Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa JamiiForums...

Hii siwezi isahau imenipa mume mwaka wa 12 now ,tulianzia kutaniana DHB mpk kuonana na mpk kuoana ahahahaaaaa
Hongera sana. Nadhani sio ndoa yenu tu, kuna ndoa kadhaa ambazo ni zao la makutano ya JF Chit chat. Hongereni sana
 
Tarehe na mwezi sivikumbuki. Lakini ninachokikumbuka ni mwaka. Mwaka huo ni 2006.

Baada ya 'condor dragon' kufanya mambo yake kule bcstimes.com, baadhi yetu tulijikuta hatuna pa kwenda kubadilishana mawazo kama tulivyokuwa tumezoea.

Mijadala ya bcstimes.com ilikuwa moto kweli kweli. Ingawa ilikuwepo mitandao mingine kama vile Youngafricans.com, tanzatl.org, darhotwire, n.k., bcstimes.com ndiyo ulijipambanua kuwa mtandao ulio makini zaidi kuliko mingine iliyokuwepo kwa wakati huo hususan kwenye vuguvugu la uchaguzi wa 2005.

Kwa wakati huo mtu kama ulitaka kupata habari moto moto kutoka jikoni basi hukuwa na budi kwenda huko.

Nakumbuka vizuri kabisa jinsi ambavyo Mzee ES [FMES - Field Marshal Emergency System], ndiye aliyekuwa kinara wa kutupakulia hizo habari moto moto kutoka jikoni.

'Condor dragon' alipofanya mambo yake wachache tukahamia TEF [Tanzania Economic Forum].

TEF ikabadilika ikaja kuwa JamboForums mnamo mwezi Agosti 2006. Baadaye [sikumbuki mwaka] JamboForums ikabadilika ndo ikaja kuwa hii JamiiForums tuliyonayo leo.

Kusema ukweli kama mwaka 2006 ungeniambia kwamba JF itadumu kwa miaka 10 ningekuona majinuni.

Ningekuona hivyo kutokana na ukweli wa kwamba huko nyuma uhai wa majukwaa kama haya ulikuwa haudumu kwa muda mrefu.

Mwanzoni mwanzoni kabisa [1996 au 1997] kulikuwepo na Nyenzi.com lakini ikaja kufa. YA nayo ikaja ikadumu kwa miaka 3 au 4 lakini hatimaye ikafa. Tanzatl.org nayo ikafuata mkondo huo huo.

Kwa hiyo halikuwa jambo la ajabu kudhani kuwa huenda JF nayo ingefuata mwelekeo huo huo.

Lakini hilo halikutokea. Matokeo yake JF imezidi kuimarika, kukua, kustawi na sasa inajulikana mpaka nje ya mipaka ya Tanzania na naamini kuwa, ingawa mwanzoni wanachama wake wengi walikuwa ni wana-ughaibuni, hivi sasa wanachama wake wengi wako Tanzania.

Katika hii miaka 10 JF imepitia changamoto nyingi sana. Kuna kipindi wamiliki wake walikamatwa na kuwekwa ndani [@Maxence Melo unaweza kunisadia hapa kama nimekosea].
LINK: Maxence Melo, Mike Mushi arrested

Kuna wakati ilifikia ikataka kufungwa kutokana na gharama za uendeshaji kuzidi kuwa kubwa lakini wanachama wakaiokoa kwa michango yao.

Kuna mijadala ambayo watu walishikana makoo na kurushiana kila aina ya maneno makali.

Moja ya mijadala hiyo ni kumhusu marehemu Dr. Ferdinand Masau. Nimejaribu kuutafuta huo uzi ili niweke kiunganishi chake hapa lakini nimeukosa. Natumaini Invisible atasaidia.
*UZI: Sakata la Dr. Masau: Msimamo wa Serikali na Hatima ya Taasisi ya Moyo (THI)

Mwingine ulikuwa ni ule wa uchaguzi mkuu wa Marekani mwaka 2008. Huu uzi sitausahau kamwe: US Election Coverage 2008

Nyuzi ingine ambayo ilivutia watu ni ile iliyohusu kukamatwa kwa aliyedaiwa kuwa ndiye aliyekuwa akiendesha ile blogu ya ZeUtamu.
UZI: Ze Utamu Blogger under arrest?

Siwezi kuzikumbuka mada zote motomoto kwani zipo nyingi sana. Zingine na wengine mtaongezea mnazozikumbuka.

Miaka 10 baadaye, nikiangalia JF ilipotoka na ilipo sasa, licha ya misukosuko ya kila aina ambayo baadhi yetu tumeipitia, kwa ujumla wake nafarijika sana.

Na nina imani kwamba, kama tumeweza kudumu kwa mwongo mzima basi bila ya shaka tunaweza kuendelea kuwepo tena kwa mwongo mwingine.

Sasa, miaka 10 ni mingi. Na katika kipindi hiki kuna wanachama wenzetu ambao hatunao tena hapa duniani. Kwa hao nasema wapumzike kwa amani huko waliko.

Pia, kuna wengine ambao tulianza nao lakini kwa sababu moja ama nyingine wameacha ushiriki wao humu. Kwa hao nasema, kwanza hongereni kwa kusimama kidete siku za mwanzoni maana bila nyie [au niseme bila sisi] hii JF ya leo isingekuwepo. Ingependeza sana kama walau mngejitokeza kwa ajili ya haya maadhimisho.

Kuna wakati mtu ulikuwa unajikuta upo mwenyewe tu humu unarandaranda kama kichaa. Lakini watu hatukuchoka wala kukata tamaa.

Hivyo basi, ningependa kuwatambua na kuwapa heshima zao wanachama wakongwe wote [waliojiunga mwaka 2006 na 2007] waliolianzisha hili jukwaa letu kwani wao ndio walijenga msingi ambao JF ya leo imeukalia.

Ningependa kuwataja wachache ninaowakumbuka:

Mzee Mwanakijiji Rev. Kishoka Augustine Moshi Kyoma Mwawado Mkandara Kibunango Steve Dii Mwafrika wa Kike Kichuguu Choveki Masatu Masanja Quemu Mlalahoi Mtanzania Bibi Ntilie Game Theory jmushi1 Zakumi Moelex23

Na wengineo wote ambao nimewasahau.

Je, wewe mdau una lipi la kusema kuhusu JF yetu? Una kumbukumbu gani kuhusu JF? JF imekusaidiaje?

Kwa Maxence Melo na Mike McKee, je, mna mpango wowote ule ulio rasmi kuhusu kusherehekea haya maadhimisho?

Hongera JF kwa kutimiza miaka 10!!!

- Duh hii post imenikumbusha mbali sana U know hahahahaha, Salute mamen kwa this thinking enzi hizo "WHEN WE WERE THE JAMBO FORUMS" hahahahaha kuna members ambao ni lazima kuwakumbuka hapa daima like:- Mwanakijiji, Field Marshall ES, Mwanasiasa, Nyani, Rufiji, Lunyungu, Philemon Michael, Zitto, 50Cents, na wengineo.

MAY GOD BLESS JAMIIFORUMS!!

le Mutuz Nation
 
Respect ma man!
 
Nikiondoka bila kuchangia huu uzi ntakua sijatenda wema kweli Mungu ibariki JF, Mungu bariki member wake walioanza toka mwanzo na wale ambao kwa namna moja au nyingine hatunao/hawatumii tena hii site kwani mchango wao umetupa kitu hapa. Ujasiri na uchapakazi wa hali ya juu wa waanzilishi wa JF ni kitu cha kujifunza kwa kweli, unaposakamwa sana we komaa ndio mafanikio yanakuja hapo. Umakini na uangalifu/uongozi mzuri wa hawa watu hakika ni jambo la kujifunza,
Nimeanza kuuona huu mtandao 2013 ila sikuupa uzito but mda ulivyozidi kwenda niliona hii nimsehemu ya kipekee sana kuelezea mambo yako ya ndani kwa usiri na usalama wa hali ya juu halafu uzuri huku ni ma great thinker! nimepata elimu kubwa sana na matatizo yangu ya mwaka jana nimesaidiwa, sure kwa neema za Mungu kama nisingeingia hapa ndani nadhani mafanikio niliyonayo ungekuta sina na ni mtu niliyekata tamaa.
God bless JF, Long live JF.
 
