Mh Rais, Taifa linahitaji tiba - Godbless Lema

Siasa zake chafu si ndio zimeng'oa ubunge, huyu ndio anahitaji tiba,tena ya haraka sana.

SOMA HAPA BWANA MAJEBERE ili uweze Kumjua Lema vizuri



IKULU ILIINGILIA KESI YA UCHAGUZI. – GODBLESS LEMA.

“Ndugu Wananchi;


Napenda kutumia nafasi hii kutoa pongezi na shukrani nyingi kwa ndugu zetu wa Arusha kwa kuwapokea vizuri na kuwakarimu vyema wageni wetu hao. Nawaomba waendelee na moyo huo mpaka watakapoondoka wote. Naomba kuwepo kwa mkutano huu kuwakumbushe umuhimu wa mji wenu kuwa tulivu. Miaka miwili iliyopita isingekuwa rahisi kwa watu au shirika kubwa la kimataifa kama Benki hii kuamua kufanya mkutano wake Arusha. Isitoshe hata sisi wenyewe tusingeshawishika kuomba au kukubali maombi ya namna hiyo. Lakini sasa imewezekana. Naomba kila mmoja wetu aweke azimio moyoni mwake la kuhakikisha kuwa hali ile haijirudii tena. Nyota ya Geneva ya Afrika lazima iendelee kuangaza. Yaliyopita si ndwele tugange yajayo . ( J.K . KIKWETE.)

“Narudia tena , IKULU iliingilia kesi yangu ya Ubunge”.

Mh Rais nimekusikiliza kwa makini sana ila nakupa pole kwani bado unafikiri unaongea na Tanzania ya mwaka 1961 , umesema sasa Arusha ni shwari tofauti na miaka miwili iliyopita kwani sasa kuna amani na utulivu wa kutosha ndio maana hata mkutano wa AFDB umefanyika Arusha .

Mh Rais , najua IKULU iliingilia kesi yangu kama ilivyoonekana na ndio sababu hata Mkuu wa Mkoa wa Arusha wakati anaapisha Wakuu wa Wilaya alimpongeza Jaji kwa hukumu nzuri aliyowafurahisha wakati kesi hiyo iko mahakama ya Rufaa , lakini jambo moja la msingi ambalo huwezi kulitambua kwa sasa ni kuwa Haki na Ukweli haviwezi kushindwa na dhuluma, ubaya wala mamlaka , natambua wewe ni Rais na unayo mamalaka makubwa katika Taifa hili lakini vile vile nataka utambue kuwa huna mamlaka makubwa dhidi ya haki , utu na ukweli.

Mh Rais hakuna Amani Duniani inayozidi Haki na usawa ,utu na ukweli , haipo na wala haitakuwepo , ndio maana kila siku nasema ni "Afadhali Vita Inayotafuta Haki na usawa kuliko Amani inayopumbaza na kudhalilisha utu wa Mwanadamu" umefurahia sana mkutano uliokupa fursa ya kutoa maneno ya kebehi na kudhihirisha ila chafu iliyofanywa na Serikali yako na kujaribu kuhadaa Umma kama ilivyo kawaida ya Serikali yako na Chama chako. Hata hivyo wakati huu kuna mambo ya msingi yakushughulikia zaidi ya kebehi na hadaa, Uchumi wa Nchi umeyumba, huduma za msingi za jamii zimepuuzwa, Mpasuko katika suala la Muungano na vururugu zinazoendelea Zanzibar, mfumuko wa bei hizi ni sababu chache ambazo haziwezi kuruhusu wakati huu kuwa wakati wa kebehi na mizaha isipokuwa kazi .

