EJM_
JF-Expert Member
- Jul 8, 2011
- 3,836
- 2,093
Leo nimekumbuka kitu nikacheka sana.
Wakati Niko Std 7 nilikuwa na mahusiano ya kitoto na sista du mmoja hivi tulikuwa tunasoma darasa Moja. Sasa communication yetu ilikuwa kuandika barua halafu inawekwa kwenye daftari nyuma ya jaladio.
Sasa Kuna kipindi tukawa na mgogoro halafu mi nikawa na kiburi Cha kusamehe. Sasa siku Moja nikawa nimeandika barua ndefu sana ya kusamehe lakini nimeweka makorokoro yote ambayo tumefanya na yaliyonikwaza. Sasa baadae nikaghairi kumpa Ile barua halafu nikaimissplace home. Ikaja ikapita kama wiki 2 hivi mara pap bi mkubwa home akakutana nayo.
Nimerudi kutoka shule nikaitwa nikapewa Ile barua naambiwa enhee hebu niambie hii Nini. Bwana bwana niliikana Ile barua siijui pamoja na Kila kitu kuanzia mwandiko na mambo mengine kasoro jina maana tulikuwa tunaitana majina ya mahaba sio majina rasmi (For security reasons for cases like these) ila mwisho wa siku bi mkubwa alikausha tu ingawa alikuwa kabisa no ya kwangu.
Ziko nyingi but hii ni mojawapo nimekumbuka Leo. Ipi ya kwako?