Mikogo ya Hemed Kivuyo wa ITV!

Huyu anatangaza kwa mbwembwe pale Yanga inapofanya vizuri na Simba inapofanya vibaya...
Ngoja leo tumsikie kwenye game la Simba na Yanga,mbwembwe zote chali...
 
ha ha ha ha halafu yule jamaa sijui msosi ni jwiii manake ukimuona utadhani ataanguka sekunde kumi zijazo...
 
Ni afadhari na Kivuyo huyu George Maratu ndo mtangazaji anayeniudhi kuliko wote nadhani kwa namna anavyovuta sauti yake hadi anaharibu I wish asiongezewe mkataba.

utakuwa prof muhongo wewe, mbona wako poa sanaaa
 
Awe mbunifu, sio lazima aongee yale yale kila siku. Lazima utamsikia: "Timu hiyo kutoka mtaa wa yule mnyama mrefu na mpole..." au "Timu hiyo kutoka mtaa wenye pilikapilika jijini..."

na ww kuwa m bunifu kwa kujaribu kuangalia vituo vingine vya habari,ili uone umuhim na utofauti wa hemedi kivuyo.
 
Hemed Kivuyo ni mtaalam na anakubalika na wengi na naweza kumfananisha na Ben Mwakikoti jasiri wa afrika. Ben akitangaza Habari za Majira watu walikuwa wanasahau kula.:lock1::lock1:
 
Mikogo yake inamfanya awe tofauti na wa peke yake maana mimi kama mtazamaji inanivitua sana.

Lakinj kama mdau ambaye ninauelewa wa habari,uandishi wa kivuyo pamoja na aina yake ya kuripoti ndiyo inapendelewe sehemu nyingi sana ba pia inamvutia mtazamaji.

Lakini kama nilivyosema hapo juu kuna aina mbalimbali za jinsi ya ripota kuweza kuripoti kazi yake kama ilivyo kwenye uandishi wa habari au stori yoyote kwa kuanza na uwasilishi wa moja kwa moja au kuweka kwanza vionjo.
 
Nimemsikia mtangazaji wa habari za michezo wa itv,hemed kivuyo ktk habari za michezo akitangaza matokeo ya lile shindano la nani mtani jembe. Hakika nimejikuta nikicheka baada ya kumsikia kivuyo akidai kuwa kama mahakama ya icc ingekuwa ikijihusisha na kuwashughulikia watesaji wa nafsi za watu basi ingeanza na mnyama mkali simba ambaye amewatesa vilivyo wana yanga bila kuwahurumia kwa kuwachabanga magoli 3 kwa 1.
Mbwembwe zake mtangazaji huyu zinakonga,anafaa kuwa mshereheshaji(mc)
 
Huyu anatangaza kwa mbwembwe pale Yanga inapofanya vizuri na Simba inapofanya vibaya...
Ngoja leo tumsikie kwenye game la Simba na Yanga,mbwembwe zote chali...
Jamaa yuko poa leo kaipaisha Simba..
Kama mahakama ya ICC ingekuwa inasikiliza kesi za watu wanaoumizwa moyo basi mashabiki wa Yanga wangesikilizwa...teh teh teh 3-1 ugonjwa wa moyo watu wamezirai uwanja wa taifa..
 
Kwa kweli ameongea vizuri sana,maana tulikuwa hatulali majumbani kwa makelele yao,ameifanya week end yangu iwe nzuri mno,ukichukulia kule nako OT Man U kaua.
 
Back
Top Bottom