Mh Rais, Mama Theresa, Nelson Mandela, Martin Luther Jr na Malcom X hawakuwa Wabunge kupigania haki za Nchi yao na watu wao. Sihitaji Ubunge kupigania ukweli, haki na utu, nahitaji dhamira safi, nia njema na huu utakuwa wajibu wangu mpaka nakwenda kaburini, nitakapomaliza mbio hizi najua nitapata fursa ya kutazama nyuma yangu nione nini nilifanya. Ukweli nisingependa kuona vituo vya mafuta, magorofa, magari na viwanja vingi kila kona ya Nchi bali Haki, Usawa na utu vikiwa kama nguzo ya imani ya watawala wetu watakaokuwepo. Pengine sitaishi miaka mingi sana kama utachukizwa sana na waraka wangu huu kwani Polisi, Usalama wa Taifa na Jeshi la Wananchi wanakutii wewe, hata hivyo siogopi kufa kwani nisipokufa kesho, nitakufa siku moja ambayo siijui, napenda kuishi maisha marefu nimwone mke wa mtoto wangu kama itawezekana, lakini kuliko iwezekane kwa kuishi kwa hofu ni bora ishindakane kwa kuthamini haki. Kwa hiyo kama utakuwa umekasirika sana, unaweza kufanya jambo lolote baya kwa kutumia mamlaka yako, niko tiyari sio kesho wala leo isipokuwa sasa hivi, najua IKULU imewazulumu watu wa Arusha Mbunge wao.

Mh Rais ninajua wazi njama zote na hasira hizi zinaweza kuwa zimetokana hasa na mkutano tuliokaa Osterbay Dar mimi na wewe kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 hata hivyo sikupuuza maongezi yetu isipokuwa nilichagua kufuata dhamira yangu na wito wangu wa utumishi wa kweli katika Jimbo langu na Nchi yangu.

Mh Rais nimekuelewa na Wananchi wamekuelewa kila mahali , wewe ni Rais unayo mamlaka makubwa na mimi ni mwananchi mamlaka yangu makubwa ni kwa mke wangu tu , sina Polisi wala Usalama wa Taifa lakini nitawaomba wanyonge wafunge na kusali tuone kama mamlaka yako inaweza kushindana na haki na ukweli .

Mh Rais “Mtu anaweza kuzini kwa siri lakini hawezi kuugua ukimwi kwa siri” Serikali na Chama cha Mapinduzi kimepuuza watu na haki zao kwa muda mrefu , lakini wakati umefika ambapo hawatapuuzwa tena hata hivyo kwa kauli yako hii naamnini haiwezi kuwafundisha kazi majaji wa mahakama ya rufaa .

“ONLY TIME WILL TELL”.


GODBLESS .J. LEMA.
 
JELA NI MAHALI PA KUISHI KAMA SABABU YA KWENDA HUKO NI VITA DHIDI YA UONEVU, UKANDAMIZAJI WA HAKI NA UTU WA BINADAMU.



Wapendwa wapiga kura wangu na Watanzania wenzangu.
Sina wakati mgumu kuchukua maamuzi haya yanayotokea leo. Upendo huu nilio nao kwa watu wa Arusha na nchi yangu ni sababu ya msingi ya maamuzi haya. Nimetishwa mara nyingi, rafiki zangu wametishwa, jamii ya watu duni imeendelea kuishi kwa mashaka na matisho kwa muda mrefu.
Katika mazingira haya, nikawaza sana kuwa anatakiwa kutokea mtu mmoja jasiri atakayeweza kuona thamani ya watu wengine. Huyo mtu anaweza kuwa wewe lakini kwa wakati huu siwezi kumsubiri tena na nimechagua kuwa mimi nikiamini kuwa utanikuta nikiendelea na safari ya ukombozi.
Tupo wengi sana tunaotaka mabadiliko, haki na ukweli. Hata hivyo hofu, woga na mashaka yamepoteza thamani yetu yote ya maana ya kuishi.
Waliofungwa kwa kuonewa na kuteswa, waliokosa chakula na kulala nje, waliokwenda hospitali na kukosa madawa, waliokosa ajira na kipato mpaka kujikuta wametoroka familia zao, waliopoteza matumaini ya maisha, waliopora utajiri wa nchi yetu kwa manufaa yao binafsi, walionunua haki na sheria dhidi ya wajane na wanyonge na kuwapora vipato vyao vidogo na mashamba yao, USIULIZE SABABU NINI!
Nimetafakari sana na nikatambua kuwa sababu ni mimi pale nilipokuwa kimya wakati wajane na wanyonge wanaonewa.
NIliposikia wengine wanaandamana kupinga uovu, uonevu, wizi, ufisadi na ukandamizaji wa haki nikasema ni hao na wala sio mimi, kumbe nilipaswa kuwa mbele katika harakati hizi.
Nilipoona wenzangu hawawezi kupata matibabu nikasema mimi sio mgonjwa, nilipopata taarifa za rafiki zangu kufungwa kwa makosa yasiyo yao, nilipoona watoto wa mitaani wanaomba chakula, nilipoona wazee wamepoteza matumaini ya kuishi katika uzee wao, nilipoona vijana hawana ajira, nilipoona mabinti wasichana wadogo wameamua kufanya biashara ya ukahaba, NIKATAFAKARI,TENA NIKATAFAKARI, dhahabu zetu, almasi yetu, Milima na mabonde yetu, Tanzaninte yetu, samaki wetu, Uranium yetu, makaa ya mawe yetu, utalii wetu, ardhi na kilimo chetu na zaidi utu na mahusiano yetu.

