Millya: Nape ni vuvuzela na saratani ndani ya CCM

mimi naona huyu mmasai ndie Vuvuzela,pia na akome kutymia jina la Mwl Nyerere ,kwani Nyerere aliwapiga chini hao maboss zake Vuvuzelya Millya ,naona Millya sasa ndio anazidi kuonyesha Uvuvuzela wake ,kisa ni vijisenti na ukabila ,kama alishindwa Simanjiro huko kwingine ndio ataweza ,KAMA MNAPENDA KAMPIKIENI CHAI,JITU ZIMA NA NDEVU LINAENDESHWA KWA REMOTE NI KAMA ROBOT VILE
 
Ccm wameanza na udini na sasa wamekuja na UKANDA,jamani ccm inatupeleka pabaya.nyie uvccm historia itawahukumu.mnaigawa nchi na hamfai kuaminiwa kwa lolote,sio wa kaskazini wala wa pwani..mmekiuka miiko ya mwalimu nyerere na misingi ya chama chake..millya you are adding salt to a wound...
 
Kuwa mwana CCM ni kazi kubwa sana! kazi yako itakuwa kujibu tu shutuma za ufisadi, si kujenga Tanzania. Mawazo ya Millya si "ustaharabu" wa CCM.
 
Kuna marafiki zangu wana CCM wakati sekretarieti mpya ya Mukama na Nape ilipoteuliwa walikua na matumaini makubwa kwamba chama chao kimefufuka upya. Siku hizi nikiongea nao,wamerudi ktk unyonge. Wanasema Nape na kundi lake wanakiua chama chao.

Mwalimu Nyerere alisema" ccm itamalizwa na wanaccm wenyewe"
 
Mhh! Ama kweli CCM imepoteza dira. Hii ni athari ya chama kuondoka kwenye misingi yake na kutekwa na utashi wa kifamilia na vikundi. Milya bado unafanya nini ndani ya Magamba? Umekwisha! Usipoacha kelele zako wakwere lazima wakung'oe hapo ulipo.
 
Kwa nini watanzania tunapenda kudanganyika na vitu vidogo, hata hapa JF ninapoaamini kuna wasomi kidogo na watu wenye upeo wa juu kidogo bado tunadanganyika.

Hapa hamna tofauti hawa Millya na Nape wote wanatumiwa na wakubwa zao waliotuibia na wanaoendeleza ufisadi nchi hii. Hawa ni vibaraka na wakubwa zao wana mtandano wao wa kuiba na wanataka kuendelea kuhodhi madaraka au kupata madaraka makubwa 2015 na wote wanaona bado ni mapema kuanza vita ya wazi wazi ndiyo maana wanatumia hawa vijana waliojiingiza kwenye siasa kwa sababu ya kuona matunda yake yenye kunyonya wananchi na kuendeleza uzembe, ubadhirifu, na uongozi usiokua na uzalendo wa kweli wa taifa hili.

Hawa wote wanalelewa na mfumo wa kinyonyaji wa kifisadi uliojengwa na CCM kwa miaka zaidi ya 20 sasa na wanataka endelezo la mfumo huo hamna kipya wala cha maana kwenye spichi hizi zaidi ya kuonyesha kwa uwazi kwamba wamekuwa wengi na hawatoshi wote kuiba haka kamkate ketu..

Fikirini vijana kwa makini mtaendelea kutumika na kudanganywa hadi lini?
 
Millya nilimwona kajisajili humu jana, natumai ataipitia hii thread na kutoa maoni yake
 
Millya sasa nakubaliana na wewe kauli yako mwezi jana kwamba huyu na Nape eti kumbe ni FuvuZela.

Hebu angalia alivyokiaibisha chama chake CCM kwa kushindwa tu kuelewa tofauti kati ya Mwenyekiti wa CCM taifa na taasisi ya urais.

Chadema hatukuomba kukutana na mwenyekiti wa CCM ndio chama fulani cha siasa kitolee maelekezo za kitoto kama hizo tulizozisikia. Huyu dogo kumbe kweli hamnazo sasa nimeamini!!
 
Bure kabisa, hamna kitu pale;

wenye kuchukia
UFISADI ndani ya chama kile ni miongoni tu mwa wajumbe saba walioonelea vema kujilindia heshma zao kwa kuondokana na hilo genge la mafisi isiokua na kitu huruma kwa kukwapua kudi zetu na kututaweshea kabisa matumaini ya ajira na maendeleo nchi.

Nasema, keleleee!!!!!!!!!!!!!
 
Cdm inapaswa kumchunguza kwa kina huyo dogo,maana mbali ya kuwa mpiganaji hodari magambani,kuna tetesi yupo kambi ya mamvi na walikuwa wanaendesha mkakati wa 2015.
 
Gamba huwa halitoki kirahisi, mpaka limwagiwe mafuta ya taa. Lakini ukimuuliza nyoka maumivu ya basi Nape atajua anachokiongea.
 
Back
Top Bottom