Mh Rais, Taifa linahitaji tiba - Godbless Lema

Hii quote ya Martin imenigusa, siku zote mimi huwa sina wasiwasi na hizi pokopoko za waislam dhidi ya wakristo, MOU, OIC, mahakama ya kadhi etc kwasababu mimi si muumini wa hizi dini zilizoletwa na majahazi.
Hata hivyo kuna siku vita ya msaraba inaweza kurudi tena eti? Unakuta kizuizi barabarani wanakuuliza dini gani,ukisema ya asili unakula panga! Asante Mh.Lema!
 
JK atamsikiliza huyu kweli halafu sio ajabu hata haya maneno ameandikiwa na Zitto.

Duh.... ni aibu kijana kuwa na kauli legevu hivi?We una hakika gani kuwa Zitto anaweza andika hilo?unajua misimamo yake kidini?Kwani yeye ni mwandishi wa hotuba?

Pengine unamsikia Lema kwa mbali, unamwona katika picture ,ila hujabahatika spend nae muda kidogo.Halafu uone kwanini akimkaribia mwana ccm asi humwacha akiwa na mashaka kuhusu ufuasi wake na CCM.Simply jamaa ni Gifted katika Majukwaa.Waulize CCM huyu jamaa kila chama alichohamia alihama na ushindi pale Arusha.Hiyo ndio karama ya CDM wanaviongozi wenye mvuto kwa jamii.
 
Mingoi umalaaniwa na wazazi wako nakuambia, na akili yako haiko sawa. Usifikirie kwa kutumia maini, upe ubongo nafasi yake na ujue kipimo cha upumbavu ni kuwa na mpumbavu. Lema yuko sahihi kabisa, ukibaraka wako ndio unaokutesa. Kaa chini na ufikirie utatumwa mpaka lini?
 
Mara nyingi dalili za mvua ni mawingu alichoandika Lema kwa Mh JK ni ukweli ambao kama tukiendelea kufanya utani Tanzania ya leo itageuka kama Nigeria.Kipisi cha sigara,njiti iwakayo moto ikitupwa msituni ina uwezo wa kuunguza msitu wote,tunaona kama mchezo wameanza kwenye sensa haya ni kama manyunyu tusipochukua mwamvuli kujikinga hakika mvua itatunyeshea. Kiongozi wao ambae alikuwa akiwaambia wasikubali kuhesabiwa huyu akibaki basi tujue ipo siku watafanya kweli
 
Ujumbe mzuri kiukweli. Nimeipenda zaidi hii "Dini na kabila lake sio jambo muhimu hata kidogo katika uongozi, hivi ikitokea katika uchaguzi Dini moja tu na kabila moja ndio likahusika katika uchaguzi wakati wa mchakato wa kutafuta viongozi , je Serikali itaahairisha Uchaguzi kwa sababu watu wengine wa Dini na Kabila nyingine hawakuona umuhimu wa kushiriki Uchaguzi?"

Tanzania tunasumbuliwa na akili ndogo kutawala akili kubwa na ukiangalia kwa karibu utaona dola inashabikia kutugawa watanzania kwa staili ya udini, ukanda, mali na hata kwa sasa wameanza kutugawa ktk makundi ya wakulima na wafugaji...we angalia tu maneno yao na programme zinazotekelezwa utaona bila shaka kuwa tz ni taifa linalogawanyika kwa kauli za viongozi. Mtindo wa viongozi kusisitiza kuwa haya ni maeneo ya wakulima na haya ni maeneo ya wafugaji yatatugharimu huko tuendako... na tayari tunayaona sehemu mbalimbali katika nchi yetu...lakini waasisi wake ni watunga sera. Tulipokuwa ni taifa ya wakulima na wafanyakazi haikuwa na maana kuwa wafugaji wa kuku, bata, kondoo, mbuzi, bata mzinga, kasuku na ng'ombe hawakuwa na nafasi na sera ilifundisha wakulima na wafugaji na wakatumwa kusaidia watu vijijini kwao. Leo hii tumeshaanza kuunda hata vyama vya wafugaji pekee yao na tena tukiangalia ufugaji kama ni ng'ombe tu wakati wachina pale Mkuza wanafuga kuku na ni wafugaji na hata wenye mabwawa ya samaki nao ni wafugaji au wakulima wa samaki... Weney kutunga sera tuondoleeni ushabiki huu wa kutugawa maana kule tunakosema ni kwa wafugaji ukipita mbona mahindi na mabogo wanalima? Wale tunaosema ni wakulima ukipita mbona nao ng'ombe na kuku wanafuga? Sera ituondolee utabaka huu la sivyo tutavuna ya Ikwiriri na Mvomero na kwingineeko yanakojitokeza.
 
Lema ulishinda kwa siasa za udini,ubaguzi na matusi leo unajifanya una busara,labda uwe umepona kaugonjwa kako
 
Kawaambie viongozi wa dini kule sumbawanga waliowatenga waumini wao kanisani kwa kuipigia kampeni ccm ndio umwandikie rais barua.otherwise unahitaji tiba wewe sio tanzania
 
Hii barua inamfaa slaa ambaye amesaidiwa na waumini wa makanisa hapa nchini kukifikisha chama chake hapo kilipo.
 
