Mhe. Chikawe, CCM na Tanzania viliuacha ujamaa lini?

"Enzi zile za mfumo wa ujamaa na chama kimoja cha siasa, hilo lingewezekana lakini wakati huu ambao nchi inatumia mfumo wa kibepari, haiwezekani," alisema Chikawe.
.

Oooh kumbe tupo kwenye UBEPARI pasee kwamba mwenye nguvu ya pesa ndiyo wa kusikilizwa, sasa nakubali kwa mtaji huu RA na wenzake HAWATAKAMATIKA.
 
anakamatika ila waliopewa mamlaka yakuwakamata wanamsubiri JK hadi aseme, dunia ya kwanza mtu akiapa kuilinda katiba na sheria za nchi yake kweli anawajibika kulinda maslahi ya UMMA si maslahi binafsi ya Rais, hawa kina DPP wanamuogopa RA kwasababu ya upatina wake na JK, wanahofu iwapo watamkamata kabla ikula haijasema vibarua vyao huwa shakani, hawapo pale kwa maslahi ya Taifa ila kulinda wala rushwa ambao ni maswahaba na mzee aka bwana mkubwa.
hebu tazama kasi ya kujiuzulu ya watu wa usalama kule USA na UK baada ya Blair na Bush Kuingiza nnchi katika matatizo yza vita ya Iraq, makamanda wawili USA waliachia ngazi kupinga kuiingiza nchi kwenye mission ambayo ingefail, hawakua wanasiasa hawa , walikua watendaji wanaolinda maslahi ya UMMA.
angalia DPP, SIJUI ANAFANYA NINI, Inafikia mahala watendaji wa idara nyeti wanarumbana hadharani wakitupiana mpira, hapo ndo ujue hawapo kwa maslahi ya umma, ila kulinda mkate wao wa kila siku.
hawafanyi lolote hadi ikulu iseme kamata yule na sasa JK kauchuna kuwaambia kamata RA, Manji ama mzee wa vijisenti.
 
rais alikutana na baraza la mawaziri na hicho ndicho walichozungumza, kikwete aliwaomba wale wanaojuwa sheria wamuokowe na sasa ndiyo wanatoka kumuokowa, eti waziri wa katiba na sheria, sasa wakati sokoine akifanya aonavyo yeye sivyo, yeye alichukuwa hatuwa gani, yaaani nyie acheni tu, lakini inasikitisha na kuuma sana jinsi tunavyopelekwa pelekwa, yani hao watu wamepewa dhamana kubwa na serikali, sasa wewe mwakyembe kama ni mpiganaji kweli na huko kwa uchungu wa nchi yako, umuonyeshe kwenye hiyo ripoti yako sehemu zote zinazoonyesha kwamba rostam ni mwizi. siyo mnatuzuga zuga hapa.
 
Ni jambo la busara kufanya uchunguzi na kujiridhisha kabla ya hatua yoyote ya kisheria. Hata hivyo swali la kujiuliza, ni kwa nini uchunguzi uchukue muda mrefu hata kwa masuala ambayo yako wazi kabisa. Kwa mfano, Kagoda Agriculture ni kampuni ambalo lilisajiliwa na wameliki wake lazima wamo kwenye jalada la usajiri pale BRELA. Inakuwaje masuala ya msingi utendaji wake unakuwa wa kisiasa zaidi? Na kama ni kufuata sheria au utaratibu, inakuwaje Rais huyo huyo ambaye hawezi kuwa juu ya sheria aweze kusamehe watu ambao hata mahakamani hawajafikishwa? Tunakumbuka siasa zilivyotumika katika suala zima la EPA, eti Rais akaagiza waliojichotea fedha BOT kinyemela warudishe na kusamhewa? Mimi hata hiyo kauli ya Chikawe naishangaa, maana inapingana na matendo yaliyotangulia ya Kikwete. Basi kama Kikwete hayuko juu ya sheria, hata suala zima la EPA asingeliingilia kabisa tangu mwaka akasubiri mhakam iamue.

Tuache siasa katika masuala muhimu yanayogusa ustawi wa taia letu! Ndiyo maana Baraza la Mawaziri la serikali yetu bado linatiliwa shaka na umma juu ya uwezo wake. Hawafanyi maamuzi kwa uchambuzi wa kisayansi na badal yake, ni kuropoka tu kama aivyosema huyo Chikawe! Ubabaishaji tuhuo. Hebu tuache mzaha, tufanye kazi tuliyoahidi kuwatumikia wananchi.
 
