia wanafunzi wa kike wapate muda mrefu wa kujisomea tofauti na nyumbani ambako muda mwingi wanautumia kwa ajili ya kufanya kazi za nyumbani.

Wazazi watimize wajibu wao katika kuwahudumia watoto wao kama kuwapa chakula na huduma nyingine za muhimu,wawanulie hata baiskeli kwa ajili ya kuendea shule,wafuatilie maendeleo ya watoto wao,wasimamie malezi bora ya watoto wao.Pia wasimamie nidhamu ya watoto wao kwa ukamilifu wasiwaachie Walimu tu.

Polisi na wengine wenye dhamana watimize wajibu wao.Kumpa mimba mwanafunzi ni kosa la jinai, wahusika hata wakikimbia au wakimalizia kesi nyumbani wasakwe na wafikishwe kwenye vyombo vya kisheria.

Na mwisho wanafunzi wapewe elimu ya afya ya uzazi, elimu hii ianzie nyumbani na iende hadi shuleni.Walimu na wazazi wawafundishe wanafunzi bila kificho madhara ya kushiriki mapenzi wakiwa na umri mdogo,pia wanafunzi wapewe elimu ya kutumia mipira ya kujikinga dhidi ya mimba na magonjwa ya zinaa. Wanafunzi wafundishwe tarehe hatari za kushika mimba, mwanafunzi auelewe mwili wake kwa undani.Pia wapewe elimu juu ya matumizi ya njia za kujikinga na ujauzito.

Tuache Mila na utamaduni uliopitwa na wakati, huu si wakati wa wazazi kuficha elimu ya afya ya uzazi kwa watoto wao.Ni bora kuwapa elimu na waende kushiriki mapenzi ambayo ni salama kuliko kutokuwapa na kwenda kushiriki mapenzi ambayo si salama.

Imeandikwa na John Ken.
Karibuni kwa majadiliano na kunipiga kura.
 
Wenye mawazo mengine mazuri karibuni kwa mjadala ili tuokoe mabinti zetu na hili janga la mimba za utotoni.
 
Mm naona hii kampeni ya kukataza watoto kuchakatana inaenda kinyume na maumbile (nature) ndiyo maana haifanikiwi. Ngono ni moja ya miito ya asili ya mwili wa mwanadamu. Ni kama njaa ama kiu vile.

Sasa mtu ameanza kubanwa na njaa ama kiu(amebalehe). Ninyi mnataka apambane kujizuia. How?

Itafutwe namna hii kitu iruhusiwe watoto walio balehe wachakatane kama kawaida. Mnapingana na mwenyezi Mungu??!!
 
Umetoa hoja nzuri,ni wakati wa wazazi kuwapa elimu ya afya ya uzazi watoto wao wa kike kama vile elimu ya kutumia kinga na njia nyingine za kuzuia mimba,kumkataza tu kwamba asifanye mapenzi haisaidii mbaya zaidi wanakatazwa kwa ukali matokeo yake watoto wanakuwa wanawaogopa sana wazazi wao na kushindwa kuwashirikisha kwenye masuala ya mahusiano yao.
 
Serikali ijenge mabweni mashuleni na kuwepo na vyakula.

Watoto wa kike waweze kuepuka vishawishi vya lifti za bodaboda wakati wa kwenda na kutoka Shule .
 
Serikali ijenge mabweni mashuleni na kuwepo na vyakula.

Watoto wa kike waweze kuepuka vishawishi vya lifti za bodaboda wakati wa kwenda na kutoka Shule .
Watoto wengi kutoka kaya masikini ndio waathirika wakubwa wa mimba za utotoni kwa sababu wazazi wanashindwa kuwapa fedha za chakula au kuchangia chakula shuleni.Umasikini unawafanya kujiingiza kwenye tamaa, mwenye njaa anaweza kufanya jambo lolote.
 
Hata wanafunzi wa kiume wengi hawamalizi Shule huamua kuacha Shule sababu ya umbali wa Shule kutembea kwa miguu na njaa.
Suluhisho ni kujenga mabweni, wazazi washiriliane na Serikali kujenga mabweni.Haiwezekani mwanafunzi atembee kilometa kumi kila siku kwenda na kurudi shule halafu aipende elimu,anaona kusoma ni kama adhabu.
 
Kujenga Shule za kata ni jambo moja lakini kujenga mabweni na kutoa chakula ni jambo muhimu sana ili kuweza kutimiza malengo ya kutoa elimu kwa wananchi.

Walimu pia wajengewe nyumba za kuishi maana nauli za bodaboda elfu 10 kila siku kwenda na kurudi watazipata wapi wakati mishahara midogo?

Ndio unakuta wanapeana zamu za kwenda kufundisha na kulipua sababu mazingira sio rafiki.