Na sasa siwezi kukaa kimya tena. NI afadhali vita inayotafuta haki na usawa kuliko amani inayopumbaza na kudhalilisha utu wa mwanadamu. Na katika msingi huu hofu na mashaka vimekosa thamani kwangu, sitamwogopa mtu yoyote, mwenye silaha yoyote, mwenye cheo chochote na wala sitaogopa jela yoyote katika kupigania haki, utu wa kweli katika jamii yangu.

Wanafikiri wataendelea kutuogopesha kwa sababu wana jela na silaha, wanafikiri tutaendelea kuabudu uoga, wanafikiri wataendela kutunyanyasabila sababu ya msingi LAKINI SISI TUNAJUA TUTASHINDA KWA SABABU HAKI TUNAYOIPIGANIA NI MAKUSUDI YA MWENYEZI MUNGU.
Leo nitakwenda jela kwa hiari yangu binafsi kwa siku kadhaa na si kwa NIA YA KUJITAFUTIA UTUKUFU WANGU bali ,” JELA NI MAHALI PA KUISHI KAMA SABABU YA KWENDA HUKO NI VITA DHIDI YA UONEVU, UKANDAMIZAJI WA HAKI NA UTU WA BINADAMU.Kila mara nilipotishiwa nikagundua wanaonitishia, wananitishia kwa jela na mauti. Na mimi nikagundua na nikatambua ni afadhali kuishi miaka hamsini jela huku sababu ikiwa ni kupinga uonevu na ukandamizaji kuliko maisha ya woga na anasa yasiyo na kusudi katika kutetea utu na heshima ya mwanadamu mwenzangu.
Wale mlionitishia kunipeleka jela sasa nimetangulia kwa hiari yangu na wale mliobaki msiogope jela endeleeni kupigania ukombozi utakaoleta usawa katika nchi yenu.
Watakaotubeza na kututukana wasameheni kwani wanahitaji ukombozi wa fikra, watakaotupongeza na kutuonea huruma wafundisheni ujasiri na waambieni mapambano bado yanaendelea tunahitaji umoja wao. Nitarudi mapema. MSIOGOPE, MSIOGOPE, MSIOGOPE , MUNGU YUPO UPANDE WETU.

Mhe Godbless Lema (MB) – Arusha Mjini 31 Oktoba 2011.
 
Hivi hii nchi kuna watu wangapi walio fikishwa mahakamani kwa kesi ya ubaguzi wa jinsia na dini? Mi najua ni mmoja tu. Leo anakuja hapa kujifanya ni malaika halafu wapuuzi fulani wanamsifia.
 
Daah lema ni jembe! Nashukuru kwa ushauri mzuri kwa jk ili amfunde Mkama.
 
Daaaah! Una kichwa kigumu sana!
Hivi hii nchi kuna watu wangapi walio fikishwa mahakamani kwa kesi ya ubaguzi wa jinsia na dini? Mi najua ni mmoja tu. Leo anakuja hapa kujifanya ni malaika halafu wapuuzi fulani wanamsifia.
 
