Mhe.Tundu Lissu ndani ITV

up date
-Operation wahalifu hawakukamatwa maana watendaji walikuwa wanasikiliza mamlaka ya uteuzi.

Tujenge mfumo mzuri wa sheria tena kwa lugha yetu ili watanzania waelewe sheria zetu. Zanziba wameweza lugha rasmi na ya kutunga sheria ni ya Kiswahili kama wao wameweza sisi tumeshindwa nini?

Tujikomboe kifikra.

up date
Tatizo la kesi kuchukua muda mrefu ni tatizo la kimahakama kwani kuna utaratibu wa kisheria wa kesi kutochukua muda mrefu mahakama wanapuuza puuza utaratibu huo.
Mfano Nimeshitakiwa 2002 mamuzi 2008 ni tatizo la kimahakama wanapuuza utaratibu

Tumewashauri kuna machache mengi wamepuuza.
 
Lissu anapiga misumari,wabunge wengi hawajui kingereza ila wanatunga sheria kwa kingereza...
 
sijui kwa nini hawakumweka kwenye tume ya katiba, angefaa sana kwa elimu yake ya kisheria..

mkuu huko kwenye sheria huwa ana wachanganya wengi hasa viongozi wake.

Kumpeleka kwenye tume ni kutaka kuwapotosha wananchi, inapofika kwenye maswala kama haya ana kuwa na jaziba sana.

Lakini kwa leo naona ana stahili pongezi.
 
Mfumo wa waingereza walituachia. Kila wakati wanasema watatafsiri lakini utekelezaji ni dhaifu.
 
Jitekenyeni na kucheka enyi magamba , nipo nafanya finishing kata ya Kisesa kwa Mabina the late
 
Anasema Rais yupo juu ya sheria na kwa mantiki hiyo watendaji wote wanaoteuliwa na Rais nao wako juu ya sheria..
 
mbutika huelewi anachozungumza halafu unaishia kusema anaropoka.
 
Mbunge wa Singida Mashariki na Waziri kivuli wa sheria na katiba, mh Tundu Lissu amedai kuwa 100% ya Watanzania wanazungumza Kiswahili na hawajui kingereza.
Anasema kwamba Sheria za nchi zinazotungwa na bunge huandikwa kwa kingereza wakati WABUNGE walio wengi ndani ya bunge hawajui kingereza, ndio maana wakati mwingine baadhi ya Wabunge huishia kupiga Makofi na kupitisha mambo mengi kwa kuwa hawajui Kilichoandikwa.

Source; ITV DK 45 na Emmanuel Buhohela
 
ukiwa ccm lazina uwe pun gu one!

Yaani nyie kupingwa hamtaki, nyie mnataka kupinga tu! Wewe na wenzio mtakubali badala ya calling names.

Nyie wabaya ni ccm tu viongozi wenu, wateule. Achana na ujinga tune supersport 3 uone tofauti.
 
Hahaaaaaa lissu bhana....imagine kuwa miongoni mwa wabunge hao ni kepteni j komba
 
Kila siku wanasema wamefunga Mjadala kumjadili Zitto lakin kila wanapoenda hawamalizi hoja zao bila ya kumtaja Zitto. Zitto anasubiri wamalize kutoa Karata zao ili nae aanze Kujibu hoja kwa hoja sio tusi wala kubeba katuni za Majeneza, na uchaguzi wa June lazima achukue fomu za kuwania Uenyekiti wa Chadema ili wamnyime asimamishe uchaguzi mpaka kesi ya msingi isikilizwe. Patamu hapo. Tundu Lissu angekubali Ushauri wa Kujiuzulu Zitto na Kitila kwenye CC ya Chama yote haya yasingetokea. Chadema lazima ilipe gharama za kuchanganya Uanaharakati na Sheria.
 
Sina imani na mtoa hoja, kuna uwezekano mkubwa wa kupotosha, maana ni kifaranga cha wasaliti !
 
KATIBA: Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria, Tundu Lissu, kupitia ITV kipindi cha dakika 45 amesema ameshitushwa na ukimya wa Vyombo vya habari wa kutoendesha mijadala ya Katiba Mpya.
 
uongo. Najua wewe learned lawyer ni pro magamba. Kuna post nyingine hapa ya ukweli. Mods ondoeni hii imetiwa chumvi na inapotosha.

mkuu umeangalia toka mwanzo kipindi cha dakika 45? Mwanzo kabisa wa kipindi na maswali yalikuwa ni kuhusu mgogoro wa chama chake na alikubali kabisa na sina sababu ya kumsingizia.
 
Back
Top Bottom