Mgonjwa wangu wa Kansa Amefariki dunia!!

Kigarama

JF-Expert Member
Apr 23, 2007
2,492
1,230
Yule mgonjwa wangu wa Kansa niliyekuja kuomba ushauri humu ndani kama kuna tiba ya Kansa ya Ubongo hapa Tanzania, Amefariki dunia saa saba usiku wa kuamkia leo.

Kuugua kwake kumenifanya niamini sisi watanzania sasa tunatakiwa kuujua ugonjwa huu kwa undani kwani jamaa kwa miaka yote kumi ya kuugua kwake hakuna hata Daktari mmoja aliyewahi kumwambia kama ana dalili za ugonjwa wa Kansa mpaka pale alipozidiwa!!
 
kuna ndugu yangu alifariki kwa cancer wamekuja kugundua mwishoni kabisa baadaya ya miaka 8 ya kutaabika..Naweza kusema huduma zetu za afya bado ni mbovu kuliko tunavyofikiri..Cancer inaweza kuzuilika katika hatua ya awali kabisa..kwa kumshauri mgojwa kutumia baadhi ya dawa na vyakula..wengi madactari wetu wanakimbilia kuwapiga wagojwa mionzi ambayo baada ya mda mgojwa upatwa na maumivu makali yasiolezeka...
 
Dah. Pole sana. Ndo dunia ya tatu. Ndo maana wakubwa wakipata mafua wanawahi india isijekuwa ni dalili ya kansa ya pua.
 
Pole sana,jana nilisoma thread yako nikashindwa cha kushauri,maana nakumbuka jinsi shemeji yangu alivyopata mateso kwa kansa ya ubongo hadi kufariki mwaka jana.then akafuata baba yangu mzazi halaf shangazi.wote kansa!ulikua mwaka mgumu mno kwangu!
 
Pole sana kiongozi. Tatizo hospital zetu hasa za serikali madaktari wako busy sana na mambo yao maana mshahara ni kidogo kwa mantiki hiyo ukiingia tu kwa Dr. kabla hujamaliza kujieleza kashaandika prescription!!! Udhaifu kila mahali!!!
 
Pole sana kaka.@Kigaram Madakatari wazuri wapo Tanzania ila Vifaa vya kufanyia kazi ndio vipo pungufu kaka pole sana ndio maana Madaktari wanabahatisha kwa kazi zao kutokana na upungufu wa vifaa kaka. Marehemu Mwenyeezi Mungu amlaze pema peponi Ameen.
 
Pole sana kiongozi wote ndo njia yetu.Mungu amlaze anapostahili
 
Pole sana kamanda,na hakika Mwenyezi Mungu atamrehemu na kumpa nafasi ya kuwa ktk ufalme wake.Pole pia kwa wanafamilia kwa msiba mzito,mmepigania kwa nguvu na moyo wa kipekee uhai wake lakini bahati haikuwa kwenu,mwenyezi MUNGU akupeni moyo wa upendo na mshikamano ktk kipindi hiki cha majonzi mazito,awape faraja na neema zake nanyi muishi kwa umoja.poleni sana na be blessed guys!
 
Back
Top Bottom