Mhe. Shibuda na kisukuma bungeni, ni msisitizo au kuchekesha bunge?

hengo

JF-Expert Member
Jun 6, 2011
402
50
Heshima kwenu wanajamvi.Baada ya mihangaiko jana nilijikaza nikaa kusikiliza mjadala wa mbunge kuhusu bajati ya Wizara ya kilimo na umwagiliaji.

Pamoja na uchovu nilifanya hivyo kwa vile kilimo ni uti wa mgongo wa watanzania na ndo ajira kwetu sisi wale 80%.Waheshimiwa wengi walituwakilisha kikamilifu japo bado wanaendelea na tabia ya kusifu na kushukuru wake zao,watoto na wajukuu.Kilicho nishangaza zaidi na wakati wa kutoa hoja zake MHE:JOHN SHIBUDA MAGALE -Mbunge wa Maswa mashariki -Chadema kutumia lugha ya kisukuma wakati akihitimisha hoja zake huku akitaja jina la Waziri mkuu.

Je, waziri mkuu na Waziri wakilimo Prof.Maghembe wanaelewa kisukuma?Kama hawaelewi watawezaji kuelewa matatizo ya Wananjchi wa Maswa kama Shibuda anatumia kisukuma mjengoni?Alidhamiria nini,kusisitiza hoja,kuchekesha kama kawmaida yake au hakupenda aeleweke kwa walengwa?Naomba maoni yenu wanaJF kuhusiana na hili.
 
Kwa ruhasa yako nakuu baadhi ya maneno niliyo yakarili hasa baaba ya kufafanuliwa na best yangu 'Ng'wanangwa ntale Mizengo bhabha bhambelijagi ambalimi yongezeke ibei ya buluba"Mengine sikuyaelewa.Je huu ni ungwana?
Hujaeleweka, kwani alisemaje maana sio wote wanasikiliza bunge siku hizi.....
 
Kwa ruhasa yako nakuu baadhi ya maneno niliyo yakarili hasa baaba ya kufafanuliwa na best yangu 'Ng'wanangwa ntale Mizengo bhabha bhambelijagi ambalimi yongezeke ibei ya buluba"Mengine sikuyaelewa.Je huu ni ungwana?
Ndugu Nyani Ngabu tafsiri tafadhali...
 
Labda ni njia ya kutaka Lugha ya Kisukuma itumike Bungeni, wanaona labda waislamu sasa hivi wanavaa Kanzu na Koti kwa wanaume au wanawake na baibui kuziba nywele...

Sheria ni Msumeno!!!
 
I don't think if MP shibuda made a mistake in sending the message to the relevant person. Mizengo Pinda anakinyaka sana Kisukuma, Shibuda hapo alimaanisha "Mkuu bwana Mizengo, watengenezeeni wakulima bei ya pamba" hiyo ni tafsiri ya maneno uliyoweza kuyakariri.
 
Watanzania bwana wana utumwa wa fikra sana!
Mbunge akiongea lugha ya Tanzania inakuwa kituko, lakini Mbunge akiongea Kiingereza anaonekana ana akili nyingi
 
Kwa ruhasa yako nakuu baadhi ya maneno niliyo yakarili hasa baaba ya kufafanuliwa na best yangu 'Ng'wanangwa ntale Mizengo bhabha bhambelijagi ambalimi yongezeke ibei ya buluba"Mengine sikuyaelewa.Je huu ni ungwana?
atakuwa kampa waziri mkuu tafsiri ya hayo maneno, ila wenzake wasijue alichoongea
 
Kwa ruhasa yako nakuu baadhi ya maneno niliyo yakarili hasa baaba ya kufafanuliwa na best yangu 'Ng'wanangwa ntale Mizengo bhabha bhambelijagi ambalimi yongezeke ibei ya buluba"Mengine sikuyaelewa.Je huu ni ungwana?
Mkuu natangaza maslahi kabla sijachangia mimi ni msukuma, kama hakuvunja kanuni ya bunge hakuna kosa, na maana yake ni kama ifuatavyo, nitatafasiri neno moja moja kabla ya kutafsiri sentensi nzima, Ng'wanangwa- kilikuwa ni cheo ambacho kinatumika kwa wasaidizi wa mtemi, ntale- mkubwa, bhabha-baba; na mara nyingi hutumika sana kuadress mwanaume yeyote unayemheshimu bila kujali kama ni baba yako mzazi, bambelijagi- wasaidieni, abalimi-wakulima, yongezeke-iongezeke, ibei-bei, ya-ya, buluba-pamba.

kwa ujumla alikuwa anamuomba waziri mkuu Mizengo kama msaidizi mkuu wa rais wawasaidie wakulima ili bei ya Pamba iongezeke.
 
Mie msukuma, lakini kila mwenye lugha yake akiruhusiwa kutumia mjengoni siafiki kama tutafika. Kama kanuni ziko kimya basi busara zitumike kudhibiti hili. Msabaha enzi zile alitumia kizaramo na papohapo kutoa tafsiri. Huyu kama hakufanya hivyo ati kwa sababu Mizengo ananyaka kisukuma si ustaarabu. Si wangeongea wenyewe tu basi, kwa nini mjengoni? Nisihukumu sana kwani sikumsikia Shibuda, pengine alitafsiri. Taratiibu tunaweza kuwa tunapanda mbegu ya ukabila bila kujua. Unataka usaidiwe na waziri mchagga kwa kumwambia kwa kichagga ili a'feel' kwamba ni mwenzako! Kwa hili simo.
 
Heshima kwenu wanajamvi.Baada ya mihangaiko jana nilijikaza nikaa kusikiliza mjadala wa mbunge kuhusu bajati ya Wizara ya kilimo na umwagiliaji.Pamoja na uchovu nilifanya hivyo kwa vile kilimo ni uti wa mgongo wa watanzania na ndo ajira kwetu sisi wale 80%.Waheshimiwa wengi walituwakilisha kikamilifu japo bado wanaendelea na tabia ya kusifu na kushukuru wake zao,watoto na wajukuu.Kilicho nishangaza zaidi na wakati wa kutoa hoja zake MHE:JOHN SHIBUDA MAGALE -Mbunge wa Maswa mashariki -Chadema kutumia lugha ya kisukuma wakati akihitimisha hoja zake huku akitaja jina la Waziri mkuu.Je, waziri mkuu na Waziri wakilimo Prof.Maghembe wanaelewa kisukuma?Kama hawaelewi watawezaji kuelewa matatizo ya Wananjchi wa Maswa kama Shibuda anatumia kisukuma mjengoni?Alidhamiria nini,kusisitiza hoja,kuchekesha kama kawmaida yake au hakupenda aeleweke kwa walengwa?Naomba maoni yenu wanaJF kuhusiana na hili.

Kheri yako kaka wewe una generator!!
 
Mkuu natangaza maslahi kabla sijachangia mimi ni msukuma, kama hakuvunja kanuni ya bunge hakuna kosa, na maana yake ni kama ifuatavyo, nitatafasiri neno moja moja kabla ya kutafsiri sentensi nzima, Ng'wanangwa- kilikuwa ni cheo ambacho kinatumika kwa wasaidizi wa mtemi, ntale- mkubwa, bhabha-baba; na mara nyingi hutumika sana kuadress mwanaume yeyote unayemheshimu bila kujali kama ni baba yako mzazi, bambelijagi- wasaidieni, abalimi-wakulima, yongezeke-iongezeke, ibei-bei, ya-ya, buluba-pamba.

kwa ujumla alikuwa anamuomba waziri mkuu Mizengo kama msaidizi mkuu wa rais wawasaidie wakulima ili bei ya Pamba iongezeke.

Masuke kweli wewe ni msukuma,hata JINA LAKO `` MASUKE`= maziwa yaliyo chekechwa.Nashukuru kwa ufafanuzi wako mkuu
 
'Ng'wanangwa ntale hengo, naona imla ulikuwa unapata zote kwa zote, ha ha ha ha. Au siyo.... I like this. We are the children of Africa bana. kuna ubaya gani kutumia rasilimali yatu ya lugha...

Kwa ruhasa yako nakuu baadhi ya maneno niliyo yakarili hasa baaba ya kufafanuliwa na best yangu 'Ng'wanangwa ntale Mizengo bhabha bhambelijagi ambalimi yongezeke ibei ya buluba"Mengine sikuyaelewa.Je huu ni ungwana?
 
"A people without the knowledge of their past history, origin and culture is like a tree without roots" Marcus Gacha
Big up Shibuda, Kisukuma mpaka mahakamani
 
Back
Top Bottom