Mgonjwa wangu wa Kansa Amefariki dunia!!

pole sana, ndio nchi yako hiyo inaharibiwa na serikali dhaifu mpaka kufikia kuchezea uhai wa watu
 
Pole sana, inawezekana madcs wa TZ hawakuweza kugundua mapema sababu yakutokuwa na vipimo sahihi vya gonjwa lenyewe, sasa likijitokeza kwa nje ndipo wanweza kuliona kwa kuona na macho yao.

Nadhani kuna haja ya wa TZ wote kuungana na kuitaka serikali iliangalie hili la vipimo kwa walala hoi.
 
pole sana.ki ukweli huu ugonjwa bado kwa tz haujapewa kipaombele.campeni yake sio kubwa kabisa.na ukitaka kujua huu ugonjwa upo nenda ocean road.sielewi kwa sababu ni suala la vifaa?huwa inanisikitisha kwa nini nimepoteza rafiki yangu mmoja wa karibu pamoja na mtu tu ambae nilionana nae hospitali wakati nilipoenda oceon road kuangalia wagonjwa.kuna mgonjwa mmoja nilizoeana nae sana.baadae alifariki
 
MUNGU amsamehe makosa yake, amuondolee adhabu zake, ampumzishe kwake mbinguni, amen!
 
ee Mwenyezi MUNGU Baba yangu usiyeshindwa kamwe ilaze roho ya marehemu mahali pema peponi ,tuseme Amen
POLE SANA MKUU
i do remember my mother died 13yrs ago huo ugonjwa ni hatari sana
 
kibongobongo ukipata kansa your dead person mama yangu alipata cervical cancer lakini madaktari hawakujua walimfanyia upasuaji eti kuna uvimbe baada ya kugundua hiyo cancer alitibiwa kwa mionzi ila hiyo mionzi ilisababisha kupooza na alikufa akiwa na maumivu makali saana chemotherapy haikumsaidia ndio ilizidsha ugonjwa pamoja na kulipia gharama kubwa miezi minane tena kaka yangu alifanyiwa upasuaji kutoa uvimbe tumboni kumbe na yenyewe ilikuwwa cancer alifanyiwa chemotherapy ambayo na yeye instead ya kumponya waliinguza utumbo so ikawa chakula hajkipiti na yeye alifariki kwa maumivu makali sana. Kutokana na hali hii ikizingatiwa kuwa wote walifariki mikononi mwangu nikiwaona huwa naumia sana nikisikia somebody amekuwa diagnised na cancer hapa bongo coz ni lazima afe tu bora hata ukimwi kuna ARVs . Siku zote nimekuwa nawish nikipata uwezo nisaidie ujenzi wa kituo cha utafiti wa cancer mikoani but hiyo imebaki ni alinacha coz sina uwezo wa kupata hela kufanya hivyo hata nikikusanya mishahara yangu ya miaka 5 bila kutumia hata senti tano nilishaandika barua kwa mbunge wangu ili alisemee hili kwa serikali iki ifanye kitu ila hola! Kwa kweli post hii imenitoa machozi baada ya kukumbuka machungu ya zamani. RIP wote waliofariki kwa ugonjwa wa cancer na Mungu awafariji wote waliopoteza ndugu zao kwa huu ugonjwa
 
inna lillahi wainailayhi rajiun! pole sana mkuu tupo pamoja Inshaallah!!
Yule mgonjwa wangu wa Kansa niliyekuja kuomba ushauri humu ndani kama kuna tiba ya Kansa ya Ubongo hapa Tanzania, Amefariki dunia saa saba usiku wa kuamkia leo. Kuugua kwake kumenifanya niamini sisi watanzania sasa tunatakiwa kuujua ugonjwa huu kwa undani kwani jamaa kwa miaka yote kumi ya kuugua kwake hakuna hata Daktari mmoja aliyewahi kumwambia kama ana dalili za ugonjwa wa Kansa mpaka pale alipozidiwa!!
 
Back
Top Bottom