Mh. Msolla kuwekwa kiti moto na wapiga kura wake

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Friday, May 25, 2012

Mbunge wa jimbo la Kilolo Profesa Peter Msolla


Na Francis Godwin Blog,Iringa



BAADA ya mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa (CHADEMA) kuweka kitimoto na wapiga kura wake sasa ni zamu ya mbunge wa jimbo la Kilolo Profesa Peter Msolla


Prof. Msolla ambaye amepata kuwa waziri wa mawasiliano Sayansi na Teknolojia atawekwa kitimoto kesho katika mdahalo ulioandaliwa na azaki za kiraia mkoani Iringa Mdahalo utakaohusisha mbunge huyo na wapiga kura wake .


Mdahalo huo kati ya mbunge Profesa Msolla na wapiga kura wake umepangwa kufanyika kuanzia majira ya asubuhi katika eneo la Ruaha Mbuyuni Sokoni katika tarafa ya Mahenge wilayani Kilolo na baada ya mbunge Prof.Msolla itafuata zamu ya mbunge wa jimbo la Ismani ambaye ni waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu (sera na uratibu wa bunge) Wiliam Lukuvi huku mbunge wa kalenga Dkt Wiliam Mgimwa ambaye ni waziri wa fedha na uchumi atahitimisha midahalo hiyo.


Mratibu wa midahalo hiyo Raphael Mtitu alisema kuwa midahalo hiyo ambayo ilianza kwa mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa imepangwa kufanyika majimbo manne ya mkoa wa Iringa na ambayo ni Iringa mjini ,Kilolo ,Kalenga na Ismani .


Hata hivyo aliwataka wabunge wote kushiriki katika midahalo hiyo ambayo imelenga kuwakutanisha wabunge na wapiga kura wao ili mbunge kuweza kueleza kile alichokifanya na wananchi kuhoji ama kupatiwa ufafanuzi juu ya ahadi zilizotolewa wakati wa kampeni ama mambo mbali mbali ya kimaendeleo ambayo yanafanyika ama hayafanyiki katika jimbo husika.


Mtitu alisema kuwa mtandao huo umeandaliwa na mashirika yasiyo ya Kiserikali katika Mkoa wa Iringa ( Iringa Civil Society Organization [ICISO- UMBRELLA]) kwa kushirikiana na mitandao ya AZAKI ya Halmashauri ya manispaa ya Iringa (Iringa Municipal Civil Society Organization – IMUCISO), Iringa vijijini (Iringa Rural Non-Governmental Organization – IRUNGO) na Kilolo (Kilolo District Non-Governmental Organzations Umbrella – KIDINGOU),


Pia alisema kuwa midahalo hiyo imelenga kuwaongezea uelewa wananchi ili waweze kushiriki kikamilifu katika masuala ya kijamii na kiuchumi yanayohusu ili waweze kumiliki michakato ya kuleta maendeleo yao badala ya kutegemea serikali na wahisani pekee.


Mradi huo utatekelezwa kwa njia ya makongamano, midahalo na mikutano ambapo itaandaliwa katika majimbo yao ya uchaguzi katika majimbo ya Kalenga, Isimani, Iringa mjini na Kilolo na Kila jimbo litafanyika midahalo isiyopungua minne.


Mtitu alisema kuwa kwa kipindi hiki cha mwezi Mei shughuli itakayofanyika ni mdahalo wa kuimarisha uhusiano kati ya wabunge, wananchi na AZAKI katika majimbo yote manne ya wilaya ya Iringa na Kilolo. Kwa jimbo la Iringa utafanyiaka Alhamisi tarehe 10/5/2012 katika ukumbi wa chuo cha maendeleo ya wananchi – Ruaha (Ipogolo).


Hata hivyo aliwataka wabunge wote kushiriki katika midahalo hiyo inayowapa fursa wapiga kura kuongea na mwakilishi wao Mwenyekiti wa Halmashauri moja kwa moja ili waweze kutoa dukuduku zao na kuuliza maswali na kujibiwa papo hapo. Wananchi wapate kujua shughuli alizozifanya/atakazofanya sehemu mbalimbali ndani ya jimbo/wilaya pamoja na utekelezaji wa ilania ya chama chake, ahadi za Rais pamoja na viongozi wengine wa kitaifa.


Mtitu alisema midahalo hiyo haifungamani na itikadi ya chama chochote cha kisiasa na kuwa hata wananchi wanaofika katika midahalo hiyo hawapaswi kuja na bendera wala sare ya chama chochote cha kisiasa.



 
Kazi ipo Wananchi sasa hivi wana Mwamko sio kama Miaka ya Nyuma piga kura ni CCM tu; Sasa hivi wanaitwa Wabunge wowote na kuwekwa kiti moto

Safi Sana Demokrasia Hiyo
 
Mbona wakati wa kampeini wanakimbia hiyo midahalo? wananchi inabidi tuweke misimamo, wakimbia midahalo wote wakati wa kampeini NO KURA zetu.
 
Mjitahid jutuletea updates hapo kesho za mhe. Huyu aliyefanya mkutano wa kuwadanganya watu juu ya mapanga ya nduli pale kihesa mgagao na kujenga chuki kati ya redio ebony na jamii, wapendwa wanakilolo wenzangu mpigeni maswali ya maana huyo jamaa.
 
Back
Top Bottom