comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,939
Wana- jamvi,
Kutokana na kulegalega kwa hali ya vyama vya mikopo kama vile Vicoba, Saccos na hali ya mabenki, hali ya fedha katika jumuiya mbalimbali au vikundi vilivyojiunga kupata fedha kutoka taasisi hizo kuwa mbaya,
hali hii inamgusa moja kwa moja kwani yeye ndio Msajili wa Hazina ndio Msajili wa hizo taasisi na msimamizi mkuu wa kuendesha fedha katika maeneo hayo.
Hali ya fedha katika taasisi hiyo ni mbaya, wakopaji wanakosa mikopo vilevile Vicoba au Saccos kukosa fedha za kukopesha wanavikundi, kwa maana hiyo Msajili ameshindwa kusimamia taasisi hizo hasa katika kutoa mgao wa fedha kwenda kwenye taasisi na vikundi hivyo.
Kama kweli Mh. Rais unampango wa kuwaneemesha wananchi kupitia vikundi na taasisi hizo basi tengua uteuzi wa Msajili wa hazina na utafute atakae kuwa mbunifu ili hali ya uchumi kwa mwananchi mmoja mmoja ili nzuri.