Mh. Mnyika kwa hili umepotoka!...

Jadili hoja wewe, unazungumzia mambo ya vyama hapa. Shule gani umesoma wewe? Wewe kwa akili zako inamaana hujamwelewa jamaa anazungumzia nini? Mpinge basi kwa hoja na sisi wataalam wa mambo yasiyo ya pension tuweze kupima uzito wa hoja na tufaidike badala ya kuleta ushabiki wa kipumbavu wa kisiasa hapa.

Kama Ungekuwa Mkali kwa Wabunge wa CCM wanaozima UMEME kwa Wananchi kama ULIVYO kwa JOHN MNYIKA

Kweli ningejua WANANCHI wanataka nchi yao; Lakini SIJAWAHI KUONA HOJA YOYOTE ya kumlaumu OLE SENDEKO na

TIMU YAKE HUMU... WOTE WAMENYWEA... NI KULAUMU anayeonyesha anafanya kazi akiwa BUNGENI kuonyesha

HAFAI... ni kweli ...............
HAANGALIWI MTU USONI...
 
Jamani naombeni nitangulize samahani kwa kutoiona hii topic mapema, nina dukuduku na sina uhakika kama limeshajadiliwa humu.

Hivi hizi hela zinazochukuliwa leo na hii mifuko ya hifadhi tutarudishiwa zikiwa hivi hivi au kuna mahesabu ya "Time value of money!".

Kwa mfano leo 2012 nina miaka 30 nimekatwa Tshs 300,000 ambazo zinaweza kununua mifuko 20 ya cement leo, nikaacha kazi. Nitakapotimiza miaka 55 (miaka 25 ijayo) nitarudishiwa sh ngapi?

i. Je ni Sh 300,000? Ambayo kwa kipindi hicho itakuwa inanunua mifuko 6 au 8 ya cement!

ii. Au nitapewa kiasi kinachotosha kununua mifuko 30 kama fedha ya awali?

Kama jibu ni i. yaani sh 300,000 ni bora nizichukue leo angalau zikiwa na thamani hii hii.
 
Kaka mi sifanyi kwenye mifuko na nina very rare skills, na usijaribu nikakujua maana unaweza pita kwenye maeneo yangu, nita ku suprise! nakutania tu. Hata hivyo sidhani kama wanaweza kupunguza kwa sababu hizo, i dont think so. Halafu unajua ukiwa umesoma vizuri wala huogopi kupunguzwa kazi, na wasomi huwa hawapunguzwi kazini na ukisema watu wajitolee kupunguzwa utawaona watu smart wanajitokeza wanavuta yale ma pesa ya bure huku wakijua watapata kazi soon lkini hawchukui pensheni zao! jaribu siku moja utaona, hiyo ni international experience. Bado haimaanishi kwamba kujitoa kwenye mifuko ni kitu kizuri hata kidogo, tuache hii proppaganda mbaya sana.

Kuna tetesi kuwa mifuko ya jamii itapunguza wafanyakazi kwa ajili ya kubana matumizi. Sitashangaa nikifahamu kuwa wewe au mwenzi wako ni miongoni mwa wahanga watarajiwa.
 
Jadili hoja wewe, unazungumzia mambo ya vyama hapa. Shule gani umesoma wewe? Wewe kwa akili zako inamaana hujamwelewa jamaa anazungumzia nini? Mpinge basi kwa hoja na sisi wataalam wa mambo yasiyo ya pension tuweze kupima uzito wa hoja na tufaidike badala ya kuleta ushabiki wa kipumbavu wa kisiasa hapa.

Ndio Maana zinaitwa HOJA... Ni jinsi ya MTU anavyosoma na kuielewa akilini Mwake...na kuijibu...

Haina sababu ya kujua shule niliyokwenda... lakini vumbi la KARIAKOO halinipati hata kidogo...

Ni kwasababu ya MAFANIKIO YA AKILI YANGU KAKA...
 
Mimi kama mwanachama wa PPF najua kwamba fao la kujitoa lipo kisheria; rejea hapa PPF Act (Amended), 2002 kifungu cha 44. Hiki kifungu kimeboreshwa tu kutoka kifungu hicho hicho cha sheria mama ya 1978. Tusome wenyewe:

“Withdraw benefits”

(1) Where a member ceases to be employed in circumstances in which he is not eligible for any pension, gratuity or any other benefit under the provisions of this Act, he shall be refunded the amount of his own contributions and that of his employer to the Fund.

