Miaka ya 60 tulikuwa tunalingana na Korea kimaendeleo, hawa jamaa walijikwaa wapi mpaka tukawaacha mbali kiasi hiki!

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
May 25, 2015
6,491
20,457
Leo asubuhi nilikuwa naangalia tv moja ya Korea kusini nilishangazwa na maendeleo hafifu ya hawa jamaa na nilipoangalia historia nikakuta kumbe miaka ya Uhuru tulikuwa karibu sawa.
Wakati Tanzania tumepiga hatua kubwa kiasi hiki wao bado wamelala usingizi mzito.
Sisi tunatengeneza Magari, electronics, kilimo uhakika wao bado wanajivuta.
Wataalamu wa uchumi,shida ni Nini kwa hawa ndugu zetu?
 
Ukishakuwa na mentality za Kijamaa unaogopa wawekezaji huwezi endelea kamwe,ni Hadi uondokane na hizo fikra za kimaskini na za hovyo.
 
Hakuna mtaji mkubwa kama kuwekeza kwenye rasilimali watu ,hasa wenye akili timamu, utajiri mkubwa ni akili ,tanzania tuna mali nyingi sna ila kuna shida kubwa sna kwenye akili zetu , wenye akili ni rahisi sana kuja kuchukua mali zetu , ili mradi tu matumbo yetu yashibe,tukishiba tunalala na akili zina lala .
 
1687235685829.jpg
 
Leo asubuhi nilikuwa naangalia tv moja ya Korea kusini nilishangazwa na maendeleo hafifu ya hawa jamaa na nilipoangalia historia nikakuta kumbe miaka ya Uhuru tulikuwa karibu sawa.
Wakati Tanzania tumepiga hatua kubwa kiasi hiki wao bado wamelala usingizi mzito.
Sisi tunatengeneza Magari, electronics, kilimo uhakika wao bado wanajivuta.
Wataalamu wa uchumi,shida ni Nini kwa hawa ndugu zetu?
Maake hapo kwanza nicheke
 
Hawa wakorea badala ya kujifunza namna ya kuendesha bandari zao wao wanazikodisha kwa wageni.
 
Leo asubuhi nilikuwa naangalia tv moja ya Korea kusini nilishangazwa na maendeleo hafifu ya hawa jamaa na nilipoangalia historia nikakuta kumbe miaka ya Uhuru tulikuwa karibu sawa.
Wakati Tanzania tumepiga hatua kubwa kiasi hiki wao bado wamelala usingizi mzito.
Sisi tunatengeneza Magari, electronics, kilimo uhakika wao bado wanajivuta.
Wataalamu wa uchumi,shida ni Nini kwa hawa ndugu zetu?
Kumbuka waliandaa Kombe la Dunia pamoja n Japan 2002.Anyway hii ni satire ,no problem.
 
Nitajie waliofanya maendelea chini ya ujamaa na hao viongozi wako wenye nia
China ni ya pili kwa uchumi mkubwa.
Tatizo sio ujamaa au upepari. Nchi nyingi sio wajamaa ila wanayumba.
Suluhu ni kuwa na viongozi wanaoyataka maendeleo, sio wanaotaka makofi jukwaani, sio wanaotaka sifa,sio wezi.
Mamiloni ya Watanzania yanapotelea mikononi mwa wachache.
 
Korea watu wameshikiwa akili na watawala wao, watawala ndio waamuzi wa mwisho, maoni ya raia ni kelele kwa watawala.

Pia chama tawala kule Korea kinawatawala watu kupitia ujinga wao na elimu ya ukasuku. Kinatumia katiba yenye viraka inayowapa kinga watawala hata wakiuza nchi.

Wananchi wa Korea unawagawa kulingana na njaa zao, hawawezi kamwe kupaza sauti kwa umoja wao.

Bora mimi nipo Tanzania. Korea hapafai.
 
Ukiacha elimu yetu duni ambayo haizalishi watu wengi wenye weledi wa kutosha pia tuna sera mbovu za kiuchumi.

Uongozi mbovu usiozingatia utawala thabiti wa sheria ambao haulindi haki za wananchi na kuwawezesha wawekezaji. Tanzania tuna utawala dhaifu ambao umewezesha ufisadi na ukosefu wa uwajibikaji.
 
Leo asubuhi nilikuwa naangalia tv moja ya Korea kusini nilishangazwa na maendeleo hafifu ya hawa jamaa na nilipoangalia historia nikakuta kumbe miaka ya Uhuru tulikuwa karibu sawa.
Wakati Tanzania tumepiga hatua kubwa kiasi hiki wao bado wamelala usingizi mzito.
Sisi tunatengeneza Magari, electronics, kilimo uhakika wao bado wanajivuta.
Wataalamu wa uchumi,shida ni Nini kwa hawa ndugu zetu?
1. Ni wavivu sana. Wanapenda sherehe na starehe kuliko kazi

2. Hawakuipa Elimu kipaumbele. Ndiyo maana mpaka Sasa kuna raia huko wasiokuwa kusoma na kuandika. Katika Moja ya ziara zangu huko, nilibaini kuna baadhi ya vijiji vyake ambako wazazi huwashawishi watoto wao, hasa wa kike, kuandika majibu ya uongo kwenye mitihani ya darasa la saba ili wasichaguliwe kwenda Sekondari. Kwao, watoto wao kusoma kujicheleweshea mahari.

3. Mfumo wao wa uchumi walioukumbatia muda mfupi baada ya uhuru ulichangia kwa kiasi kikubwa kukwamisha kasi ya Maendeleo.

4. Mipango ya kukurupuka. Kila Rais anayeingia madarakani anaingia na Mipango yake na kupelekea baadhi ya iliyoanzishwa na watangulizi wake kutupiliwa mbali au kuwekwa kando kwa muda.

5. Watu wake wengi hawana exposure na mambo ya mataifa mengine. Katika ukanda wake, inaweza ikawa ndiyo nchi inayoongoza kwa watu wake kutokwenda nchi zingine. Hata utoaji tu wa passport ni nongwa haswa. Hawatoi passport mpaka kusudi la safari lithibitishwe. Wakati mwingine, huweza kutakiwa hata kuonesha tiketi ya ndege kabla ya kupewa passport.

6. Ubinafsi nao umetawala. Hiyo imepelekea rushwa kutamalaki. Wakati fulani, ilishawahi kupewa na jina lililopunguza makali, badala ya rushwa, ilibatizwa jina la takrima.

7. Hawaamini katika uwajibikaji. Kwao, kiongozi wa umma ni bosi, siyo kama kwetu ambako kiongozi ni mtumishi wa umma. Viongozi wetu wanajitahidi sana kutumika kwa uaminifu kwa sababu wanajua wakizembea tutawawajibisha.
 
Unachanganya mambo, miaka hiyo ilikuwa ni English monarchy kwa hiyo ni english monarchy ndiyo iliyokuwa sawa au zaidi ya Korea lkn siyo sisi, sisi hatujawahi kuwa sawa au kumzidi yoyote yule kiuchumi, …
 
Back
Top Bottom