Miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika1961: All Muslim National Union of Tanganyika (AMNUT) 1959

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,922
30,271
MIAKA 60 YA UHURU WA TANGANYIKA 1961: ALL MUSLIM NATIONAL UNION OF TANGANYIKA (AMNUT)

Uchaguzi wa Kura Tatu ulisababisha farka ndani ya TANU na wa kwanza kujitoa katika chama alikuwa Zuberi Mtemvu akaunda African National Congress (ANC) chama hiki kikajulikana kama Congress katika umaarufu wake.

Wanachama wake wakaweka kibwagizo cha maneno haya katika kukisifu chama chao, ''Congress Mwamba Usiovunjika.''

Baada ya Mtemvu kutoka TANU, Mashado Ramadhani Plantan na yeye akajitoa TANU akaunda All Muslim National Union of Tanganyika (AMNUT).

Hiki chama kilisababisha hofu kubwa sana na si tabu kuelewa kwa nini.

Zuberi Mtemvu chama chake kilikuwa kimesimama kwenye sera ya Afrika kwa Waafrika lakini chama cha Mashado Plantan kiliangalia maslahi ya Waislam baada ya uhuru hofu ikiwa Waislam kutotendewa haki na wale watakaoshika madaraka.

Kitu gani killisababisha hii shaka?

Ukoloni uliwanyima Waislam elimu, elimu ikawa katika mikono ya serikali na Wamishionari.

Ikawa wazi kuwa uhuru utakapopatikana watakaoshika madaraka ya kuendesha nchi watakuwa Wakristo.

Swali likawa, je hawa Wakristo wakiongozwa na Julius Nyerere watafanya uadilifu kuona kuwa Waislam wanatendewa haki na watapata fursa za elimu kama wengine?

AMNUT ikadai kuwa uhuru ucheleweshwe hadi pale Waislam watakapo kuwa na elimu ya kushiriki katika uendeshaji wa serikali.

Dai hili lilipingwa na TANU kwa mantiki kuwa hali ya baadae ya Waislam si suala la kujadiliwa na Waingereza waliokuwa wanaitawala Tanganyika.

Suala la Waislam hili litatatuliwa na serikali huru ya Tanganyika.

Huu ndiyo ulikuwa msimamo wa TANU na ahadi ya TANU kwa Waislam wa Tanganyika.

Katika hotuba yake maarufu ya kuaga alipostaafu aliyoitoa Ukumbi wa Diamond mwaka wa 1985 Mwalimu Nyerere aliwaeleza Wazee wa Dar es Salaam aliokuwa anawahutubia kuwa ametimiza ahadi yake ya kuleta usawa baina Waislam na Wakristo kiasi kuwa hawezi kujua waziri anayemteua ni Muislam au Mkristo.

Akasema hawezi kujua imani ya anaemteua hata kama jina lake litadhihirisha dini yake.

Angalia picha ya Mashado Plantan iliyopigwa siku ya kufungua ofisi ya African Association mwaka wa 1933.

Juu yake ni picha ya Zuberi Mtemvu wakati akiwa kiongozi wa Congress.

Soma barua ya AMNUT hapo chini:

Screenshot_20211201-120203_Facebook.jpg
 
Back
Top Bottom