Chama chenye udini kinajulikana, viongozi wa kidini ni wangapi CDM, na waislamu ni wangapi? Ukweli uko wazi kabisa, waislamu hawaikubali CDM na kina Slaa wanahitaji kura za waislamu lakini hawata zipata. Huu unafiki wa kina Lema na Slaa ni kujipendekeza kwa waislamu kufanikisha siasa zao. CCM oyee.
 
Sadam Hussein,Gadafi walikomaa mpaka mwisho na waliuhaminisha ulimwengu kuwa wapo strong kukabiliana na mapambana but we all know it ends...stay tune
 
Sadam Hussein,Gadafi walikomaa mpaka mwisho na waliuhaminisha ulimwengu kuwa wapo strong kukabiliana na mapambana but we all know it ends...stay tune
kabila moja litaiangusha ccm? Wewe kweli umelewa mbege.
 
NI NYEMA Mh Lema umeamua kusema kwa vile hata maandiko matakatifu yana sema ukiona jambo baya usipolikemea na likaja kuathiri, basi dhambi hiyo utaibeba wewe, ila kama ulisema na uliowaambia hawakuchukua tahadhari na ikatokea basi, dhambi hiyo itakuwa mikononi mwao.

wewe umemaliza ujumbe wako waachie dhambi ibaki kwao. Hakuna utawala unaodumu milele.
kuna siku tutakuwa na Taifa lenye kuwa na viongozi walio na hofu ya Mungu

:hat::hat::A S 465::israel:
 
Tanzania tunasumbuliwa na akili ndogo kutawala akili kubwa na ukiangalia kwa karibu utaona dola inashabikia kutugawa watanzania kwa staili ya udini, ukanda, mali na hata kwa sasa wameanza kutugawa ktk makundi ya wakulima na wafugaji...we angalia tu maneno yao na programme zinazotekelezwa utaona bila shaka kuwa tz ni taifa linalogawanyika kwa kauli za viongozi. Mtindo wa viongozi kusisitiza kuwa haya ni maeneo ya wakulima na haya ni maeneo ya wafugaji yatatugharimu huko tuendako... na tayari tunayaona sehemu mbalimbali katika nchi yetu...lakini waasisi wake ni watunga sera. Tulipokuwa ni taifa ya wakulima na wafanyakazi haikuwa na maana kuwa wafugaji wa kuku, bata, kondoo, mbuzi, bata mzinga, kasuku na ng'ombe hawakuwa na nafasi na sera ilifundisha wakulima na wafugaji na wakatumwa kusaidia watu vijijini kwao. Leo hii tumeshaanza kuunda hata vyama vya wafugaji pekee yao na tena tukiangalia ufugaji kama ni ng'ombe tu wakati wachina pale Mkuza wanafuga kuku na ni wafugaji na hata wenye mabwawa ya samaki nao ni wafugaji au wakulima wa samaki... Weney kutunga sera tuondoleeni ushabiki huu wa kutugawa maana kule tunakosema ni kwa wafugaji ukipita mbona mahindi na mabogo wanalima? Wale tunaosema ni wakulima ukipita mbona nao ng'ombe na kuku wanafuga? Sera ituondolee utabaka huu la sivyo tutavuna ya Ikwiriri na Mvomero na kwingineeko yanakojitokeza.

wewe ndio una akili ndogo mana analysis yako iko sawa kabisa na ufinyu wa fikra zako.ungekuwa na akili kubwa ungegombea hata uenyekiti wa kijiji.pili unashindwa kuelewa madhara yatokanayo na mapigano ya wakulima na wafugaji kwa kutumia eneo moja.mfano hapa morogoro wafugaji wamepigana na wakulima.umeandika maneno meeengi lakini hayana mana ht kidogo.
 
Sadam Hussein,Gadafi walikomaa mpaka mwisho na waliuhaminisha ulimwengu kuwa wapo strong kukabiliana na mapambana but we all know it ends...stay tune

hawa wazee waliuawa na wafadhili wenu ambao nape alisema wanavuruga nchi za wengine ili wachukue rasilimali wakati wenye nchi wanapigana.tunajua wameshaanza kuwapa na nyie pesa ili tupigane ila mungu amekuumbueni.
 
Siasa zake chafu si ndio zimeng'oa ubunge, huyu ndio anahitaji tiba,tena ya haraka sana.

Kwa kweli tangia 2010 siasa za ccm zimekuwa zikiigawa nchi ktk misingi ya kabila, dini na kanda wakidhani ndo njia pekee ya kuwabakisha madarakani bila kuangalia mwelekeo wa baadae wa taifa
 
Lema anaandika waraka kama mwananchi wa kawaida ama kuna kitu? Nitoeni tongotongo wadau
 
Hivi ni chama gani cha siasa hapa nchini ambacho kimejaa wachungaji na mapadre?ambacho wafuasi wake ni watoto wa wachungaji na mapadre?lema wakati unamnyooshea mwenzako kidole kimoja,vitatu vinakurudia,watanzania sio wajinga kama unavyofikiri wewe.
 
Back
Top Bottom