Unajua unacho kiongea?
Alicho kiongea kamanda na wewe unachosema ni vitu tofauti jaribu kupunguza kupanic

Siasa zake chafu si ndio zimeng'oa ubunge, huyu ndio anahitaji tiba,tena ya haraka sana.
 
Hivi ni chama gani cha siasa hapa nchini ambacho kimejaa wachungaji na mapadre?ambacho wafuasi wake ni watoto wa wachungaji na mapadre?lema wakati unamnyooshea mwenzako kidole kimoja,vitatu vinakurudia,watanzania sio wajinga kama unavyofikiri wewe.

umejipambanua kwa jina lako ulivyolishwa na ccm dhidi ya Cdm.
 
mh rais , taifa linahitaji tiba . godbless lema

mh rais , nakusalimu .
mh rais na huu ni ushauri wangu kwako kama mkuu wa nchi na mtazamo wangu juu ya matukio yanayotokana na changamoto katika sensa ya taifa hivyo nakunifanya nikuandikie waraka huu.

mh rais , kama taifa hili kwa miezi michache mbele inayokuja siasa za udini , ukabila na ukanda utaendelea kushabikiwa katika kiwango hiki cha sasa , ukweli ni kwamba siku chache zinazokuja taifa hili litaanguka na halitasimama tena, propaganda zilizofanyika huko nyuma dhidi ya vyama vya upinzani mbali mbali zilifikiriwa kuwa lengo lake lilikuwa ni kuviangamiza vyama hivyo tu na huku watawala wakibaki salama, lakini leo tunaanza kuona lugha za udini zikitawala katika taifa letu kila siku na ule mpango wa kuangamiza vyama hivyo umekwenda mbali zaidi na sasa unakaribia kuangamiza taifa.

mh rais nchi hii haiko salama hata kidogo na pengine wahusika wanaopaswa kulinda usalama wa nchi wanakupa ripoti za hofu na woga na hivyo unashindwa kupata taarifa kamili ya ukweli wa mambo yanavyoendelea katika taifa letu, ukitazama suala la sensa na changamoto zake kwa sasa utagundua kwamba sio faida hata kidogo kulazimisha jambo hili kwa kutumia nguvu kwani sio sahihi hata kidogo kujua tu idadi ya watu bila kuzingatia hofu ya watu hao na mashaka ambayo yamejengeka katika imani.

mh rais , siasa chafu ambazo zimekuwa zikitafuta madaraka bila kuangalia siku njema za baadae za nchi ndio chanzo cha kinachotokea sasa, tulipokuwa igunga chadema ilifanyiwa propaganda za udini sana na kwa bahati mbaya waliofanya hivyo walishinda uchaguzi na huku watu wale waliofanya hivyo waliamini na kufikiri siasa hizo za kibaguzi zitaishia igunga tu na bila kutambua dini ni imani na lazima kutaendelea kuwepo na mpasuko mkubwa hata baada ya uchaguzi.

mh rais , uhuru wa kweli sio mtu kufanya kila anachotaka bali kile anachopaswa tena katika haki na kweli " kama lengo la watawala kubaki madarakani au kuongoza litafanywa kwa nguvu na namna yoyote hile hata kwa kuwagawa watu kwa dini zao na kabila , basi siku chache zinazokuja taifa letu halitaweza kutawalika tena na mamlaka hayo yanayotafutwa hayataweza kuwa na faida kwa kizazi hiki na kizazi kinacho kuja na ukweli ni kwamba kwani kila aina ya ubaguzi wa aina yeyote unaofanyika ama kwa siri au hadharani hautaacha jamii yetu kuwa salama.

mh rais, chama tawala siku zote wajibu wake katika kujibu hoja za wapinzani ipasavyo ni kutekeleza ahadi zake ambazo walizitoa wakati wa uchaguzi na huu ni wajibu mkuu katika kutawala kwa chama tawala , lakini chama kilichoko madarakani kinapoanza kuwagawa watu kwa dini na kabila ili mradi kifanikishe malengo ya kutawala basi ni lazima tutambue kuwa viongozi wa chama hicho wamekusudia kabisa kuipeleka nchi yetu katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.

