Mh; Rais Magufuli Ikikupendeza Mpe Nafasi Mh James Mbatia Awe Katibu Mkuu Wizara ya Elimu.

Mpinzire

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
7,225
12,947
Mh; Rais John Pombe Joseph Magufuli pole sana kwa kazi ngumu unayokabiliana nayo lakini ni ukweli usipingika tulikuchagua ili utufanyie kazi wananchi wako na binafsi nalidhishwa haswa na utendaji wako wa kazi na hili linanifanya kamwe nisijutie uamuzi wangu wa kuweka tick kwenye box la kulia kwenye ile karatasi la kupigia kura ile 2015.

Mh Rais wangu Magufuli umejitahidi sana kutatua changamoto ambazo kama taifa tukikumbananazo na ili tusonge mbele, Mh Rais ile staili yako ya kukutana wadau wa sekta husika kama ulivyofanya kwenye sekta ya madini jana pale JNICC na kuwapa fursa direct wadau kwa kila eneo lake azungumze vitu gani vinawakwaza huko kwenye biashara zao, ile ni staili mzuri sana na usiiache maana inaibua mengi ambayo huyajui, pia ulifanya hivi ulipokutana na wafanya biashara pia, wadau wa sekta ya utalii nao wanaomba sana Mh Rais ukutane nao nao wapate nafasi kama ile ya jana ya kusema yao direct. Niishie Mh Rais kwa jambo hili naende kwenye hoja yangu.

Mh Rais kama Kichwa cha Habari yangu kilivyojieleza hapo juu, Mh Rais ikikupendeza naomba umpe nafasi Mh James Mbatia (MB Vunjo) ata awe katibu mkuu wizara ya Elimu, Mh Mbatia anauchungu mkubwa sana Elimu yetu nahisi anakitu tofauti katika nafsi yake ambacho angependa kifanyiwe kazi kuokoa Elimu yetu. Mh; Rais wengi wetu humu jukwaani tunaamini Mh; Prof; Joyce Ndalichako ni zao la mawazo ya wana Jamii Forums basi nami kama mwanachama wa jukwaa hili pendwa natumia fursa hii kukuomba umfikilie Mh; james Mbatia.

Mh; Rais nakumbuka jinsi ukivypenda kufatilia kipindi cha 360 pale Clouds Tv na sikuzote ukizopiga simu kwa Hudson Kamoga na ni imani yangu kuwa kweli ulimuona Hudson Kamoga ni kijana mwenye mawazo mbadala, na ni kweli kijana yule akiwa kwenye kipindi alikuwa anatoa mawazo chanya kwa viongozi wa mikoa na nakumbuka kuna wazo siku moja aliwauliza ata watangazaji wenzake pale kuwa " Hivi hawa wakuu wa Mikoa wanashindwa vipi ata kila mmoja angekaa na wataalamu wake wakatenga eneo ata moja tu na kufanya sehemu ya utalii wakaijenga vizuri ili kuvutia watu wakawa wanapata mapato?" Mh Rais kwa jinsi ukivyopenda kufatilia kile kipindi nami naamini yule Kijana Hudson kamoga ulimjulia pale na ukawa unayaelewa mawazo yake na ukampa nafasi.

Mh; Rais na ndiyo maana naleta ombi kwako umuangalie Mh Mbatia ana kitu nadhani anaweza kutuvusha kama Taifa kwenye sekta ya Elimu japo sina Mashakha na Prof Ndalichako ila naamini wakishirikiana wanafanya kitu bora japo ni mwanasiasa lakini naamini pia ni mtendaji mzuri lakini kwa nafasi yeyote utayopenda kumpa kama Waziri, Naibu au katibu mkuu lakini nafikiri zaidi awe mfanya maamuzi na si mretewa maamuzi. Vyovyote itakavyo kupendeza Mh Rais kama utaona sasa au baada ya uchaguzi 2020 ili miaka mitano ya mwisho ufanye kazi nayeye sawa tu mawazo yako nitayaheshim.
1548225398218.png

Ni hayo tu Mh Rais.
Wako katika Elimu Bora
JF Member.
 
Hata Mimi naunga mkono yeyote atakayeonekana kufaa mwenye nidhamu na uzalendo apewe nafasi kwenye serikali bila kujali chama chake.hii nchi tutaijenga sisi wenyewe tushikamane mamlaka zipo wakati mkuu wa kufanya mabadiliko makubwa Sana na hayatachelewa.
 
"mimi huwa sipangiwi wara sishauriwi, mimi ni mgumu kweli kweli, mimi ni JIWE.
 
"mimi huwa sipangiwi wara sishauriwi, mimi ni mgumu kweli kweli, mimi ni JIWE.
Sijampangia na wala hajawai kusema hashauriwi wala hataki ushauri wa mtu! Jana pale JNICC alikuwa anapokea pia ushauri na ameupokea kama kawaida na amewapa ahadi kuwa mambo atayafanyia kazi alimradi taifa lisonge mbele ila pia

katiba ya JMT 1977 haimlamishi Mh Rais kupokea ushauri wa mtu yeyote isipokuwa baraza la mawaziri, Bunge na vyombo vingine ambavyo vimeorodheshwa kwenye sheria mbalimbali za nchi.
 
Back
Top Bottom