(2) Where a member has been employed for a period of not less than five years and the cessation of such employment is not due to dismissal for misconduct the amount of his own contribution and that of his employer together with a simple interest at that rate to be determined by the Board of Trustees shall be paid to him.


Kwa sheria ya SSRA, 2008, sijaona hiki kifungu kubadilishwa. Naomba mwenye hii sheria ya Social Security Laws (Amendment), 2012 atuwekee hapa. Najua bado ni siri, tukiipata itapanua wigo wetu wa mjadala maana mpaka sasa tunazungumza tu kwa juu juu.
 
Nashukuru sana Sober na wachangiaji wengine kwa michango yenu. Nitatafuta wasaa wa kusoma yote kwa ajili ya kupata maoni. Kwasasa tunaendelea na mkutano mpaka saa 11 jioni kwa ajili ya kupata maoni ya moja kwa moja katika masuala ambayo nimeomba yafanyiwe uchambuzi, mnaweza kurejea kupitia:JOHN MNYIKA: MKUTANO WA MTANDAONI KUHUSU MUSWADA WA SHERIA YA MAREKEBISHO YA SHERIA YA HIFADHI ZA JAMII KWA HATI YA DHARURA KUREJESHA FAO LA KUJITOA

Nimepitia kwa haraka haraka hoja za wanaopinga nisiwasilishe muswada wa marekebisho ya sheria za hifadhi ya jamii kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kukinzana na dhana ya malengo ya hifadhi ya jamii ya kutoa pensheni uzeeni, pia hoja za kupinga muswada usipelekwe kwa hati ya dharura bila kwa kuwa muswada husika wa kuwa haujatokana na mawazo ya watalaamu. Ni vizuri tu Sober na wengine mkarejea mchango wangu bungeni tarehe 13 April 2012 siku marekebisho husika yalipopitishwa ambapo nilitaka marekebisho ya ziada ambayo serikali haikuyaleta kwenye muswada wala marekebisho, aidha pitieni taarifa yangu kwa umma ya tarehe 3 Agosti 2012 ambayo mnaweza kuirejea kupitia: JOHN MNYIKA: Muswada binafsi kwa hati ya dharura: Marekebisho ya Sheria za Hifadhi ya Jamii kuhusu namna kinachoitwa 'marekebisho yaliyositisha fao la kujitoa' yalivyofanyika. Aidha, katika taarifa hizo nimeweka bayana kuwa "kufutwa kwa mafao ya kujitoa msingi wake haupo kwenye marekebisho ya sheria yaliyofanyika tarehe 13 Aprili 2012 pekee bali ni udhaifu katika mfumo mzima wa kisera na kisheria wa hifadhi ya jamii nchini hali ambayo inahitaji wadau kutaka mabadiliko makubwa". Nashukuru katika michango yenu nanyi mmeeleza baadhi ya marekebisho yanayopaswa kufanyika.

Nitarejea kutoa maoni yangu kuhusu hoja ambazo tumetofautiana kimtizamo kwa kuwa kwa sasa ninachofanya nikuchukua tu maoni mbalimbali. Kuhusu kushirikisha wataalamu, hili kwangu ni kipaumbele, ndio maana nimeandika rasmi kwa Katibu wa Bunge kutaka kupewa ushauri wa kitaalamu wa kutafsiri matakwa ya wafanyakazi na ya wadau wote muhimu wa sekta ya hifadhi ya jamii kuwa marekebisho ya sheria yenye maslahi kwa umma. Mpaka sasa ninapozungumza, hatujaandaa muswada wa sheria, wala kuwasilisha taarifa ya muswada huo yenye kueleza malengo na masuala mengine ya msingi. Nilichowasilisha ni kusudio, na katika taarifa yangu kwa umma nimeeleza bayana kwamba nimetoa wiki moja ya kupata maoni ikiwemo ya kitaalamu kabla ya kwenda hatua inayofuata. Uamuzi wa kukusanya saini, ni kupata wabunge ambao wanaona haja ya marekebisho ya dharura ili hatua huo ushauri wa kitaalamu na hatua nyingine ziweze kufanyika kwa haraka zaidi kuepusha migogoro inayoanza kujitokeza. Naendelea kupokea maoni.
 
