Mh. Zitto Kabwe mgeni Rasmi siku ya mavuno kanisa katoliki Ilala

Safety last

JF-Expert Member
Mar 24, 2011
4,227
1,389
Mbunge wa kigoma kaskazini zito kabwe kesho december 11 atakuwa kanisa Anglican (mt Nikolai) ilala katika sherehe za siku ya mavuno ibadani hapo wote mnakaribishwa kumuunga mkono kamanda wetu , source tangazo kanisani na Clouds fm!
 
CCM NDIO WAMEANZA KAMPENI ZA makanisani sasa zimesambaa hadi CHADEMA. Wakati wa uchaguz 2010 Kikwete alilalamika Udini Lakini Lowasa wa CCM alipo anza kwenda Makanisani hakulalamika.Leo Chadema wameanza kualikwa Makanisani utasikia moto!
 
HIVI KWENDA MAKANISANI/MSIKITINI NDIYO UDINI ???? Tafuta tafsiri ya UDINI itakusaidia
 
Hapo ndipo wanaponifurahishaga cdm full kujichanganya na raia. Goooo makamanda. Mtaacha historia nzuri ktk taifa hili. Mungu awabariki sana. Lolote litakalofunguliwa duniani na mbinguni vivyo hivyo.
 
kama ni kweli, it is a big plus kwa opposition campi.
kwa muda mrefu madhehebu (makanisa) mengi yamekuwa yakikwepa kuonekana yanaji-associate na wapinzani.
 
Naona ushauri wa mwalimu mkuu wa watu hauzingatiwi kabisa. yeye alishauri kuwa kumualika mtu wa dini nyingine kwenye kanisa/msikiti wako sio sawa kwasababu anawaona mnafanya kitu ambacho kwake hakina maana ndio maana JK aliropoka kanisani kwamba kuna maaskofu wanauza unga ingekuwa ni muumini wa dini ile hasingeweza kusema vile kwa kuwa pale sio forum ya kutoa matamko ya mtindo huo.
Lakini kwa kuwa tumeamua kuonesha sisi wamoja acha tuendelee hivyohivyo jambo haioneshi ushirikiano wowote kwani maeneo mengine ukiacha sehemu za harambee lugha ni ileile udini.
Inabidi utafute namna ya kutibu/kuondoa huu udini kwa kuwachukulia hatua wale wote wanaosambaza chuki za kidini. Kushiriki tu harambee za dini tofauti hakutibu/hakuondoi udini.
Mtazamo wangu.
 
Inaelekea kuna watu hawajui hata maana ya mavuno lakini ndiyo wa kwanza kuanza kujadili. Mgeni rasmi anaweza kuwa mwanasiasa/waziri/mbunge, mfanyabiashara nk bila kujali dini yake. Hi watanzania wamekuaje mpaka kila kitu lazima wakitazame kwa miwani ya udini?
 
Mada inajadilika ukichukulia kasi ya wanasiasa kuingia makanisani kijinadi inazidi kukua. Wakati kanisa linawaharika kwa madhumuni ya kiimani, wanasiasa wanatumia nafasi hiyo kijinadi na kupigana vijembe.

Lakini kuna makosa kwenye title ya hii mada. "St Nicholas and African Martyrs Cathedral" la ilala ni kanisa la Anglican, na ndio makao makuu ya Kanisa hilo na ni makazi ya Askofu Valention. L. Mokiwa. Kanisa la katoliki la ilala na msimbazi linaitwa "Kanisa katoliki msimbazi parish" na sio st, Nikolai. Marekebisho yanaitajika kwenye title ya hii mada.
 
Nimekupata mkuu !

Mavuno yanahitaji mtu wa kuhamasisha, ndo maana wakamuita kamanda. Angeitwa mtu kama Wassira angeshusha morali ya waumini, na hakuna ambacho kingepatikana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom