Mh Rais JK, unalijua hili?

nilivyosoma katika vitabu vya nyuma, nilivyosikia matangazo katika redio na runinga nimegundua yafuatayo katika safu ya viongozi wa nchi yetu.

1. Mwalimu nyerere.
kwa mawazo yangu huyu mtu alikuwa sana anapenda utaifa kwa sababu aliikomboa nchi kutoka kwa wakoloni, alichukua mali zilizokuwa zinashikiliwa na wakoloni na kuwa chini ya serekali yake na ndivyo hivyo aliingia kwenye siasa ya ujamaa akiamini ushilikiano wa pamoja wa serikali, wananchi na mali zao. kwa hiyo alikuwa anapenda maendeleo yake na taifa lake.

2. Raisi mstaafu Hussein Mwinyi.
huyu alikuwa pia anapenda maendeleo kwa wananchi wake kwa sababu aliruhusu uingizaji wa bithaa za nchi za nje kwa ajiri ya kukidhi haja za watu wake ijapokuwa ilileta matatizo lakini alikuwa na nia nzuri na watu wake.(kila kitu ruksa)

3. Raisi mstaafu benjamini mkapa
katika kipindi chake alikuta uchumi wa nchi ukiwa mbaya na kuanza kuupandisha. kiukweli alifanikiwa na mpaka anaondoka madarakani aliacha uchumi ukiwa 4% tofauti na sasa. alijenga madarasa akiongozwa na mmem na mesi, alijenga daraja, alijenga uwanja na mwisho alirudisha heshima ya wafanyakazi ambayo ilikuwa imeshuka kwa sababu ya kutokuwa na pesa za kujikimu wakati wafanyabiashara wakiringa mtaani.

4. Raisi Jakaya Mlisho Kikwete.
mpaka sasa mimi sijui raisi wangu anafikilia nini kuusu hii nchi ikiwa pamoja na watu wake na rasilimali zake. ndugu zangu pamoja na mambo yate yaliojitokeza katika kipindi chake mpaka sasa. JE RAISI WETU ANAFIKILIA NINI KUUSU HII NCHI HAPO BAADAE?. NISAIDIENI MAJIBU.

JK atahakikisha Mama Salma ni bilionea,Yeye mwenyewe bilionea,Riz1 Billionea na Ukoo wake wote.Uzalendo haupo nchi hii ni kula nchi kama wenda wazimu!!!
 
Tatizo, hapa jamvini baadhi ya wadau wanataka hoja za CDM tu....pokeeni na mawazo ya wengine.

Binafsi, sioni tatizo ktk hoja ya Nyami, kuna kushauri lazima ushauri upokelewe?
 
Back
Top Bottom