Midahalo kwa Wagombea Urais

Mmeku Tukulu

Member
Feb 11, 2012
92
27
Katika uchaguzi 2010 Tanzania
tulishuhudia CCM wakiikimbia midahalo
iliyokuwa inaendeshwa TBC na hata
kuwakataza wagombea wao kushiriki.
Midahalo hii ni fursa muhimu kwa
wananchi na upatikanaji wa viongozi bora.
Wana jamii mnaonaje swala hili lisiwe tena
la kihiyari bali la lazima na liwekwe
kwenye katiba?
 
Nakubaliana kabisa na wazo hilo, liwekwe kwenye katiba! Tufanye kama wafanyavyo marekani tuwe na presidential Debate angalau 4 au 5, pia tuwe na vice presidential Debate angalau 3-4. Pia na wagombea ubunge na udiwani wafanye! Mgombea yeyote asiyeshiriki aondolewe kwenye kinyang'anyiro! Media mbalimbali zitumike kama vile tv'. Mfano Tido alijaribu kwenye mchakato majimboni, lakin baadae akapigwa stop!
 
Kama tutakuwa wagombea wenye elimu na busara kama Slaa as opposed to Kiwete type hili ni jambo bora. Kikwete hakukimbia mdahalo. Jamani mlitegemea Kikwete aseme nini kwenye jambo kama hili linalotaka weledi na seriousness? Laiti ingekuwa kuandaa kutembelea misiba badala ya midahalo hapa CCM wangekuja kwa nguvu zote na Kikwete angeibuka mshindi. Je watakufa akina Kanumba wangapi ili Kikwete apate sehemu ya kuonyesha "ujuzi" wake?
 
CCM ndiyo yenye serikali, jeshi, mahakama na magereza. Na ndiyo inayounda tume ya katiba!

Kipengele cha mdhahalo sahau kabisa kwenye katiba mpya!
 
Kama tutakuwa wagombea wenye elimu na busara kama Slaa as opposed to Kiwete type hili ni jambo bora. Kikwete hakukimbia mdahalo. Jamani mlitegemea Kikwete aseme nini kwenye jambo kama hili linalotaka weledi na seriousness? Laiti ingekuwa kuandaa kutembelea misiba badala ya midahalo hapa CCM wangekuja kwa nguvu zote na Kikwete angeibuka mshindi. Je watakufa akina Kanumba wangapi ili Kikwete apate sehemu ya kuonyesha "ujuzi" wake?

Je? Tutaendelea kuwa na viongozi wanaogopa kuongea na kuhojiwa na wananchi wao hadi lini? Tutaendelea kusikiliza kampeni zenye ahadi hewa zisizo hojiwa hadi lini? Tutaendelea kupiga kura kwa kufuata propaganda na kauli mbiu za kiualinacha hadi lini?
 
Je? Tutaendelea kuwa na viongozi wanaogopa kuongea na kuhojiwa na wananchi wao hadi lini? Tutaendelea kusikiliza kampeni zenye ahadi hewa zisizo hojiwa hadi lini? Tutaendelea kupiga kura kwa kufuata propaganda na kauli mbiu za kiualinacha hadi lini?

Tambua kwamba Viongozi walioko madarakani sasa hawaongozi, bali wanatawala!
Kuna tofauti ya kiongozi na mtawala mazee!

Kumbuka kauli ya mzee Makamba, aliwahi kusema hata kama wananchi wataamua kuichagua chadema, ccm watatangazwa washindi
 
Katika uchaguzi 2010 Tanzania
tulishuhudia CCM wakiikimbia midahalo
iliyokuwa inaendeshwa TBC na hata
kuwakataza wagombea wao kushiriki.
Midahalo hii ni fursa muhimu kwa
wananchi na upatikanaji wa viongozi bora.
Wana jamii mnaonaje swala hili lisiwe tena
la kihiyari bali la lazima na liwekwe
kwenye katiba?

Usifikiri waliokimbia mdahalo ilikuwa ni kwa bahati mbaya. Walikwepa kuonyesha aibu yao jinsi wasivyofaa katika nafasi hiyo. Mdahalo ni njia mojawapo muhimu sana ya kumpima kiongozi unayetaka kumchagua, ila sisi tunazugwa na uziri wa picha na wingi wake. Ni muhimu swala la mdahalo liwepo hata kama halitawekwa kwenye katiba ili tuweze kuwapima viongozi wetu vizuri zaidi kabla ya kuwachagua.
 
Hadhi yako na umri wako na matusi uliyaporomosha havioani.Kama ungetoa hoja bila kushusha matusi ungeeleweka.Kwasasa umechemsha
 
Sahihi kabisa, nakubali. Midahalo itawezesha wananchi kutoingizwa mjini na wagombea wa mitandao ya kifisadi kwa ahadi hewa zisizotekelezeka. Pia itakuwa ni fursa ya kujua wagombea, uwezo wao na sera zao; vinginevyo tuwe tayari kuendelea na siasa zinazojadili watu badala ya masuala (issues). Siasa za kujadili watu haziwezi kuepuka udini, ukabila, ukanda, umri ujana au uzee, urembo na mambo mengine ya kipuuzi.
 
Wazo nzuri,litasaidia tutambue uwezo na uelewa wa viongozi wetu wanavyo elewa matatizo yetu na solution zake,kama wafanyavyo romney na obama.:poa
 
Mdahalo ni kitu muhimu sana hasa ukizingatia dunia ya sasa. Ikumbukwe si kila mtu anaweza kupata fursa ya kuhudhuria katika mikutano ya kampeni kutokana na sababu mbali mbali za msingi kabisa. Lakini hata ukiweza kuhudhuria mikutano ya kampeni bado mikutano hii inakuwa kwa sehemu kubwa kama si sehemu yote huwa ni ya upande mmoja tu. Yaani mgombea au mwakilishi wake husimama na kunadi sera zake/za chama chake na kumwombea kura kwa wananchi. Mikutano haitoi fursa kwa upande wa wananchi waliohudhuria kumuuliza maswali au hata kumpa maoni mgombea. Fursa pekee na muhimu ni kwa njia ya mdahalo wa kuwakutanisha wagombea toka vyama mbali mbali na kuwapiga maswali ya papo kwa hapo.

Hili litatoa fursa kuweza kutambua uwezo wa mgombea kama mgombea na/au chama chake. Na kwa kufanya midhahalo na haswa ya kupitia vyombo vya habari kama redio na televisheni ni fursa kwa wananchi ambao wakati mwingine huwa hawafikiwi na wagombea wakati wa kampeni aidha kutokana na muda kutotosha au mahali pengine kutofikika kwa sababu ya barabara.

Midhahalo hii ihusishe wagombea wa ngazi zote katika maeneo yao. La mwisho ni umuhimu wa kuangalia kiwango cha elimu cha chini anachotakiwa kuwa nacho mgombea hasa wa Urais na Ubunge. Maana dunia ya sasa kiukweli kuwa na wabunge wa kidatao cha nne au cha sita tu bila zaidi hatuwezi kupiga hatua. Dunia tuliyonayo inahitaji mtu mwenye uwezo wa kuchambua mambo mbali mbali ya dunia ya sasa.
 
Back
Top Bottom