Sikujua kama serikali imeshatamka rasmi kuwa sasa ni ubepari kwa kwenda mbele. Kwa mtaji huo alosema mh. Chikawe Ufisadi ruksa Tz. Samaki wakubwa kuwala Dagaa/wadogo ndiyo kanuni ya Bahari na Maziwa. Uuwi Twafa!
 
aaaah Chikaweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee.....usinivunje mbavu mie
 
Ni jambo la busara kufanya uchunguzi na kujiridhisha kabla ya hatua yoyote ya kisheria. Hata hivyo swali la kujiuliza, ni kwa nini uchunguzi uchukue muda mrefu hata kwa masuala ambayo yako wazi kabisa. Kwa mfano, Kagoda Agriculture ni kampuni ambalo lilisajiliwa na wameliki wake lazima wamo kwenye jalada la usajiri pale BRELA. .
hakuna ukweli wowote kua kuna uchunguzi, SERIKALI hii imekua inaendeshwa kwa mashinikizo na imekua bingwa kuchukua maamuzi yenye sura ya kulinda siasa za chama na upuuzi mwingine. Rostam kaiweka CCM ya kikwete kiganjani , inateswa na dhambi ya kula hela za mag=fisadi wakati wa uchaguzi mkuu, wamekwama, hawawezi hata kumkemea.
 
Sikujua kama serikali imeshatamka rasmi kuwa sasa ni ubepari kwa kwenda mbele. Kwa mtaji huo alosema mh. Chikawe Ufisadi ruksa Tz. Samaki wakubwa kuwala Dagaa/wadogo ndiyo kanuni ya Bahari na Maziwa. Uuwi Twafa!

Mkuu Haruna,

Kwa definition ya serikali, tamko la waziri ni tamko la serikali. Sasa sijui unataka serikali itamke mara ngapi kwamba kwa sasa tunafuata uchumi wa kibepari. Mimi nampongeza huyu waziri kwa kuwa mkweli juu ya hili kwani wengine wanaona kigugumizi kulisema hadharani. Sikumbuki kumsikia kiongozi mwingine wa serikali akiliweka wazi suala hili.

Tiba
 
Hata kama ingekuwa kweli kwamba Tanzania inafuata Ubepari ni ubepari gani huu? Ni ubepari gani huu unaotegemea faida toka misaada ya kigeni na njia yake kuu ya kuzalisha mali ni ufisadi?
 
Hata kama ingekuwa kweli kwamba Tanzania inafuata Ubepari ni ubepari gani huu? Ni ubepari gani huu unaotegemea faida toka misaada ya kigeni na njia yake kuu ya kuzalisha mali ni ufisadi?

Hakuna ujamaa hakuna ubepari. wanatumia hoja fulani kutokana na matakwa ya wakati huo. Hapa hoja ya ubepari ina nguvu kwao. Kesho utasikia sisi wajamaa
 
Wakuu, mfumo wa nchi hauwezi kubadilishwa kwa kauli za viongozi walevi.

Ni dhahiri kabisa kuwa Chikawe (kama kweli alisema maneno hayo hapo juu) ameidhalilisha serikali na amevuja katiba ya nchi. Anatakiwa ajiuzuru mara moja kwa kutotetea Katiba aliyoapa kuitetea.

Kuna waliouliza Azimio la Zanzibar liliamua nini. Ukweli ni kwamba hakuna azimio lililoandikwa ambalo linaitwa Azimio la Zanzibar. Azimio hilo lilifanyika kihuni kwa viongozi kukaa na kukubaliana namna ya kulinda maslahi yao kwa kukubaliana jinsi wanavyoweza kufanya biashara wakiwa kwenye utumishi wa umma, na vile vile kulivunja (kwa maneno) Azimio la Arusha ambalo liliweka misingi ya uongozi wa nchi. Hivyo, hakuna Azimio la Zanzibar linaloweza kutumika kama kigezo cha namna mpya ya uongozi wa nchi, kisheria.

Mjadala wa nani amefanya nini katika wizi wa fedha za EPA hauhitaji kauli za kisiasa, kama anazotoa Chikawe. Wizi ule unahitaji hatua za sheria na kwa vitendo. Chikawe anaposema kuwa Rais hawezi kuchukua hatua za kuhakikisha kuwa sheria inafuatwa kwa kuwashitaki wahusika wa wizi wa EPA, anadhihirisha kuwa serikali imeshindwa kufanya kazi kama ilivyoapa kwa mujibu wa Katiba na kwa kutumia vitabu vitakatifu.

Lakini zaidi ya hilo, amedhihirisha pia kuwa serikali haiko tayari kuchukua hatua za kisheria kwa baadhi ya watu (ambao wana haki zaidi ya wengine wote) na wakati huo huo wakiachia hali duni zaidi kuendelea kusakama wananchi na hatua kali kuchukuliwa kwa wananchi wenye makosa madogo na ambao hawana nguvu kama hao wanaolindwa.