- Duh hii post imenikumbusha mbali sana U know hahahahaha, Salute mamen kwa this thinking enzi hizo "WHEN WE WERE THE JAMBO FORUMS" hahahahaha kuna members ambao ni lazima kuwakumbuka hapa daima like:- Mwanakijiji, Field Marshall ES, Mwanasiasa, Nyani, Rufiji, Lunyungu, Philemon Michael, Zitto, 50Cents, na wengineo.

MAY GOD BLESS JAMIIFORUMS!!

le Mutuz Nation
Pamoja sana Le Baharia, You know, JF imekubalika sana nchini.
 
Pamoja sana Le Baharia, You know, JF imekubalika sana nchini.

- Kuna siku moja miaka ya nyuma ilikuwa ni Sherehe za Kuzaliwa kwa JF Miaka mingi ya nyuma nilitabiri kwamba one day hiki chombo kingekuja kuwa kama kilivyo sasa, Salute kwa Max and Mike na hasa Mwanakijiji hawa ndio the Pillar of this forums, hii thread imenikumbusha mbali sana na all the things we went through kutoka tulikotokea,

- Ninakumbuka uchaguzi wa Rais Mwaka 20005 na jinsi moto ulivyokuwa unawaka hapa na habari zote za ndani hahahaha, ninakumbuka Taifa zima lilivyokuwa linasubiri habari zote kutokea hapa, ninakumbuka zile enzi kikao cha Kamati Kuu kinaendelea hapa tunapiga info za kikao mwanzo mpaka mwisho word to word, ninakumbuka siku Mzee Mkono anakuja kusoma hapa JF uamuzi wa Kamati Kuu kumuengua kinyang'anyiro cha Mwenyekiti wa Wazazi, hata kabla kikao hakijaisha hahahahaha,

- Ninakumbukia Max anakamatwa na kule US Mwanakijiji anakamatwa, ninakumbuka JF tuanachangishana na mambo mengine behind the scene mpaka kuwatoa, ninakumbukia JF imekwama kwa kukosa funds ya kuiendesha na ninakumbuka kufwa kwa BCS Times na kuhamia Jambo Forums kwa kweli Mungu akibariki hiki chombo na ni matumaini yangu historia itawakumbuka FAIRLY wale wote waliojitoa kwa kila kitu kuifanya JF ifike hapa,

- My Super Salute always ni kwa Max, Mike, Mwanakijiji, Zitto na Philemon Michael hawa watu wamejitoa sana for what I know kuisimamisha na kuifikisha JF hapa ilipo, najua kuna wengine wengi sana lakini ninarudia for what I know hawa ndio waliopigana sana kuwepo kwa JF mpaka leo!!

MUNGU IBARIKI JF NA AIBARIKI TANZANIA

Le Mutuz Nation
 
Wakongwe wa JF utawajua tu.

Historia wanayo kiganjani.

Massive big up!
 
Nakumbuka ilikua 2009 nilikua namshawishi rafk yangu ajiunge Facebook akaniambia hawezi ila kama ninaweza nijiunge jamiiforum, nikawa namshangaa maana ilikua kitu kipya kwangu basi akaanza nielezea toka hapo nikawa msomaji mzuri tu ila sikutaka kuwa na ID. Mwaka 2014 wakat nna ujauzito nilikua ninahitaji ushauri kuhusu mambo ya ujauzito ikabidi nijiunge ili nipost na kupata msaada ninaohitaji. Hapa ndiyo ninapata vitu vingi sana kuliko sehemu yoyote idumu JF
 
Dah,tumetoka mbali sana, nakumbuka majukwa yote yalikuwa kwa wote, then tukaanza kuzibagua baadhi zikawekwa ni maalum kwa members na mengine ikawa hadi upewe access ili kuzifikia. vile vile wakati jamboforums ikibadilika kuwa jamii sikuwa aware nikashtukiza siku nataka kuingia jambo nakutana na jamii ilikuwa supprise sana.
hakika kuna kila 7bu ya kujipongeza kwa kutimiza muongo miaka 10
 
Back
Top Bottom