Miaka 50 ya UDSM!

Apollo

JF-Expert Member
May 26, 2011
4,920
3,221
Maazimisho ya miaka 50 ya chuo kikuu cha Dar es Salaam. Hebu tufikirie...ndani ya miaka hiyo, serikali imefanikiwa kwa yapi na imeshindwa kwa upande upi?

Kwangu mimi naona miaka 50 ni mingi sana kitanzania, chuo kilitakiwa kiwe kimepiga hatua kubwa sana. Bado kuna dosari nyingi zinazoonyesha uzembe upo..... Mpaka leo kuna vitanda wanalala watu wawili wawili, uhaba wa majengo ya hostel, vifaa vya kazi....hii inasikitisha sana. Pia chuo kina miaka mingi wakati kuna watoto wa wakulima bado hajanufaika japokuwa ni kikongwe.

HESLB V/S TCU.......Katika program yangu, tupo watu 9 tu wenye mkopo, wote waliobakia hawana mikopo. Just imagine. Inasikitisha sana, sijui field watafanyaje.

Jk atakuwepo, atakuwepo pia na Rais Museven, kuna maswali mengi itambidi ajibu, maana sasa serikali inatuona sisi wanafunzi ni wajinga na hatujui wanachokifanya. Inabidi tum'bane mpaka kieleweke kesho.

Nasikitika kusikia kuwa sherehe imeangukia kwenye msiba wa mwanafunzi mwenzetu. Mungu ailaze roho ya marehemu, mahali pema peponi.
 
Back
Top Bottom