Vile vile, ni dhahiri kuwa serikali iko tayari kwa lolote ambalo wananchi wanaweza kuamua kufanya endapo watashindwa kuvumia hali inayoendelea ya utetezi na ulinzi wa wezi wa mali za Taifa kwa manufaa binafsi.
 
Huyu vipi?

Nani aliyemshinikiza rais amkamate RA? au EL vyombo husika vifanye kazi kwa mujibu wa sheria? waziri naona kaamua kuwasaidia mafisadi na kuwatisha DDP na PCCB wasifanye kazi zao kwa uhuru?

Kwa hiyo ubepari ni sawa na uwizi? inabidi aombe radhi kwa wananchi wa nchi zote za kibepari duniani? Nani kasema ubepari ni uwizi wa mali za umma?

anajua concept ya ubepari? kweli elimu zingine zinatia huruma? lol
 
"WAZIRI wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe amesema Rais Jakaya Kikwete hana uwezo kutumia mamlaka yake kuwapeleka mahakamani watuhumiwa wa ufisadi …(ni) …jambo ambalo haliwezekani katika mfumo wa kibepari.
"Enzi zile za mfumo wa ujamaa na chama kimoja cha siasa, hilo lingewezekana lakini wakati huu ambao nchi inatumia mfumo wa kibepari, haiwezekani…mawazo ya namna hiyo (ya kumshinikiza rais achukue hatua kali dhidi ya mafisadi) yanatokana na watu wengi kuendelea kuwa na mtazamo wa mfumo wa kijamaa na chama kimoja na kusahau kuwa tayari nchi
"Waziri huyo mwenye dhamana ya kusimamia katiba na sheria za nchi", ni mwanasheria!

Hapa Waziri Mathias Chikawe ametapikia KATIBA!

Rais, tunajua mlisoma naye hapo Mlimani. Lakini fukuza huyu mtu!
 
Hata kama ingekuwa kweli kwamba Tanzania inafuata Ubepari ni ubepari gani huu? Ni ubepari gani huu unaotegemea faida toka misaada ya kigeni na njia yake kuu ya kuzalisha mali ni ufisadi?

Hii nimecheka sana, masuala ya nchi ya kusadikika kumbe ipo na ni dhahiri.
 
Prof Shivji kwa maoni yake alisema hilo haliwezekani kwani katiba inasema kuwa tunajukumu la kujenga taifa la kijamaa na kujitegemea ambalo kwa mujibu wake katiba hiyohiyo imetoa nafasi kubwa ya kumanipulate maana halisi ya taifa linalofuata siasa za ujamaa na kujitegemea.

omarilyas

Hapana Katiba haisemi hivyo. Kama Shivji amesema hivyo inabidi arudi kuisoma tena.
 
Huyu vipi?

Nani aliyemshinikiza rais amkamate RA? au EL vyombo husika vifanye kazi kwa mujibu wa sheria? waziri naona kaamua kuwasaidia mafisadi na kuwatisha DDP na PCCB wasifanye kazi zao kwa uhuru?

Kwa hiyo ubepari ni sawa na uwizi? inabidi aombe radhi kwa wananchi wa nchi zote za kibepari duniani? Nani kasema ubepari ni uwizi wa mali za umma?

anajua concept ya ubepari? kweli elimu zingine zinatia huruma? lol
Hawa jamaa ndio reflection ya uongozi wa Taifa letu. Wanaongea ongea tu kama watu wasiokuwa na fikra. Mara nyingine kama hawana maneno bora wakae kimya maana mwisho wa siku utaweza kuta wengi wanatakiwa kwenda kupima afya za vichwa kama ziko sawasawa.
 
HIvi Chikawe alikuwa wapi wakati Rais Kikwete alipotamba kule Bungeni kuwa yeye ana nguvu sana kiasi kwamba akisema Dr. Slaa akamatwe atakamatwa?
 
HIvi Chikawe alikuwa wapi wakati Rais Kikwete alipotamba kule Bungeni kuwa yeye ana nguvu sana kiasi kwamba akisema Dr. Slaa akamatwe atakamatwa?

Mbona alishasema Zombe akamatwe na akakamatwa. Mbona alishasema Mramba, Yona, Mgonja wakamatwe na wakakamatwa. Mbona alikubali (ingawa kwa shinikizo la wakubwa wa nje) uchunguzi EPA ufanyike na wahusika wakamatwe, na baadhi wakakamatwa. Anashindwa nini waliobaki (Kagoda) nao wakamatwe.
 
Back
Top Bottom