Mikasa iliyotokea kipindi wanaigiza filamu za Yesu

Haikuwa kazi nyepesi kuigiza movie za Yesu. Songombingo lilianza katika ile scene ya msalabani. Scenes zote ilikuwa rahisi sana isipokuwa ile ya msalabani.

Kwenye ile movie ya mwaka 1979 ya Yesu iliyoigizwa na Decon, Brian Deacon anasimulia kwenye interview kuwa wakati wa scene ya msalabani haikuwa nyepesi kuigizwa kwani walikumbana na dhoruba kubwa la radi kiasi cha kushindwa kuigiza hivyo wakasubiri siku inayofuata. Haikubadilika, Hali ilitulia lakini baada ya Decon kuwekwa msalabani upepo mkali ulivuma, lakini hawakukata tama. Movie ya yesu ya Brian Deacon ndio movie mpaka sasa inayoshikilia rekodi ya Dunia ya kutazamwa mara nyingi na pia inashikilia rekodi ya movie iliyotafsiriwa kwenda lugha mbalimbali Duniani. Movie hii ilichezewa huko katika milima ya nchini Israel. Na mpaka leo hii Director (Muongozaji) wa filamu huyo hajulikani ni nani. Na baadhi ya waigizaji walishafariki na muigizaji mkuu aliyeigiza kama Yesu sasa ana takribani miaka 75 mwaka huu 2024.

Mikasa Haikutokea kwao tu kina Deacon bali hata kwenye movie ya Passion of Christ ya 2004, Muandaaji wa hiyo filamu, Mel Gibson alielezea songombingo la namna hiyo, walisitisha kuigiza filamu hiyo kwa siku tatu mfululizo kutokana na radi za mara kwa mara zilizoibuka tu na tetemeko la ardhi, anasema hata Jim Caviezel aliyeigiza kama Yesu alinusurika kuuwawa na radi. Pia alikumbwa na magonjwa mbalimbali ya mapafu ikiwemo Pneumonia, pamoja na kuishiwa joto la mwili. Filamu hiyo iliigizwa huko Italia katika kipindi cha majira ya baridi kali.
Si kwa sababu walifanya filamu zao msimu wa mvua na baridi?
 
Yaani story bila picha ya jamaa yenu? 😂!!
mqdefault.jpg
 
Luka 18
19 Yesu akamjibu, “Mbona unaniita mwema? Hakuna mtu aliye mwema ila Mungu peke yake.


Yohana 17
3 Na huu ndio uzima wa milele: wakufahamu wewe ambaye pekee ni Mungu wa kweli, nakumfahamu Yesu Kristo ambaye umemtuma.


Mathayo 27:46​

Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?
Ally Hassan Mwinyi na Hussein Mwinyi
 
Titanic (1997)
Achana na Titanic... Filamu ya Yesu ya mwaka 1979 ndio inaongoza kwa kutazamwa zaidi Duniani

Titanic ilikuwa inashikiliwa record ya filamu yenye mauzo makubwa, ila badae 2010 Movie ya AVATAR ikapindua na kuvunja record ya Titanic na kuifanya AVATAR kuwa ndio filamu yenye mauzo ya juu zaidi.

Jua kutofautisha Filamu kutazamwa zaidi na Filamu kuuza zaidi... Hivyo ni vitu viwili tofauti.

Filamu ya YESU ya mwaka 1979 imetazamwa karibia Duniani kote, na bado inazidi kutizamwa
 
Inategemea na chanzo chako, kuna mahali

inaonyesha AVATAR ndio inaongoza
Jua kutofautisha Filamu kutazamwa zaidi na Filamu kuuza zaidi... Hivyo ni vitu viwili tofauti.

Filamu ya YESU ya mwaka 1979 imetazamwa karibia Duniani kote, na bado inazidi kutizamwa. Titanic ilikuwa inashikilia rekodi ya mauzo makubwa ya filamu ila badae AVATAR ikavunja record ya Titanic.

Lakini filamu ya YESU ya mwaka 1979 bado inashikilia rekodi ya kutizamwa mara nyingi Duniani. Hizo Titanic sijui Avatar hazifikii rekodi ya movie ya Yesu
 
Achana na Titanic... Filamu ya Yesu ya mwaka 1979 ndio inaongoza kwa kutazamwa zaidi Duniani

Titanic ilikuwa inashikiliwa record ya filamu yenye mauzo makubwa, ila badae 2010 Movie ya AVATAR ikapindua na kuvunja record ya Titanic na kuifanya AVATAR kuwa ndio filamu yenye mauzo ya juu zaidi.

Jua kutofautisha Filamu kutazamwa zaidi na Filamu kuuza zaidi... Hivyo ni vitu viwili tofauti.

Filamu ya YESU ya mwaka 1979 imetazamwa karibia Duniani kote, na bado inazidi kutizamwa
Weka source inayoonyesha hiyo ni the most watched movie of all the time,
 
Kupitia filamu hii ya mwanzo iliokoa mamilioni ya watu ulimwenguni wamgeukie Yesu.
So ilikuwa ni mitihani ya shetani ili isifanikiwe kutoka.
Jesus filamu ndio za mwanzo zilizogusa hisia za mamilioni ya watu ulimwenguni
 
Weka source inayoonyesha hiyo ni the most watched movie of all the time,

anzia mtaani kwako,achana na source za google labda kusoma kiingereza kikakuchanganya.

uliza watu kadhaa,dini tofauti wangapi wameangalia avatar,na wangapi wameangalia mkanda wa Yesu.

utaelewa unachoambiwa.hiyo ni kama biblia.
ndicho kitabu ambacho kimetolewa copy nyingi zaidi kuliko vyote duniani kwa mbali,lakini sina uhakika katika kuuzwa maana sehemu nyingi kimetolewa kama zawadi.
angalia ktk rates iko no 10,lakini ndio pekee yenye melezo maalum.
IMG_0136.png
 
Back
Top Bottom