Migogoro ya Ardhi Jijini Dodoma

WaHapahapa

Member
Apr 11, 2014
44
52
Mhe. Rais na mgombea wa Chama cha mapinduzi, kunajambo yawezekana wasaidizi wako wanakuficha kuhusu migogoro ya ardhi katika eneo la ngome ya CCM Dodoma. Kumekua na migogoro ya kutengenezwa na ile iliyokuwa CDA ambayo uliivunja mara moja ili kuondoa Migogoro ya ardhi jijini Dodoma, Lakini kitu ambacho ulikisahau ni kuwa haukuondoa yale waliyoyafanya kitu ambacho kinasababisha suala la kuiondoa CDA litafsiriwe kama ni sawa na kubadilisha chupa ya Gongo ilhali Gongo ni ile ile.

Mfano dhahiri ni hili suala la UKANDA WA KIJANI. yaani hii CDA iliweka maeneo ya ukanda wa kijani ambayo kisheria ni yalikua chini ya umiliki wa vijiji husika. Huku wakibadilisha maeneo makubwa na kuwa makazi ya watu mfano wa maeneo hayo ni NZUGUNI,MTUMBA NA MKONZE (nia ni kuuza na kugawana viwanja watumishi wa CDA pasipo na Mwananchi wa Dodoma kudai maeneo hayo huku wakiwaaminisha ni mali ya CDA na sio Wananchi wa Dodoma).

Sasa kuna eneo dogo sana ambalo lilibaki pasi na kubadilishwa kuwa makazi kutoka kwenye hilo walilolidai ni Ukanda wa kijani lipo katika kata ya NTYUKA, katika eneo hilo mamlaka ya kijiji ilisharuhusu watu kufanya shughuli za maendeleo kwa kuwa maeneo hayo kisheria yapo chini ya Kijiji na shughuli ya kijiji ni kilimo, makazi na ufugaji.

kumejengwa Hospitali ya Ntyuka inaitwa DCMC, kuna shule ya sekondari ya Ntyuka, kuna shule ya msingi ya Shekinah, kuna makazi ya wananchi zaidi ya elfu ishirini ambao wameweka makazi ya kudumu katika maeneo hayo.

Hoja kama hizi ndizo zinazopelekea kunyang'anywa kata chache za Hapa Dodoma na kupewa vyama vya upinzani. utakumbuka ule mgogoro wa Kizota nk.
Kama kutakuwa na uwezekano basi fanya kuimaliza migogoro hiyo kabla ya uchaguzi kwani unawapa wakati mgumu sana wagombea wa Udiwani na ubunge kuchomoka kwenye kilengeo hiki.

MGOGORO WA KATA YA NTYUKA
Mkurugenzi wa Jiji alipeleka wataalamu wa kupima viwanja katika aneo hili na wataalamu wale walipima eneo lote la Ntyuka. Ambapo hata Chuo cha Taasisi ya Mwl Nyerere ilipata eneo kwa ajili ya kujenga tawi la chuo chao hapa Dodoma.
Sasa Baada ya Chuo hiko kuhitaj eneo katika Jata ya Ntyuka, wananchi ambao walikua wanamaeneo katika eneo chuo walihitaji walikubaliana gharama za kulipwa na walipigwa picha ili kulipwa fedha zao.

lakini fedha za kulipwa zilotoka, uongozi wa Jiji la Dodoma ukaanzisha sekeseke kuwa eneo hilo ni la ukanda wa kijani. suala ambalo linafikirisha sana. moja ya maswali yanayotia shaka ni pamoja na:-

1. endapo eneo hilo sio la wananchi ilikuaje Mkurugenzi wa Jiji alete kampuni ya upimaji na kupima (waliingia mkataba wa upimaji huo)
2. Mkurugenzi wa jiji aliandikia barua kata kwa ajili ya kuomba wananchi eneo kwaajili ya ujenzi wa Chuo cha mwl. Nyerere sasa kama eneo lilikua ni la jiji ilikuaje waombe kwa wananchi.
3. Waliruhusuje hospitali na shule mbili kujengwa ndani ya eneo hilo?

Wadau wa maendeleo Dodoma tunakushauri uimalize migogoro ya Ardhi ya Jijini Dodoma kabla ya kuingia kwenye uchaguzi wa mwaka huu kwani wapinzani wako wakisimamia hoja hizi basi kata pamoja na jimbo linaweza pokonywa kiurahisi hasa ukizingatia Mbunge aliyekua mwanzoni wa jimbo hili , mwaka huu amegombea kupitia Chama cha upinzani.

NAKUTAKIA KAMPENI NJEMA
 
Nasikia jeshi linakuja kujenga huko? Alafu chuo hiko kinajengwa sehemu gani? Baada ya kuvuka korongo kama unatazama hostel za Udom?
 
Nasikia jeshi linakuja kujenga huko? Alafu chuo hiko kinajengwa sehemu gani? Baada ya kuvuka korongo kama unatazama hostel za Udom?
Chuo kinajengwa maeneo ya Chidachi, yaan ni huu upande ambao kumejengwa hospitali ya DCMC kwa mbele kidogo baada ya kuvuka shule ya sekondari Ntyuka. Watu wamepigwa mpaka picha kuwa wanalipwa fedha zao halafu wameanza kuleta longolongo zao
 
Hilo jeshi linajenga mbali sana sio karibu na ntyuka, ila ni ile barabara inayokwenda Mvumi
 
Chuo kinajengwa maeneo ya Chidachi, yaan ni huu upande ambao kumejengwa hospitali ya DCMC kwa mbele kidogo baada ya kuvuka shule ya sekondari Ntyuka. Watu wamepigwa mpaka picha kuwa wanalipwa fedha zao halafu wameanza kuleta longolongo zao
Ha kuna kuhama wakija shikeni panga muwatoe nduki
 
Wamechukua pia eneo la michese na kuwapa wananchi viwanja mbadala ambavyo vipo mbali sana na mjini na viwanja hivyo wanapaswa walipie. Imagine mtu alikuwa na kiwanja chake lakini anahamishwa na kuhitajika kulipia upya tena. Inahuzunisha sana…
 
Back
Top Bottom