Miaka >30 ijayo: ni vitu gani utasimulia kwa wanaozaliwa sasa kuhusu "Enzi Hizo"?

The Inquisitive

Senior Member
Oct 27, 2010
177
29
Kuna thread hapa inataka utaje vitu vya enzi za zamani ambavyo unadhani vijana hawakuviona ila wamesikia tu. Yametajwa mambo mengi ya mavazi, usafiri, mambo ya kijamii n.k. Basically reminiscing about the past. Naona wengi wana kumbukumbu za kufurahisha kuhusu enzi hizo.

Nikiwa nasoma hizo comments nimejiuliza, miaka >30 ijayo likiulizwa swali kama hili vitatajwa vitu gani? Mtakaokuwa watu wazima/wazee wakati huo mtasimulia nini kwa wajukuu?

Mimi kati ya nitakayosimulia: enzi hizo tulikuwa na blog iliitwa Jamiiforums ilikuwa moto wa kuotea mbali, hata serikali ilikuwa inaigwaya...
 
mie nadhani nitasimulia kwamba nchi hii ishawa kuongozwa na Mfalme Juha ambaye alikua anahusudu sana kutalii nchi za Mabepari, na nimehifadhi mipicha yote aliyopiga na Boyz II Men, Steven Seagal nk
 
Kabla ya kuforecast utakuja simulia nini, kwanza juilize utakuwepo?maana hapo tu ulipo hata 40 hujagonga lakini umechoka mbaya hata km 5 huwezi tembea!
 
Kucheza kiduku! Rafikiangu ana POP mguuni baada ya kucheza kiduku akiwa na viatu virefu!
 
Msijisifu kwa ajili ya kesho maana hamjui yatakayozaliwa na siku moja, basi yatosha maovu yenu ya siku enyi wa kizazi cha nyoka.
.
"WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI".
 
Back
Top Bottom