Shetani
Member
- Oct 23, 2007
- 29
- 0
I have some breaking news on KLH News.. check it out!
Nawewe umezidi kuwa desperate kwa watu kutembelea website yako,break news hapa hapa kama unazo acha gimicks za kuvutia trafic kwenye kitovuti chako
I have some breaking news on KLH News.. check it out!
Nawewe umezidi kuwa desperate kwa watu kutembelea website yako,break news hapa hapa kama unazo acha gimicks za kuvutia trafic kwenye kitovuti chako
Hii Kali kweli, Mtu wa Pwani!! unamtanguliza mwenzako kwenye hukumu ya mwenyezi Mungu kirahisi hivyo? ama unataka kutuambia unafahamu ama ulishiriki kuchapa mapanga na unauhakika hata pona? pole pole mkuu
Yeah mwenyewe JK anasema ni "work hazards"... halafu akazimulia kwa kusema "siyo kwamba nawatishia, fanyeni kazi zenu"...
Ndio maana I love this forum, yaani Mkuu Theory, hebu weka vitu mwanangu, tuchambue mchele na pumba!
Kwa kifupi unachosema GT ni kwamba huyu mwandishi amefanya kosa la kuelewana na mafisadi kwa kukubali fedha zao lakini akaendelea kuwaumbua gazetini. Am I right? And by the same token unaelekea kutoshtushwa na yaliyompata. Am I right again?
Mkuu GT,heshima mbele,
nimesoma post yako unadai kuwa ndugu Kubenea alikuwa "anavuta hela" kutoka kwa hao mafisadi ili asiwaumbue,na kuwa kumwagiwa kwake acid ni mafarakano baina yake na hao jamaa,sasa kuna FMES alikuwa anadai ushahidi kutoka kwa baadhi yetu waliousisha tukio la kumwagiwa acid kwa Kubenea na CCM an mafisadi,na akawataka watoe ushaidi,sasa mi pia nakuuliza swali moja,hilo swala la Kubenea kuwamo katika payroll ya mafisadi unao ushahidi wake?Ikiwa hoja yako itakuwa sahihi kuwa alifarakana na mafisadi ambao humlipa (kama unavyodai wewe kulingana na ushahidi utakaoutoa hapa) basi wewe na kina ES na wenginea mtakuwa mnakubaliana nasi kuwa tukio hili la Kubenea lina mkono wa mafisadi,na kwa kuwa mafisadi ni wana CCM basi ni CCM ndo wahusika wakubwa,simple logoc will tell you that.Unless you can bring someting else out of all this.
Quote:-
"kina ES na wenginea mtakuwa mnakubaliana nasi kuwa tukio hili la Kubenea lina mkono wa mafisadi,na kwa kuwa mafisadi ni wana CCM basi ni CCM ndo wahusika wakubwa,simple logoc will tell you that.Unless you can bring someting else out of all this."
Mkuu sio mfisadi wote ni wana-CCM, na CCM has nothing to do na mafisadi, halafu ninaomba nikuambie wazi kuwa so far toka hii topic ianze GT ndiye peke yake ametoa hard evidence ya anachokisema, ninaweza kumpa some support kwa sababu wengine wote mmeshindwa kutoa angalau a hint kuhusiana na madai yenu kuwa serikali ya CCM au mafisadi ndio wanaohusika na huu uharamia,
Ninarudia tena so far ni GT peke yake ndiye anaye make a sense kwa kutoa angalau "Evidence" ku-back up theory yake, hebu na nyinyi toeni japo dataz kidogo, badala ya kuanza analysis over analysis, bila dataz, siamini 100% anayosema GT, lakini kama mjadala ukifungwa sasa theory yake inasimama tena kwa nguvu sana, kwamba Mwandishi alikuwa aki-play double stadard against the rules za uandishi, Mkuu Kithuku, lete facts tuacheni na analysis bila facts!
Please tunahitaji facts na sio itikadi na hisia, pia tunawaombea walioathirika kupona haraka warudi kutuamusha wananchi. Lakini ukisoma hapa chini GT makes a lot of sense na pia ana back-up theory yake na some "Evidence" ingawa siamini lakini angalau mnyonge mnyongeni lakini ninaichukulia hii chini as a fact unless mwingine aje naz tofauti, please enough of analysis tunahitaji facts!!