Nashukuru sana Sober na wachangiaji wengine kwa michango yenu. Nitatafuta wasaa wa kusoma yote kwa ajili ya kupata maoni. Kwasasa tunaendelea na mkutano mpaka saa 11 jioni kwa ajili ya kupata maoni ya moja kwa moja katika masuala ambayo nimeomba yafanyiwe uchambuzi, mnaweza kurejea kupitia:JOHN MNYIKA: MKUTANO WA MTANDAONI KUHUSU MUSWADA WA SHERIA YA MAREKEBISHO YA SHERIA YA HIFADHI ZA JAMII KWA HATI YA DHARURA KUREJESHA FAO LA KUJITOA.....
Mnyika ww n mtetez wa watu wewe ni shujaa wetu
 


Kwanza, katika nchi zote za Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara, hakuna kitu kinaitwa mafao ya kujitoa

Pili, ukiondoa PPF na NSSF, Tanzania ina mifuko mingine pia, nayo ni LAPF, PSPF na ZSSF, huko kote hakuna hilo fao la kujitoa na halikuwahi kutolewa.....

Ndugu Sober sababu ulizotoa hazina uzito wowote kuweza kuhalalisha shutuma dhidi ya wananchi wenzako.

1. Kwa vile nchi zilizo chini ya jangwa la sahara hazina huo utaratibu haiwezi kuwa sababu pekee ya Tanzania kutokuwa na utaratibu huo.

2. Vile vile kutokuwapo fao la kujitoa katika mifuko mingine hapa nchini haiwezi kuhalalisha kufuta fao hilo kwa mifuko inayotoa. Ukumbuke pia katika mifuko uliyoitaja kuna mafao ambayo hutolewa na mifuko hiyo lakini hayapo PPF n.k.

3. Si vema kufikiri kuwa kuwa mtaalam wa sekta fulani basi wewe si mjinga katika sekta hiyo. Hapo utakuwa umepotea njia. Napenda nikukumbushe kuwa wahenga waliposema elimu haina mwisho, sio lazima wakwambie pia ujinga hauna mwisho. Swala la kuondoa ujinga ni endelevu kwa hiyo kwa msingi huo hakuna anayeweza kusema si mjinga katika sekta ambayo ana taaluma nayo.

Pia lazima usiwapuuze watu wanaopaza sauti zao kudai fao hilo. Na katika watu wanaodai fao hilo wamo pia wataalam wa sekta ya hifadhi za jamii.

Sioni kosa kwa Bwana Mnyika kuomba kukusanya maoni na wala sio mtu wa kwanza kufanya hivyo. Mtu wa kwanza kuanza kutoa hoja hiyo na kisha kuambiwa na spika akakusanye kwanza maoni alikuwa Selemani Jaffo. Lakini sijaona ukimshambulia kama unavyofanya kwa Mnyika. Nashindwa kuelewa iwapo kweli una ajenda ya kuwatakia mema wastaafu au ajenda nyingine.

4. Takwimu halali za kukokotoa urefu tarajali wa maisha ni lazima uhusishe rika zote. Huwezi kupindishapindisha kanuni kwa sababu tu umeona hupati jibu ulilopanga kupata. Kwa vile takwimu hizo halali ndizo zinazotumika pia katika mipango ya maendeleo ya serikali duniani kote basi ni sawa kutmia kanuni hizo hizo pia katika mipango binafsi.

Katika hitimisho lako umeongelea mambo kadhaa ikiwamo kufeli kwa biashara, umuhimu wa pensheni na pia umetoa mfano jinsi wazee wa kizungu wanavyokula maisha kwenye fukwe za Zanziba.

Naona kwamba ni hoja zisizo na msingi kwa sababu zifuatazo:

Kwanza hapa Tanzania pekee ni wazee chini ya 5% wanaopata pensheni. Na hao pia sidhani kama wanaishi maisha ya raha kwani ukiacha wanasiasa, wazee wengi wanapokea pensheni chini ya 50,000 kwa mwezi. Ni kichekesho kusema mzee huyu atapata mahitaji yake na kisha akale raha kama unavyouambia umma.

Pili hiyo 95% ya wazee wasiopata pensheni umejiuliza wanaishi vipi?.

Tatu wazee wa Afrika mashariki wamepata malipo gani mpaka sasa?.

Swala la kufeli kwa biashara ni jambo la kawaida haliwezi kuwa kigezo cha kuzuia kuanzishwa biashra mpya. Iwapo itakuwa hivyo basi hata hizo zaidi ya 30% ya biashara zilizofanikiwa hazitakuwepo.
Biashara nyingi zinakufa kwa sababu ya mzigo wa kodi. Ni ajabu kwa serikali badala ya kusaidia biashara hizi ili ziongeze wigo wa ajira na baadae inufaike na kodi ndiyo kwanza inaziua na kukumbatia wageni mpaka sasa mchango wao kwa uchumi ni kiduchu.