Halafu kuelewa hili ni kwa kwenda mikoani hapa , Wilayani na vijijini.

Kata moja kwenda nyingine ni mbali sana na maporini.

Usafiri pekee ni bodaboda na ni bei gali.
 
Ujenzi wa nyumba za walimu pia ni muhimu kwa sababu wao ndiyo walezi wa wanafunzi wanafunzi wanapokuwa shule.
 
"Moja kati ya mambo yanayokwamisha maendeleo ya watu wengi na taifa kwa ujumla ni mimba za utotoni,vijana wengi wamepata mimba za utotoni zisizotarajiwa huku wakiwa hawana uwezo wa kuwatunza watoto wao na hivyo wanaongeza wigo kwa familia zao na taifa" nukuu kutoka kwa Nick Simon aka Nick wa pili mkuu wa wilaya ya Kisarawe.
 
Elimu ya afya ya uzazi ni muhimu kwa ustawi wa mabinti kwani sio kila bint ataelewa athari ztokanazo na msukumo wa mabadiliko ya mwili kwa kuishiwa kuonywa tu.
 
Elimu ya afya ya uzazi ni muhimu kwa ustawi wa mabinti kwani sio kila bint ataelewa athari ztokanazo na msukumo wa mabadiliko ya mwili kwa kuishiwa kuonywa tu.
Ni kweli kabisa,jamii yetu ibadilike ianze kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa watoto wote wa kike na wa kiume.Mambo ya kuona aibu yamepitwa na wakati.
 
"Moja kati ya mambo yanayokwamisha maendeleo ya watu wengi na taifa kwa ujumla ni mimba za utotoni,vijana wengi wamepata mimba za utotoni zisizotarajiwa huku wakiwa hawana uwezo wa kuwatunza watoto wao na hivyo wanaongeza wigo kwa familia zao na taifa" nukuu kutoka kwa Nick Simon aka Nick wa pili mkuu wa wilaya ya Kisarawe.

Ukiwa maskini unapaswa kutafuta solution ya karibu Na inayotekelezeka. Wazazi wawafundishe watoto wao wa Kike Elimu ya uzazi. Utaboo uishe. Nimekaa Ujerumani Sasa zaidi ya miaka 12. sio rahisi mtoto wa Kike kupata mimba. Watoto wanaruhusiwa kuwa na mahusiano kuanzia 14 na nahisi Sasa wengine mapema. Sina uhakika kama wanasex kabisa. Mana hawa wazungu unaishi naye Sex mpaka uombe kama Ajira. Sex sio jambo rahisi na pengine Hii Tradition Yao ya uwazi wa miili inawafanya kwenye Kusex yawe maamuzi ya dhati sana.

Lingine wenzetu hawana Siri Siri. So boy wa 14 years anajulikana mpenzi Wake and so hata uaminifu unakuwa upo upo.
 
Jana sikumsikia waziri Ummi mwalimu akiongekea swala la kujenga mabweni ya Shule na nyumba za Walimu kwenye Shule za kata inaonekana halipo kabisa kwenye mipango ya hivi karibuni.
 
Ukiwa maskini unapaswa kutafuta solution ya karibu Na inayotekelezeka. Wazazi wawafundishe watoto wao wa Kike Elimu ya uzazi. Utaboo uishe. Nimekaa Ujerumani Sasa zaidi ya miaka 12. sio rahisi mtoto wa Kike kupata mimba. Watoto wanaruhusiwa kuwa na mahusiano kuanzia 14 na nahisi Sasa wengine mapema. Sina uhakika kama wanasex kabisa. Mana hawa wazungu unaishi naye Sex mpaka uombe kama Ajira. Sex sio jambo rahisi na pengine Hii Tradition Yao ya uwazi wa miili inawafanya kwenye Kusex yawe maamuzi ya dhati sana.

Lingine wenzetu hawana Siri Siri. So boy wa 14 years anajulikana mpenzi Wake and so hata uaminifu unakuwa upo upo.
Uwazi

Wazazi wakazanie elimu ya afya ya uzazi kwa watoto wao,mambo ya kuficha ficha na ukali yamepitwa na wakati.Unakuwa mkali lakini mtoto anaishia kupata mimba na magonjwa.Hawa watoto wanakutana na changamoto nyingi sana.
 
Jana sikumsikia waziri Ummi mwalimu akiongekea swala la kujenga mabweni ya Shule na nyumba za Walimu kwenye Shule za kata inaonekana halipo kabisa kwenye mipango ya hivi karibuni
Mabweni yangesaidia sana kupunguza mimba za watoto wa kike.Serikali iweke mkazo ujenzi wa mabweni kama ilivyo kwa madarasa
 
Back
Top Bottom