Miaka 4 baadaye: Kikwete vunja bodi ya Mikopo!

sizungumzii mabadiliko ya muundo tu, nazungumzia kuwatimua wanabodi wote, na ikiwezekana kuwatupa kwenye genge! Halafu kuwaweka watu ambao wanajua nini maana ya kutoa mikopo ya elimu!!
mwanakijiji
historiaa inaonyeshaa huwa wakiondolewa hawa wanawekwaa walee..pitia mifano ya Bodii mbali mbali ujuazoooo..

mfumoo bado hauruhusuu ufanisiii..
 
Habari Leo

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, imekataa taarifa iliyowasilishwa na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kwa kuitaka menejimenti ikutane nayo mwezi ujao Dodoma kujadili namna ya kuiendesha kwa tija na ufanisi.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Estheria Kilasi, alisema jana Dar es Salaam kuwa kamati haikukubaliana na maelezo ya uongozi wa Bodi hiyo kuhusu utekelezaji wa maelekezo waliopewa katika kikao kilichopita.

Kilasi, ambaye ni Mbunge wa Mbarali, alisema Bodi imeshindwa kutoa maelezo ya kuridhisha kuhusu matumizi, ukusanyaji usioridhisha wa mapato, na kushindwa kutoa taarifa iliyokamilika.

Kwa mujibu wa Kilasi, matumizi ya jumla na kiwango cha fedha kilichotumika kwa ajili ya posho ni kikubwa. Kasoro nyingine zilizoainishwa na kamati ni pamoja na Bodi hiyo kushindwa kukusanya madeni kutoka kwa watu waliopata mkopo kutoka kwenye Bodi hiyo.

Kamati pia ilieleza kushangazwa na kitendo cha Bodi kushindwa kutoa maelezo kuhusu namna mkopo wa Sh bilioni 58 kutoka Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) unavyolipwa.

Jambo lingine lililofanya kamati ikatae ripoti ni kutokana na kile ambacho Kilasi alisema HESLB imeshindwa katika ripoti yake kutoa maelezo ya namna ambavyo watatumia Sh bilioni 21 zilizoahidiwa kutolewa na Wizara ya Fedha na Uchumi.

Kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti huyo, wakati wa Mkutano wa Bunge ujao, watakaa na viongozi wa Bodi katika kikao kitakachomshirikisha pia Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi pamoja na Waziri wa Fedha na Uchumi.

Lengo la kikao hicho ni kujadili namna ya kusaidia bodi hiyo kufanya kazi kwa ufanisi na tija.

Wakati huo huo, Kamati imeitaka Bodi kumthibitisha Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Yusuf Kisare katika nafasi hiyo baada ya kubaini kwamba tangu Januari 2007 amekuwa akikaimu.

Mkurugenzi wa HESLB, George Nyantega aliieleza kamati kwamba walishawasilisha majina Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwa ajili ya kupata mhusika, lakini hadi sasa hawajapata jibu.

My Take:
Hivi uzembe unatakiwa uvumiliwe hadi miaka mingapi? Kweli mnafikiria watu wale wale watabadilika na mara moja kuwa watendaji kazi wazuri mkiwapa fedha zaidi!? Please Mr. President, just sack this stupid board, would you?

Mmh,kazi ipo.
 
Teuzi za KISIASA na KISHIKAJI na gharama zake. Sio bure lakini. Iko namna ya kufaidika na teuzi hizi.
 
sizungumzii mabadiliko ya muundo tu, nazungumzia kuwatimua wanabodi wote, na ikiwezekana kuwatupa kwenye genge! Halafu kuwaweka watu ambao wanajua nini maana ya kutoa mikopo ya elimu!!

Mzee, wishful thinking! Katika Tanzania ya leo kweli tutegemee hayo kutokea na kuweza kuibuliwa watu wa aina hiyo unayoelezea? Hata kama wapo, katika system iliyokengeuka kiasi hiki nani atahangaika kuwatafuta na kuwaona?
 
Habari Leo

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, imekataa taarifa iliyowasilishwa na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kwa kuitaka menejimenti ikutane nayo mwezi ujao Dodoma kujadili namna ya kuiendesha kwa tija na ufanisi.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Estheria Kilasi, alisema jana Dar es Salaam kuwa kamati haikukubaliana na maelezo ya uongozi wa Bodi hiyo kuhusu utekelezaji wa maelekezo waliopewa katika kikao kilichopita.

Kilasi, ambaye ni Mbunge wa Mbarali, alisema Bodi imeshindwa kutoa maelezo ya kuridhisha kuhusu matumizi, ukusanyaji usioridhisha wa mapato, na kushindwa kutoa taarifa iliyokamilika.

Kwa mujibu wa Kilasi, matumizi ya jumla na kiwango cha fedha kilichotumika kwa ajili ya posho ni kikubwa. Kasoro nyingine zilizoainishwa na kamati ni pamoja na Bodi hiyo kushindwa kukusanya madeni kutoka kwa watu waliopata mkopo kutoka kwenye Bodi hiyo.

Kamati pia ilieleza kushangazwa na kitendo cha Bodi kushindwa kutoa maelezo kuhusu namna mkopo wa Sh bilioni 58 kutoka Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) unavyolipwa.

Jambo lingine lililofanya kamati ikatae ripoti ni kutokana na kile ambacho Kilasi alisema HESLB imeshindwa katika ripoti yake kutoa maelezo ya namna ambavyo watatumia Sh bilioni 21 zilizoahidiwa kutolewa na Wizara ya Fedha na Uchumi.

Kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti huyo, wakati wa Mkutano wa Bunge ujao, watakaa na viongozi wa Bodi katika kikao kitakachomshirikisha pia Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi pamoja na Waziri wa Fedha na Uchumi.

Lengo la kikao hicho ni kujadili namna ya kusaidia bodi hiyo kufanya kazi kwa ufanisi na tija.

Wakati huo huo, Kamati imeitaka Bodi kumthibitisha Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Yusuf Kisare katika nafasi hiyo baada ya kubaini kwamba tangu Januari 2007 amekuwa akikaimu.

Mkurugenzi wa HESLB, George Nyantega aliieleza kamati kwamba walishawasilisha majina Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwa ajili ya kupata mhusika, lakini hadi sasa hawajapata jibu.

My Take:
Hivi uzembe unatakiwa uvumiliwe hadi miaka mingapi? Kweli mnafikiria watu wale wale watabadilika na mara moja kuwa watendaji kazi wazuri mkiwapa fedha zaidi!? Please Mr. President, just sack this stupid board, would you?

Tulipokuwa mbele ya wakati..
 
Back
Top Bottom