Mhando kukaangwa kabla ya ripoti ya Ngwilizi

EmeraldEme

Senior Member
Mar 8, 2012
116
20
Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO inakutana leo muda huu ili kumuondoa Mkurugenzi Mtendaji Injinia William Mhando licha ya kwamba tume huru ya kumchunguza imemkuta hana makosa. Lengo kuu ni ku pre empty report ya Ngwilizi.

Mambo mbalimbali ambayo kamati ya Ngwilizi ilichunguza ni kama ifuatavyo:

Uagizaji wa Misumari
Kamati ilichunguza na ikabainika kuwa misumari iliagizwa mwaka 2004(wakati huo Mhando alikua Zonal Manager-Southern Higherlands)kipindi ambacho TANESCO ilikuwa ikiongozwa na NETGROUP SOLUTIONS ya SouthAfrica, na bidhaa hiyo ilikosewa, ikaja kuwa rectified wakaleta bidhaa husika.

NGUZO:
Kamati ilibaini kuwa sio kweli kwamba nguzo zinaagizwa Sao na kupelekwa Nairobi kisha kuletwa hapa kwa kivuli cha kuwa zimeagizwa South Africa. Kamati ilipata taarifa za uagizaji wa nguzo kutoka South africa Revenue Board, Kenya Revenue Authority na Tanzania Revenue Authority.

Kamati huru ilifuatilia tuhuma za kampuni za Mc Donald live line na ile ya St Clara ambapo zote ilikuja kugundulika kuwa yalikuwa ni majungu tu na hakuna ukweli wowote. Zaidi sana, hata process za tender zilifanywa na kufuatwa kulingana na Sheria na zilikua approved na Mwanasheria wa TANESCO.

Bodi ya Wakurugenzi imeagizwa kwenda kinyume na taarifa hiyo ili kumuondoa kazini Mhando. Kimsingi kazi ya bodi ilipaswa kusubiri taarifa ya Ngwilizi na maazimio yake ili kuona hatua zinachukuliwa.

Nia ya kufanya uchunguzi sio kumuonea mtu, ila kuacha haki itendeke, kwa mtoa tuhuma na kwa mtuhumiwa.

Source: kutoka ndani ya kamati zote 2.
 
Hiyo kamati iliundwa na nani? kama ni upande wa Bunge majibu ya yaliyotolewa ni sawa,kwani baadhi ya wabunge nao ni watuhumiwa,ilitakiwa iundwe tume huru.
 
Tangu lini hapa kwetu tanzania

1. Wanaoshikwa na dawa za kulevya wakathibitika, baada ya uchunguzi kuwa na makosa huishia kusafishwa?

2. Tangu lini hapa kwetu tanzania wanasiasa na waheshimewa mbalimbali wakakutwa na kashifa kama sio kila siku tume za geresha na kusafishana? Hata ile ya Richmond nini kimetokea hadi hivi leo? imeishia ....

Tume, sijui kamati, nk, nk, nk, haziaminiki hapa kwetu ni upuuzi tu na matumizi mabaya ya kodi zetu.
 
mhando na waziri wa nishati hawawezi kufanya kazi pamoja...mmoja wao inabidi aondoke kwa manufaa ya shirika...sa watajua wenyewe nani aondoke amwache mwenzie
 
Nadhani hapa unachanganya madawa,.....
1. Mahando alisimamishwa na board ya tanesco, na walikuwa na matatizo yao ambaya wanayajua na walikuwa wanayafanyia kazi
2. Tume ya Ngwilizi ilikuwa inachunnguza tuhuma za rushwa kwa wabunge....kwa maana kuna wabunge watano (5) walihongwa na watu wanaofaidika na biashara ya Tanesco ili wapingane na maamuzi ya wizara ya madini na nishati, na ikiwezekana wantoe waziri na katibu

kama kuna kikao cha board ya Tanesco hakiwezi kujadili ya Kamati ya ngwilizi

Kama waaamua kufukuza kazi au kumrejesha kazini, itakuwa ni kwa sababu ya uchunguzi wao
 
hii taarifa imeletwa na mtu yupo karibu na Mhando'kwa tuhuma alizo nazo Mhando hawezi kurudi tena kazini'ila atalipwa chake atembee mbele'nyie ndio mliofaidika na uongozi wake kaeni pembeni kwani Muhongo na Muhando hawawezi kukaa meza moja
 
mhando na waziri wa nishati hawawezi kufanya kazi pamoja...mmoja wao inabidi aondoke kwa manufaa ya shirika...sa watajua wenyewe nani aondoke amwache mwenzie

Kwa hiyo hata kama hana makosa inabidi aondoke ili ampishe Waziri?
 
Kwa hiyo hata kama hana makosa inabidi aondoke ili ampishe Waziri?

hivi kweli wewe unaamini mhando hana makosa? migao ya umeme ilivyokua inaendelea chini yake..hayo madili ya nguzo na misumari hata kama hakua yeye anahusika moja kwa moja bt huo ufisadi umefanyika chini yake so yeye kama kiongozi lazima awajibike
 
Siasa zikiingia sehemu tu....zinafuruga mambo.....watu wanaweka kando taaluma.....taarabu inachukua nafasi....yetu macho
 
Nadhani hapa unachanganya madawa,.....
1. Mahando alisimamishwa na board ya tanesco, na walikuwa na matatizo yao ambaya wanayajua na walikuwa wanayafanyia kazi
2. Tume ya Ngwilizi ilikuwa inachunnguza tuhuma za rushwa kwa wabunge....kwa maana kuna wabunge watano (5) walihongwa na watu wanaofaidika na biashara ya Tanesco ili wapingane na maamuzi ya wizara ya madini na nishati, na ikiwezekana wantoe waziri na katibu

kama kuna kikao cha board ya Tanesco hakiwezi kujadili ya Kamati ya ngwilizi

Kama waaamua kufukuza kazi au kumrejesha kazini, itakuwa ni kwa sababu ya uchunguzi wao

asante kwa kumrekebisha mtoa mada aliyekurupuka na kukoroga chai ya maziwa ya mgando.
 
tuambie na tuhuma za kujipa tenda kwenye kampuni mkurugenzi mkewena mwanae?hapo ulisahahu kufikiria mkuu kajipange ulete nyingine ukiweza na sisi tuhonge tukukubalie mbona kawaida sana
 
Back
Top Bottom