Miezi Kumi sasa bila Ben Saanane

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Miezi 10 sasa tangu Ben Saanane apotee. UTG tumeshirikiana na vyombo vya dola, taasisi na mashirika ya kiraia ktk juhudi za kumtafuta. Tumetoa full support kwa jeshi la polisi na mamlaka zingine za nchi. Ktk vikao vyetu na vyombo vya dola tulieleza doubts zetu na tukahitaji wazifanyie kazi ili kuziclear.

Walituhakikishia kuwa wangedeal na kila posibility ambayo ingeweza kuleta taarifa ya Ben alipo. But miezi 10 sasa doubts are still there. Vyombo vy...a dola vimeshindwa kuclear hata doubts ndogo tu, eg mtu aliyempigia simu ya vitisho Ben.

TCRA walitoa mawasiliano ya Ben ikiwa ni pamoja na watu waliokua wakimtisha. Polisi wakaahidi kufuatilia na kubaini watu hao. Sasa ni miezi 10 polisi WAMESHINDWA kuwakamata watu hao, wameshindwa hata kuwabaini tu kwamba ni akina nani wakati wamepewa mawasiliano yote na TCRA.

Hiki ni kielelezo kwamba vyombo vyetu vya ndani vimeshindwa kumtafuta Ben. Mara ya mwisho tumeenda makao makuu ya polisi, taarifa tuliyopewa ni kwamba bado wanaendelea na uchunguzi. Miezi 10 ya uchunguzi wameshindwa hata kujua waliokua wanamtisha Ben wakati namba wamepewa na TCRA? Uchunguzi gani huu?

Siingilii kazi za polisi lakini inawezekanaje uchunguzi wa mtu anayekashifu serikali unatumia siku moja ameshakamatwa, lakini mtu aliyemtishia Ben maisha unatumia miezi 10 na bado wameshindwa kumpata?

Na hili ni moja dogo, yapo mengi makubwa kuhusu Ben ambayo polisi waliahidi kuchunguza. Lakini kama hili dogo limewashinda hayo mengine itakuaje?

Tunalipenda jeshi letu la polisi, tunaliheshimu, lakini tunadhani wamefikia kiwango chao cha mwisho cha uchunguzi. Hawawezi tena. Tunawasiliana na wenzetu wa LHRC ili kuomba serikali iruhusu wachunguzi wa kimataifa.

Tuliomba "Observers" kutoka Umoja wa mataifa na wakaonesha interest lakini serikali ikatuambia tusubiri kwanza polisi wamalize uchunguzi wao, kama wakishindwa ndipo tufikirie wachunguzi kutoka nje. Serikali ilituhakikishia tuendelee kuwa na IMANI na jeshi la polisi.

Ni kweli tuna imani na polisi lakini tunadhani uwezo wao ni mdogo kuchunguza suala la Ben. Tutawaomba waweze kudeclare kwamba wameshindwa, ili tupate uhalali wa kuomba wachunguzi wa kimataifa. [HASHTAG]#BringBackBenAlive[/HASHTAG]!

Ben Saa nane.jpg
 
Kubenea mwanzoni si alionesha dalili nzuri za mahali alipo Ben saa8, mbona sasa hasaidii tena kupatikana kwa kijana huyo!!!!
 
Kama wao ndio wamemuweka msukule, unataka wamutoe?

Hiyo damu itawatafuna milele
 
Hili la LISSU,LA SAANANE ebu muulizeni vizuri M/kiti wa chama....huyu jamaa watu wengi wanamnyooshea sana kidole Na ninashangaa sana hamshtuki....
Na nina shauri sana Familia ya LISSU iwe macho sana huko NAIROBI maana kuna maadui wakubwa sana wa NCHI YETU including hao mapacha wawili waliouziana chama na HUYO HOSTER wao mkuu hapo KENYA tunajua kabsa anachuki kubwa sana na nchi hii hivyo anaweza kutake advantage kufanya yake kwa lissu mwisho wa siku WATIMIZE LENGO LAO kuu la KUMCHAFUA RAIS wetu......Tunajua kabsa hiyo combination ya hao wa wawili from TZ na hao wawili from KENYA ni hatari kabsa kwa mustakabali wa LISSU huko...hivyo familia ya LISSU kaeni macho msiwaamini hao so called viongozi wa chama....
 
Back
Top Bottom