Kinachokufanya useme GT katoa "hard evidence" ni nini? So far yeye kaja na theory nyingine tu ya possible reasons za ndugu yetu kupigwa mapanga na kumwagiwa tindikali. Nasema hivyo kwasababu hakuna ushahidi wowote wa kuthibitisha kuwa alikuwa anapokea pesa toka kwa hao mafisadi unless mzee unajua zaidi ya haya yanayosemwa hapa.
FMES: Evidence aliyetoa GT kuhusu huyu bwana kuwa kwenye payroll ni ipi? Can you please show us pengine itasaidia nasi kubadili mawazo yetu.
Kubenea ambaye amepata athari katika macho yake, ameondoka muda si mrefu kuelekea India kwa matibabu zaidi ili kumuepusha na upofu.
Baraza la Vijana wa Chadema wametoa tamko hili:
IJANA WA CHADEMA TUNALAANI SHAMBULIO KWA WAANDISHI
Vijana wa Tanzania wasikubali kutumika na mafisadi
kufanya uhalifu
Vyombo vya dola vichunguze wahusika wakuu na kusudio
la shambulizi
Ni uvamizi dhidi ya haki ya kikatiba ya kupata na
kutoa habari
Kalamu za Wanahabari zina nguvu kuliko upanga wa
mafisadi
Kwa niaba ya Baraza la Vijana wa CHADEMA(BAVICHA),
vijana wa CHADEMA tunaungana na wapenda haki na ukweli
kote nchini kutoa pole kwa wanahabari Saed Kubenea na
Ndimara Tegambwage kwa kushambuliwa kwa mapanga na
tindikali. Mwenyezi Mungu awawezeshe kupona haraka
waweze kurejea katika majukumu yao ya kulijenga na
taifa na kwa namna ya pekee tunaziombea familia zako
utulivu katika kipindi hiki.
Aidha tunalaani vikali uvamizi na shambulizi hili
dhidi ya wahabari hawa na ofisi yao wakiwa katikati
ya jukumu la kuandaa toleo la gazeti kwani ni
shambulizi dhidi ya binadamu na juu ya haki ya
kikatiba ya kupata na kutoa habari.
Kutokana na mtiririko wa matukio na ushahidi wa
kimazingira, tungependa tukio hili lisichukuliwe kama
vitendo vya kawaida vya ujambazi bali lichunguzwe kama
kitendo cha kigaidi na uharamia dhidi ya waandishi wa
habari, uandishi wa habari na chombo cha habari. Si
wajibu wa wananchi kuhukumu, na ni mapema mno
kuhusisha moja kwa moja tukio hili na mtu au watu
fulani. Hata hivyo, kwa mtiririko wa matukio na
ushahidi wa kimazingira ni rahisi kutuhumu kuwa upo
uwezekano mkubwa wa uvamimizi na shambulizi hili kuwa
limefanywa na baadhi ya mafisadi wakiwatumia vijana
kufanya tendo hili la kifisadi.
Wanahabari hawa na chombo chao wamekuwa mstari wa
mbele kwa uwazi bila woga katika mapambano dhidi ya
ufisadi na kutetea rasilimali za taifa, na kuwa sehemu
ya mashujaa wa habari nchini. Mwanahalisi ni moja ya
magazeti ambayo yamekuwa mstari wa mbele katika
kuandika tuhuma za ufisadi na/au matumizi mabaya ya
madaraka zinazowakabili viongozi kadhaa wa serikali,
makampuni na taasisi mbalimbali.
Itakumbukwa kuwa, mwishoni mwa mwaka jana vyombo
mbalimbali vya habari viliandika kuhusu vitisho
vinavyotolewa kwa chombo hicho cha habari na vyombo
vyake. "Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya
habari na Mkurugenzi Mtendaji wa gazeti hilo, Saed
Kubenea, ilieleza kuwa kuna mienendo ya chinichini ya
kusambaza vitisho kwa vyombo vya habari hususan
MwanaHalisi, wachapishaji wake, wahariri, waandishi na
wachangiaji wa makala na taarifa mbalimbali.(Rejea
Tanzania Daima-28/9/2007). Hilo lilikuja baada ya
gazeti hilo kuandika habari na kuweka hadharani majina
ya waliotajwa kwenye orodha ya mafisadi.
Pamoja na kuwa jeshi la polisi limetangaza kuwatafuta
watuhumiwa vijana watatu waliohusika na uvamizi huu;
tungependa kutoa rai kwa vyombo vya dola kwamba
jitihada za uchunguzi zielekezwe katika kuwaibaini
pia waliowatuma vijana hawa kufanya uhalifu huo.
