Milo mitatu kwa siku ni kwa masikini

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Mar 11, 2020
2,704
6,501
Masikini sisi ndio tunapiga milo mitatu kwa siku tena sio miatatu tu inaweza kuwa minne. Make tunapiga Chai, mchana tunapiga Chakula jioni Supu na bado tena Chakula cha usiku. Hapo katikati kabla ya saa 7 kuna mara soda, mara karanga maea matunda.

Matajir wengi wanakula milo miwili kwa siku, asubuhi na jioni basi inatosha na wana ratiba na mpangilio wa kula, sisi masikini ssala la mpangilio wa kula halipo na ndio maana tuna figire hazieleweki eleweki.

Prof Janabi akisema anakula milo miwili mimi namuelewa fika hio ni hulka ya watu wengi wenye pesa zao. Sasa masikini lazima tushangae anaweza vipi kula milo miwili kwa siku.

Kisayansi kwanza ieleweke hakuna kitu na hahisi njaa, ile ni saikolojia isha jengeka kwemye ubongo ikifika saa 7 tu unataka kula, au saa 4 chai. Ila mwili sio kwamba ubakuta umeishiwa chakula hapana ila ni uramaduni mwili umeijengea.

Watu wanao funga ndio maaana siku za mwanzo wanapata sana shida ila wakisha zoea ile hali inapotea kabisa, sasa wakina Prof Jajabi walisha jitwin, mchana hawezi hisi njaa make kamwe.
 
Mkuu umeshakaa na matajiri ukaona wanakula milo miwili au ni nadharia tu ?...

Hata hivyo unaweza kula hata mara tano kwa siku maana cha msingi ni unachokula na kwa kiasi gani na sio mara ngapi unakula...

Wengi tunakula mara tatu kwa kufukia maana hamna uhakika wa evening coffee and desserts au fruit salad. Ukila umekula
 
Excellent
 
Jamaa ni muongo sana.
Wenzetu wenye nazo;
1.Asubuhi kifungua kinywa wengine wanaita starter

2. Saa 4 chai/,kahawa

3. Saa 6 hadi 7 lanchi

4. Saa 9 hadi 10 kahawa/juisi nk

5. Usiku ndio...nini vile?

Wenye nazo hawaishi kutafuna kutwa.

Acha Janabi awatie moyo sijui ni siasa?
 
Mbona wenzetu wazungu wanakula milo minne na asilimia kubwa wana afya nzuri zaidi kutuliko sisi?!
Wengi sasa kuishi miaka 90 hadi 100 ni kitu cha kawaida.
Acheni kuwafariji watu.
Serikali iache kukwepa majukumu ya kupunguza ukali wa maisha ili raia wapate kula milo mitatu au zaidi.
 
Back
Top Bottom