Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa JamiiForums...

Binafsi nimejifunza mengi sana kupitia jamii forum nawapongeza sana waazilishi kwa kazi nzuri sana
 
Tarehe na mwezi sivikumbuki. Lakini ninachokikumbuka ni mwaka. Mwaka huo ni 2006.

Baada ya 'condor dragon' kufanya mambo yake kule bcstimes.com, baadhi yetu tulijikuta hatuna pa kwenda kubadilishana mawazo kama tulivyokuwa tumezoea.

Mijadala ya bcstimes.com ilikuwa moto kweli kweli. Ingawa ilikuwepo mitandao mingine kama vile Youngafricans.com, tanzatl.org, darhotwire, n.k., bcstimes.com ndiyo ulijipambanua kuwa mtandao ulio makini zaidi kuliko mingine iliyokuwepo kwa wakati huo hususan kwenye vuguvugu la uchaguzi wa 2005.

Kwa wakati huo mtu kama ulitaka kupata habari moto moto kutoka jikoni basi hukuwa na budi kwenda huko.

Nakumbuka vizuri kabisa jinsi ambavyo Mzee ES [FMES - Field Marshal Emergency System], ndiye aliyekuwa kinara wa kutupakulia hizo habari moto moto kutoka jikoni.

'Condor dragon' alipofanya mambo yake wachache tukahamia TEF [Tanzania Economic Forum].

TEF ikabadilika ikaja kuwa JamboForums mnamo mwezi Agosti 2006. Baadaye [sikumbuki mwaka] JamboForums ikabadilika ndo ikaja kuwa hii JamiiForums tuliyonayo leo.

Kusema ukweli kama mwaka 2006 ungeniambia kwamba JF itadumu kwa miaka 10 ningekuona majinuni.

Ningekuona hivyo kutokana na ukweli wa kwamba huko nyuma uhai wa majukwaa kama haya ulikuwa haudumu kwa muda mrefu.

Mwanzoni mwanzoni kabisa [1996 au 1997] kulikuwepo na Nyenzi.com lakini ikaja kufa. YA nayo ikaja ikadumu kwa miaka 3 au 4 lakini hatimaye ikafa. Tanzatl.org nayo ikafuata mkondo huo huo.

Kwa hiyo halikuwa jambo la ajabu kudhani kuwa huenda JF nayo ingefuata mwelekeo huo huo.

Lakini hilo halikutokea. Matokeo yake JF imezidi kuimarika, kukua, kustawi na sasa inajulikana mpaka nje ya mipaka ya Tanzania na naamini kuwa, ingawa mwanzoni wanachama wake wengi walikuwa ni wana-ughaibuni, hivi sasa wanachama wake wengi wako Tanzania.

Katika hii miaka 10 JF imepitia changamoto nyingi sana. Kuna kipindi wamiliki wake walikamatwa na kuwekwa ndani [@Maxence Melo unaweza kunisadia hapa kama nimekosea].
LINK: Maxence Melo, Mike Mushi arrested

Kuna wakati ilifikia ikataka kufungwa kutokana na gharama za uendeshaji kuzidi kuwa kubwa lakini wanachama wakaiokoa kwa michango yao.

Kuna mijadala ambayo watu walishikana makoo na kurushiana kila aina ya maneno makali.

Moja ya mijadala hiyo ni kumhusu marehemu Dr. Ferdinand Masau. Nimejaribu kuutafuta huo uzi ili niweke kiunganishi chake hapa lakini nimeukosa. Natumaini Invisible atasaidia.
*UZI: Sakata la Dr. Masau: Msimamo wa Serikali na Hatima ya Taasisi ya Moyo (THI)

Mwingine ulikuwa ni ule wa uchaguzi mkuu wa Marekani mwaka 2008. Huu uzi sitausahau kamwe: US Election Coverage 2008

Nyuzi ingine ambayo ilivutia watu ni ile iliyohusu kukamatwa kwa aliyedaiwa kuwa ndiye aliyekuwa akiendesha ile blogu ya ZeUtamu.
UZI: Ze Utamu Blogger under arrest?

Siwezi kuzikumbuka mada zote motomoto kwani zipo nyingi sana. Zingine na wengine mtaongezea mnazozikumbuka.

Miaka 10 baadaye, nikiangalia JF ilipotoka na ilipo sasa, licha ya misukosuko ya kila aina ambayo baadhi yetu tumeipitia, kwa ujumla wake nafarijika sana.

Na nina imani kwamba, kama tumeweza kudumu kwa mwongo mzima basi bila ya shaka tunaweza kuendelea kuwepo tena kwa mwongo mwingine.

Sasa, miaka 10 ni mingi. Na katika kipindi hiki kuna wanachama wenzetu ambao hatunao tena hapa duniani. Kwa hao nasema wapumzike kwa amani huko waliko.

Pia, kuna wengine ambao tulianza nao lakini kwa sababu moja ama nyingine wameacha ushiriki wao humu. Kwa hao nasema, kwanza hongereni kwa kusimama kidete siku za mwanzoni maana bila nyie [au niseme bila sisi] hii JF ya leo isingekuwepo. Ingependeza sana kama walau mngejitokeza kwa ajili ya haya maadhimisho.

Kuna wakati mtu ulikuwa unajikuta upo mwenyewe tu humu unarandaranda kama kichaa. Lakini watu hatukuchoka wala kukata tamaa.

Hivyo basi, ningependa kuwatambua na kuwapa heshima zao wanachama wakongwe wote [waliojiunga mwaka 2006 na 2007] waliolianzisha hili jukwaa letu kwani wao ndio walijenga msingi ambao JF ya leo imeukalia.