Mwisho Je hao wazee wa kizungu una uhakika kama wote walikuwa ni waajiriwa?. Na hata kama walikuwa ni waajiriwa unafahamu mfumo wa penshemi wa mataifa yaliyoendelea?.

Natoa wito kwa Bwana Mnyika kuendelea na mchakato alioanza wala asikatishwe tamaa bali aendelee kukusanya maoni yakiwamo haya ya Ndugu Sober.
 
Maoni yangu kuhusu marekebisho sheria za mifuko (hii iliyolengwa na nyinginezo) ya hifadhi za jamii.

Fao la kujitoa ni haki ya mwanachama, liwepo.

Ili kuweka usawa kwa wale wanaotaka kusubiri miaka 55, kuwe na hiyari toka kwa mwanachama mwenyewe, kuchukua chake au kusubiri miaka 55/60.

Mapendekezo mengine (Haya yameshaelezwa na wengine ila nayarudia kuweka msisitizo)
Mifuko ya jamii ni vyombo vya umma, ni lazima kuwe na chombo cha kudhibiti mishahara na marupurupu. Kwa sasa inaonekana kila kitu kipo hovyo kiasi kwamba fedha za wanachama wachangiaji zinachezewa hovyo tu kwa wakurugenzi wa mifuko kujipangia mishahara na marupurupu makubwa huku wanachama wakipewa mafao duni. Hata SSRA ambao wangekuwa tegemeo wameingia kwenye njia hiyohiyo.

Mafao ya msingi ni lazima yafanane mifuko yote hasa kwenye fomula ya kukokotoa mafao,kuumia kazini, na elimu kwa watoto wa mwanachama ambao umri wao ni chini ya miaka 18.

Mwanachama ni lazima aruhusiwe kukopa fedha zake zilizo kwenye mfuko kulingana na kiasi ambacho amekwisha changia kwa riba isiyozidi mara 2 ya riba ambayo mfuko unatoa.

Riba iwe inatozwa kwenye deni halisi (outstanding debt) kwa hiyo kiasi cha riba kipungue kadiri malipo yanavyorejeshwa.

Hii itawasaidia wengi kujiandalia maisha badala ya kusubiri hadi wastaafu.
 
mkuu unapotosha umma wa watanzania nssf mfanyakazi huchangia 10% na mwajiri ni 10%.
pili nimesikitika kwa kauli yako kwamba mnyika anatafuta cheap popularity, hivi kuu wewe upo nchi gani?
maybe upo nje ya Tanzania hii na unapata habari kupitia blog za hapa tz
ningependa kukufahamisha labda kama hujui au kwa uelewa wangu mdogo. kupitishwa kwa sheria hii na nssra kumekuja baada ya CAG kutoa ngalizo kuhusu ufujaji wa pesa
ambazo ni malimbikizo ya wafanyakazi
sasa je hii mifuko ya hifandhi kama imefanya ufujaji wa hizi pesa ambazo kwa uhalisia ni mali na miliki ya wafanyakazi wanaokatwa kila mwezi kama hifadhi ya baadae.
na ikiwa kama mifuko hii inavyosemekana kwamba itashindwa kuja kutoa marejesho kwa wakati. je huoni kama huu ni mchanga wa macho kwa wananchi na wafanyakazi wanaokatwa malimbikizo haya?
huoni kama huu ni wizi wa waziwazi kwa sababu serikali inafanya haya kupitia shinikizo la ssra ili kupunguza muda wa wao kama serikali kurudisha pesa ambazo wali invest kwenye miradi isiyo endelevu iliyo sababisha kushindwa kurejesha pesa walizochukua kwenye mifuko hii?
huoni kama hii inaziba mianya ya waajiriwa kupata wasaa wa kujiajiri na inatoa nafasi ndogo kwa ongezeko la ajira nchi kwa maana halisi ya kwamba kama mtu akiweza kuacha kazi na kuanzia biashara binafsi anatoa wigo mpana wa kutoa ajira mpya wa watu waliomzungua
kiongozi hii ni nchi ya dunia ya tatu unapota mifano ya dunia ya kwanza unakosea . leo hii sisi bado kupata mahali pa malazi ni tatizo swala la jira ni tatatizo tena unataka kuzuia mitaji ya wajasilia mali wadogo wadogo

