GHOST RYDER
JF-Expert Member
- Jun 10, 2011
- 1,025
- 475
View attachment 34967
Nimevutiwa na dukuduku hili nililolifumania jana likitafutiwa ufumbuzi na mamlaka husika bila kupata jibu nikaamua kujaribu kutafuta ukweli wake mwenyewe kwa niliyoyasikia kwa kulinganisha ya ukweli wak ama ni hofu tu kwa mjadala niliousikia.
Kibo kya ndesi, Huwezi kuamini tunasherehekea miaka 50 ya uhuru na nembo za kutosha tu. Sasa ipi ni ipi, Viongozi wenye mamlaka hili wanalijua zaidi yetu...tuuite uzembe, uchakachuaji , ubadhilifu, uhujumu au kukosa umakini kulikopitiliza kwa wasimamizi wa mamlaka husika.
Bado nashindwa kujua mintarafu ya huu mkanganyiko, ni kwamba hili limefanyika kwa makusudi, ubunifu wa watanzania au ujanja ujanja ujanja wa kurahisisha mambo, huu ni msalaba mwingine kwa serikali.
Kibaya nembo zote zinatumika katika machapisho mbalimbali ya serikali hata katika wavuti za ofisi kadhaa za viongozi wa serikali wanaokwenda na nguvu ya kiteknolojia nao kila mmoja katika wavuti ya ofisi yake ana nembo ya aina yake kuanzia ofisi ya Rais, waziri Mkuu hadi mawaziri wengine...Aaah Tanzania.
Zichunguze kwa makini hizo nembo hapo juu uone watanzania tulipofikia sasa.
Wabunge huko mjengoni hebu tutafutieni majibu kwa waziri husika, kama hawa jamaa wa jana nilivyokuwa nawasikia wakirushiana mpira na kila mmoja akionekana kushangaa na macho pima kama mjusi aliyebanwa na mwango,
ADIOS