Ningependa kuwataja wachache ninaowakumbuka:

Mzee Mwanakijiji Rev. Kishoka Augustine Moshi Kyoma Mwawado Mkandara Kibunango Steve Dii Mwafrika wa Kike Kichuguu Choveki Masatu Masanja Quemu Mlalahoi Mtanzania Bibi Ntilie Game Theory jmushi1 Zakumi Moelex23

Na wengineo wote ambao nimewasahau.

Je, wewe mdau una lipi la kusema kuhusu JF yetu? Una kumbukumbu gani kuhusu JF? JF imekusaidiaje?

Kwa Maxence Melo na Mike McKee, je, mna mpango wowote ule ulio rasmi kuhusu kusherehekea haya maadhimisho?

Hongera JF kwa kutimiza miaka 10!!!
USA byb
 
Historia ya mijadala hii kwangu mimi ilianza miaka ya 90 na muhimu ilikuwa ni Tanzanet. Hii ilikusanya wa-TZ wengi walioko ughaibuni kwa hamu yao ya taarifa za nyumbani. Ikawa kujua habari za magazeti ni muhimu sana. Kupitia kitengo cha kompyuta pale UD wakati huo kikiwa kimeanza, tuliweza kupata taarifa za nyumbani.

Mijadala ya Tanzanet ilikuwa ktk nyanja zote na hasa siasa na hata technolojia. Tatizo, hii haikuwa blog. Ilikuwa ni e-networking. Nyenzi.com alianza kipindi hicho na mijadala mingine ilikuwa sumu hadi kukabana kama unavyosema. Nakumbuka mjadala wa "Punguwani Mwakasisi" ulivyoleta balaa ndani ya Tanzanet. Lakini pia Tanzanet iliokoa matatizo ya kifamilia. Namkumbuka m-TZ aliyefia Japan na kupitia Tanzanet tulichanga ili mwili wake uweze kuzikwa na si kuchomwa kama ilivyo Japan.

Ktk hii Jamiiforums nimejifunza umuhimu wa anonymity. Kumbe Binadamu akificha utambulisho wake: anasema ukweli zaidi ya anavyoweza, Anakuwa shujaa zaidi ya anavyoweza, pia atajidai kujua zaidi ya anayoyajua. Ni sahihi kuwa na kura ya siri ili hata rafiki wa karibu akukatalie kuwa kiongozi.

Bado niko ughaibuni, lakini sasa sihitaji kuletewa taarifa za magazeti. JF inaleta hata mambo ya dk moja iliyopita lakini pia magazeti yako mtandaoni.

Kwa uzoefu wangu huenda wengine watanishangaa ninavyojibu hoja ndani ya JF, lakini naomba nitoe ushauri kwa vijana wanaojiunga JF. Enzi hizi ni kujifunza kitu kipya kila siku kwa yule anayetaka. Naomba vijana JF isiwe sehemu ya kuja tukana usiowapenda kwa dini, siasa , nk. ni sehemu ya kuongeza ufahamu na kujifunza busara. Usijifunze ubishi hata yale usiyoyajua. Someni kwa ubora wa akili zetu. Dunia hii inahitaji wenye mwanga na siyo shabiki wa fulani.
 
Ukipitia comments page za website nyingi na kupitia forums nyingi; anonymity inafichua sana the dark side of humans. Matusi na comments zisizo na staha unaziona kila mahali; kama ambavyo JF political discussions zilivyo siku hizi. Ili uone point inabidi uwe emotional mega filter unayeweza kupitia matusi, kejeli, mizaha, uzandikiki, n.k. bila kuvutwa navyo. Nadhani hilo limedhibitika kuwa gumu sana kwa walio wengi. Mtu akitaka kuvuruga mjadala fulani huingiza tu tusi, kejeli, mzaha, n.k. kisha utaona mara moja mjadala ukivurugika.

Kitu kingine ambacho wengi tumejifunza ni kuwa mijadala ya kujadili watu na mambo yao ina nguvu sana; maana yake ni kuwa wale wanaoitwa simple minds (wanaopenda sana kujadili watu) ni wengi sana katika jamii yetu - hata katika kundi la wale ambao wanaitwa wenye mwanga (waliosoma si haba).
 
Watanzania wengi wanapenda kujadili watu
 
Hahaha,asante mkuu

Mkuu Kimbunga wiki iliyoisha nilikuwa Itagagumba nimeona wakazi wa huko wanakausha dagaa mwenye majani wanalalamika dagaa za kwenye mchanga siyo nzuri.

Nyani Ngabu umenikumbusha huyu mtu anaitwa mzee mwanakijiji kuna mada fulani aliianziasha jambo forum akaniambia niingie jambo forum niisome kuanzia hapo nilikuwa mpenzi wa jambo forum hata ilipobadilika bado nilikuwa msomaji nzuri sana ila nimechelewa sana kujiunga, sijui huyu jamaa yupo wapi sasa nina mfahamu sana sijamuona miaka mingi sana zaidi ya kumi

Nakumbuka wakati nipo chuo kikuu rafiki yangu ndio alinigusia kuhusu jf,hiyo ilikuwa ni 2009,there after nikawa naingia kama guest mpk nilivyojiunga rasmi 2012,kiukwel jf is never boring, nimekuwa niki enjoy sana pamoja na kujifunza for all these years pricelessly. Shukurani sana kwa waanzilishi wa mtandao huu
 
Back
Top Bottom