mh rais , siku hizi katika forum mbali mbali zinazojadili mambo ya siasa katika mitandao ya kompyuta hapa tanzania , kumekuwepo na maoni mbali mbali na mitazamo haswa wakati wowote ule unapofanya uteuzi au kuchagua mtendaji katika serikali , mara nyingi , ghafla utaanza kuona watu wananza kuuliza kabila au dini ya mtu aliyeteuliwa au kupendekezwa, hii ni hatari kubwa kuwa na taifa ambalo sifa ya mtu ya kwanza kwa wachambuzi na wadadisi inajadiliwa kwa dini au kabila ya mtu fulani , kwani hatuwezi kuongozwa kwa mlinganisho wa kabila au dini ili kupata utawala bora . Tabia hii wakati mwingine inapelekea kutafuta viongozi mbali mbali kutoka kila pembe ya nchi ili kupata mlinganisho wa ukanda na kimkoa na hivyo kusababisha kuishia kupata viongozi pengine viongozi wasiokuwa na uwezo kwa sababu ya kutafuta mlinganisho katika kupanga safu ya uongozi na utawala . Na kwa kweli huu nao ni ubaguzi uliojificha unaoendelea katika taifa letu.

utawala thabiti mahali popote , utazingatia , uwezo , sifa , maarifa ,uadilifu na hekima ili mtu kuchaguliwa kuongoza . Dini na kabila lake sio jambo muhimu hata kidogo katika uongozi, hivi ikitokea katika uchaguzi dini moja tu na kabila moja ndio likahusika katika uchaguzi wakati wa mchakato wa kutafuta viongozi , je serikali itaahairisha uchaguzi kwa sababu watu wengine wa dini na kabila nyingine hawakuona umuhimu wa kushiriki uchaguzi ? Ni swali ambalo linaweza kuonekana halina msingi lakini kwa wanaona mbali watajua ni nini namaanisha ? Hata hivyo tunakoelekea sasa tusipokuwa makini , tutanza kupokezana madaraka na utawala kwa kuangilia udini na sio uwezo na uadilifu na tukifika hapo taifa hili halitasimama tena.

mh rais ni wajibu wako sasa kusaidia taifa hili kwa mamlaka uliyonayo ni imani yangu hata wewe umekwishaona hili na ni matumaini yangu kuwa unalifanyia kazi . Mfano wa wazi ni pale katibu mkuu wa ccm bwana mkama , alipotaka kuleta siasa za kibaguzi katika msiba wa marehemu bob makani pale karimjee wakati akitoa salamu za rambi rambi ambapo wewe mwenyewe ulikuwepo kama kiongozi mkuu wa taifa na ulishuhudia upotoshaji wake huo ambao ulionekana kama lengo ilikuwa kuidhoofisha chadema huku hakisahau kuwa dhambi ya ubaguzi aina mipaka.

mh rais , martin niemoller , alisema maneno yafuatayo yalipomkuta " when hitler attacked the jews i was not a jew, therefore i was not concerned. And when hitler attacked the catholics, i was not a catholic, and therefore, i was not concerned. And when hitler attacked the unions and the industrialists, i was not a member of the unions and i was not concerned. Then hitler attacked me and the protestant church -- and there was nobody left to be concerned"

mh rais , tatizo ni kubwa na ni vyema likashughulikiwa kwa nguvu zote sasa na kwa hekima , hata hivyo nafikiri waraka huu hautakukwaza kwani ni ukweli wangu juu ya hali halisi inayoendelea kujitokeza katika nchi yetu na mimi nikasema nisikae kimya ni bora niseme , taifa linakwenda mahali pabaya kama dhambi ya ubaguzi isipodhibitiwa.

nakutakia kazi njema.

" only time will tell "
godbless jonathan lema
26/8/2012

Tanzania inaangamia, watawala wameshindwa kutimiza wajibu wao, wananchi wamesongwa na matukio ya uhalifu kila uchao na katika kila kona ya nchi.
 
Back
Top Bottom