Katika mazingira ya wahalifu vijana wa kawaida, ni
vigumu kuhusisha jitihada za kulenga mwanahabari na
kummwagia tindikali machoni, hali ambayo inaashiria
shambulizi hili ni la kutumwa na mtu ama mtandao
Fulani wa watu. Kadhalika, pamoja na kuwatafuta
wahusika, vyombo vya dola vichunguze kusudio hasa ya
shambulio hilo- kama nia ilikuwa ni kuwadhuru
waandishi hawa siku hiyo ili habari Fulani isitoke au
ni kisasi kutokana na habari Fulani ambayo chombo
hicho kimekuwa kikiandika. Uchunguzi kamilifu kama huu
na hatua zitakazochukuliwa kutokana na uchunguzi huo
ni muhimu katika kulinda uhuru wa vyombo vya habari na
kulinda maisha ya wanahabari hapa nchini.
Kama kweli shambulio hili limefanywa na watuhumiwa hao
kwa kutumwa na fisadi ama mtandao Fulani wa
mafisadi wanaotapatapa, basi tunasikitishwa na pia na
jinsi ambavyo habari na mwanahabari
wanavyochukuliwa. Tunakumbusha kuwa mwanahabari ni
mjumbe tu wakufikisha ujumbe katika jamii; ambaye
anapaswa kulindwa na kuheshimiwa. Tabia inayoanza
kuchipua ya kumshambulia mjumbe au chombo
kilichofikisha ujumbe tena kwa njia ambazo ni kinyume
cha sheria na ustaarabu wa binadamu badala ya
kuushughulikia ujumbe wenyewe; ikiachwa ikashamiri
inaweza ikatishia ufanisi wa sekta ya habari ambayo
inapaswa kudumishwa kama mhimili wa nne wa dola.
Serikali ni vyema ikalichukulia suala hili kwa uzito
wake, kwani vitendo kama hivi vya wanahabari
kushambuliwa vikiendelea vinaweza kuhamia kwa watetezi
wengine wa haki; na hali hii ikiachwa itazalisha chuki
miongoni mwa jamii na hatimaye jamii itaanza kutoa
hukumu ya umma(mob justice) kwa wanaotuhumiwa kufanya
vitendo kama hivi vya kifisadi.
Aidha tunachukua fursa hii kutoa mwito kwa vijana kote
nchini kutokubali kutumika kufanya vitendo vya
uhalifu, na tunatoa rai kwa jamii kuwataja
wanaowatumia vijana kufanya vitendo hivyo vya kinyama.
Fisadi yoyote aliyetayari kuyaweka rehani maisha ya
watanzania waliowengi kwa ufisadi wake hawezi
kushindwa kuweka hatarini maisha ya mtanzania mmoja
ambaye anachimbua ufisadi wake na kumweka katika
mstari kuhukumiwa; hivyo vijana wasikubali kuingia
katika mtego huu wa kufanya kazi za mafisadi. Mwisho,
tunawaomba vijana wote nchini wakiwemo vijana
wanahabari kuendeleza harakati za kutetea haki na
ukweli kwa kutumia uandishi wenye kuchochea fikra
mbadala zenye kuleta demokrasia na maendeleo nchini.
Vitisho visirudishe nyuma uandishi wa habari wenye
kupambana na ufisadi na kutetea rasilimali za Taifa
kwani kalamu za wanahabari zina nguvu kuliko upanga
wa mafisadi
John Mnyika
Mkurugenzi wa Vijana
0754694553
Tunasubiri mabaraza ya vijana wa vyama vingine nao kutoa matamshi yoyote yale.
KAMA ALIKUWA HANA LA KUSEMA ..SIJUI KWA NINI AKAENDA PALE..rais anategemewa kila jambo analofanya liwe ni statement ya maelekezo..sio maneno shallow tu ya juu juu yasiyoweka muongozo..
kama hakuwa na ujumbe aliopanga kuufikisha kwa ziara ile[as certain gesture] rather angeabakia ikulu acheze karata kwenye laptop yake ..au kutuma mails kwa marafiki....akisubiria kuonana na watu wa ODM
Gharama za matibabu zimechangiwa na "wadau mbalimbali wa habari" na serikali si mmojawapo waliochangia.. as far as I know.. na kwenda India wengi wanapelekwa India hata watoto wenye matatizo ya moyo..