Miaka 90 ya ILO: Ajira zitolewa kama nafasi za ubunge na uraisi

fiksiman

JF-Expert Member
May 17, 2008
402
104
Siku chache zijazo kabla ya kusherehekea miaka 45 ya Muungano, shirika la Kazi duniani (ILO) wataadhimisha miaka 90 tokea kuundwa kwa taasisi hiyo ya kimataifa. Kwanza niwapongeze wana jumuiya hiyo hasa wale walio katika nchi zinazoendelea kama ya kwetu hapa Tanzania. Miaka 90 ndugu yangu si mchezo mdogo!!!

Naomba kutoa Hoja sasa: Hivi karibu waziri wa kazi, ajira na maendeleo ya vijana alizungumza na waandishi na kukiri kuwa takribani watanzania 48,000 wameshaachishwa kazi kwa kile kilichodaiwa "MTIKISIKO" wa uchumi duniani. Na aliendelea kwa kusisitiza kuwa takwimu hizo ni sasa na zimewagusa zaidi wafanyakazi waliokatika ajira rasmi (hapa sikosei anamaanisha wale walamba unyunyu na mufindi huko mijini). Kwa maana nyingine ni hivi, wale wabangaizaji na ndugu zangu pale mtaa wa kongo, lango la jiji pale mji wa mawe na maeneo mengine wamesalimika. Samahani hawa wamepona kwa kuwa hawajulikani kirahisi...(tafsiri yake hapa waziri anatuambia hata mapato yanakusanywa kutoka kwa watu hawa "hayajulikana" kama si kutaka kujenga mazingira ya ufisadi nini?) haya hiyo sio hoja nayotaka kuileta maana wakubwa wameshatuulia kale kamjadala ketu ka dowans na EPA eti kisa wanasema kuna sijui DECI matapeli sasa wewe inakuhusu nini? Si waachieni wanausalama wafanye kazi zao.

Kiukweli haingii akili waziri mkubwa anautangazia umma eti watu fulani matapeli achaneni nao....ukitusiwa utasema nini mmh?? Acha haya mambo ya kutegana bana eboo!!! Kama mnaona watu hawafanyi vitu kwa utaratibu basi mi nadhani waachieni wenye kazi zao wasimamie zaidi ya hapo mi nitapata hisia mnataka kutuhamishia mijadala yetu ya msingi ona hata mimi naanza kuhama kwenye hoja yangu nayota kuileta.

Nilikuwa wapi...eeh ndio ni suala la miaka 90 ya ILo na Ajira nchini. Sasa nilikuwa nasema hivi...ilikuondoa tatizo la ajira nchini na malalamiko ya kukosa mitaji mi nataka kutoa pendekezo: Kama wabunge, madiwani na hata Mjomba anapewa muda wa miaka 5..kwanini ajira zisitolewa kwa mpango huo ili kama watu wanaiba waibe waondoke zao tutajua moja kuwa walikuwa wanatengeneza mtaji wa baada. Hebu tuchukulie mfano wabunge, ile mijihela wanayopewainatosha kabisa kwenda kuanzisha maisha ya kifahari au wenye akili kama waziri mkubwa wa ya tatu wanaanzisha mahekalu na mashamba makubwa ya mang'ombe. Kisha anakula pensheni tuu.

Kwahiyo wanajamii wenzangu hoja ndo hiyo "ajira zote zitoke kwa awamu na hakuna najira ya milele eti hadi miaka 60 ndo mtu aache" na hao vijana watakuwa wapi muda huo???

Hebu angalie hivi vigezo hivi je tutafika kwa mpango huu......The ideal candidate will have:

A Master's degree in communication or a related field
Proven experience in donor reporting
An understanding of education policies and practices in East Africa
Excellent writing and editing skills
Experience of at least 5 years in a similar position
(2 positions: 1 for Kenya, 1 for Uganda)
 
Back
Top Bottom