tupunguze ubinafsi tufikiri na upande wa pili elimu bila uhalisia ni sawa uendawzimu. tukifanya masihara tutakuja kuwalipa marehemu malimbikozo ya uzeeni. na hii ni mwanzo wa wizi na zulumu kwa jasho la wanyonge
 
nimesikitika sana mkuu ila nina maswali kwako juu ya hili

mosi vipi kwa wanyakazi wa migodini ambao wengu wao hupewa mikataba ya miaka mi 2 mi 2 na ajira zao sio zakudumu. sasa iwapo ikatoa wamepunguzwa kazi rejesho lao la hifadhi huwa stiri?
pili. huoni kama kumnyima mtu asipate rejesho lake pindi anapokatisha au katishwa mkataba ni kama kumnyanyasa kwa pesa ambazo ni miliki yake mwenyewe na jasho lake mwenyewe kwa mfano leo hii amepunguzwa kazi na kazi yake ni ya msimu sasa unataka alale njaa au akose malazi angali na pesa anazo za kumkimu?
tatu huoni kama unafuta ndoto za waajiriwa wengi za kuwa wajasiliamali na wao kutoa ajaira mpya kwa taifa la leo na kesho?
nne hudhani kama pato hili la hifadhi ya mfuko ni nafasi chanya kwa ukuaji wa sekta ya uzalishaji na soko la ajira kwa jamii

kiongozi labda nikukumbushe, tuu ondoa mawazo mgando na tegemezi ya wewe kuwa mwajiriwa kwa maisha yako yote, taifa makini na uchumi imara hujengwa na watu wajasilia mali na watu wenye mawazo chanya

ELIMU BILA UHALISIA NI SAWA NA UJINGA. TUMIA ELIMU IKUSAIDIE KUENDESHA MAZINGIRA YALIO KUZUNGUA
 
Hata kama una hamu ya kumuona Mnyika kapotoka, basi ni bora ungemsubiri tu pengine siku moja anaweza kupotoka kweli kuliko huko huku kulazimisha huko kupotoka unakokutaka. Katika hili wala sijaona hicho unachokiita kupotoka kwake, ila kwa mtindo wa kimagamba wa kulazimisha mambo, haya endeleeni!
 
ni kweli ni tanzania pekee ndio kuna fao la kujitoa lakini umesahau kuwa tanzania ndiyo nchi pekee ambayo serikali inachukuwa pesa za wanachama na kuwekeza kwenye miradi ambayo mingi kati ya hiyo pesa zake zinapotea na nyingine hazilipwi kwa makusudi mfano machinga complex,general tyre,kiwira mine kutaja hayo machache.Pia unatambua nssf inatoa riba ya 1.8% kwa mwaka kutokana na michango ya wanachama ambayo huwa hawatangazi na pia kiwango hicho ni kidogo hakilingani na riba ya benki na ukichukulia mfumuko wa bei ni 19% kwa sasa na mtu akijitoa inabidi asubiri miezi 6 bila kujali hali ya mfumko wa bei
kama wanataka kuiga na nchi nyingine zinavyoendesha mifuko yao ya hifadhi waige mambo yote mazuri kama kuheshimu pes za wanachama na sio kunufaisha wasio wanachama kama ukopeshaji pesa kwa manji na sumaye,watoe riba inayolingana na soko,wasiwekeze kwenye miradi isyo na faida kama ujenzi wa nyumba za polisi na hata uanzishwaji wa ssra ni upuuzi mwingine hiyo kazi ingeweza kufanywa na benki kuu
 
3. Mh. Mnyika mara nyingi kama sio zote, amekua ni mtu wa kufanya kazi kwa data za uhakika na huwa namkubali sana kwa kufanya homework. Ajabu kwenye hili, mara baada ya kikao kuahirishwa kakutana na waandishi wa habari na anaongelea kutafuta sahihi za wabunge!!!... Yani jambo la kitaaluma analitreat kisiasa. jambo litalo impact maisha ya maelfu ya wazee siku za usoni analichukulia kama masihara na kitu cha kushangiliwa kama umefunga goli.


Miaka 50yote ya uhuru cjaona impact yake badala yake serikali inanyanyasa wazee wa watu wa EAC hiyo sio ishu....!

Mkuu umeshindwa kuelewa kazi zetu hapa bongo ni za mikataba mifupi sana na kupata kazi tena ni ishu endapo mkataba umeisha.

Imagine m2 umefukuzwa kazi au umeacha kazi au kwa namna yoyote ile unaacha kazi ukiwa na miaka 30 hadi 35 ina maana unaweza ishi vipi more than 20years ati unasubiri pension? Hiyo c ndo itasababisho vifo vingi vya middle age au working class sababu ya Ugumu wa maisha?
 
Mkuu mtoa hoja (Sober)umeongea mengi, nimekusoma na kukuelewa na yapo mengi ya kukuchangia kwani naona umeongea kijumla mno na hapa nakuona na wewe ukipotoka kwa kujipa ufahamu mkubwa wa tasinia hii na wakati huo huo kushindwa kuona upande wa pili, labda kwa makusudi ili kufikisha ujumbe wako kuwa fao la kujitoa ni baya. Swali dogo tu je, una habari na majadiliano ya SSRA na wafanyakazi wa migodi? Umeona barua SSRA waliyowandikia? Hapa SSRA nao tuseme hawana utaalamu wa tasinia au wewe umewazidi?

niendee kidogo kwa pia kukuuliaza maswali haya mawili ili kuanza kumegua vipengele vichache katika hoja yako pana:
1. Hivi wanachama wa mifuko ya pension wako katika makundi mangapi?
2. Wewe unaongelewa wa kundi lipi?

Mfano tu kuna wenye ajira za kudumu(hadi kustaafu) wako ajira za mkataba wa mwaka mmoja, miwili n.k. nafikirii wapo hata wa miezi, wapo pia wa sekta isiyo rasmi.
 
SSRA ilipoundwa nilidhani ina watu makini lakini naona ina watu wa aina ya Sober. Nina mengi ya kumueleza sober lakini itawachosha wasomaji. Hebu nieme hivi.

Sober asitoe mifano ya kipuuzi. Eti ktk Afrika hakuna nchi yenye utaratibu huu. Sawa tueleze ktk Afrika ni nchi gani ina mifuko mingi kiasi hiki. Mifuko hii ilipoundwa ilikuwa na malengo. Usione ajabu PPF na NSSF kuwa na utaratibu huo, hiyo ni kawaida na ndo maana watumishi wa muda wengi walikuwa NSSF. PSPF hii ni hivi karibuni pamoja na hiyo mingine ya local government.

Huna haja ya kuweka assumptions eti fikilia kijana wa miaka 25 ...... hebu mfikilie kijana huyo huyo afanye kazi kwa miaka 8, enzi hizi za ajila binafsi huju kijana ataacha au kuachishwa kazi. Awe kijiweni kwa miaka 2 halafu apate kwingine tena kwa miaka 3 au hata aachane na ajila za watu aingine kwenye biashara ya kwenda uchina. Yaani kijana huyu unataka asubiri mpaka awe na miaka 55 ndo atafute pensheni yake!! Rubbish!

Kujitoa miaka yote ilikuwa ikiruhusiwa kwa watumish walioko ktk ajira kwa miaka pungufu ya kumi. Hata serikalini ulikuwa unakuwa permanent and pensionable baada ya michanco ya miaka kumi. Chini ya hapo unaweza kujitoa. Safi

Hii mifuko inajidai inawajali wanachama wake na eti kuna niya njema. Hii mifuko iseme wazi kwamba iko ktk hali mbaya kwa upuuzi tu! Mifuko imeruhusu serikali kuingiza mikono kila wakati na kuchota pesa. Wamechota na kuchota na wezi ndani ya mifuko pia wanachota kwa nguvu. sasa wamefulia wanaanza kuzuia watu kutoa pesa yao.

Mifuko imekuwa kama ule mfuko chakavu wa kikao cha harusi. Nasikia mfuko wa bima ya taifa nao wameuanza. Nasubiri nione kama bima hii ya taifa itadumu. Wanachota na kuiba na kununulia malori ya biashara. Stupid!

Mifuko hii inaanzisha miradi feki ya majengo ili wachote 10%, halafu wewe sober unakuja na hesabu dhaifu za maisha ya wa TZ!

PPF wako wapi sasa? Wameambiwa mara ngapi kwamba watakosa wanachama kwa uzembe wao wa kutotoa malipo mazuri. wakahonga waandishi wa habari ili wasiandikwe. Sasa yako wapi wanashindwa kupata wanachama wapya wakati wakitakiwa kulipa wazee. Wazee watalipwa kwa pesa ipi wakati hakuna wapya wanaoingia. Watakula jeuri yao.

Kama ni umri wa kuishi mbona kila mfuko unatumia umri tofauti?*
 
Back
Top Bottom