Mgomo wa wauguzi Mara waua watu wanne

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,896
wauguzi.jpg

Baadhi ya Wauguzi waliogoma

Watu wanne wamepoteza maisha kufuatia wauguzi katika hospitali ya mkoa wa Mara kugoma kutoa huduma kwa wagonjwa, wakidai malipo ya malimbikizo kama ilivyoagizwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda walipwe.Taarifa kutoka chanzo chetu cha habari zimedai kuwa watu waliokufa ni watoto wanne na mtu mzima mmoja.

Walipoteza maisha ni wale waliokosa huduma na baadhi ya wagonjwa walilazimika kuhamishwa na ndugu zao kwenda kutibiwa katika hospitali za binafsi ili kunusuru uhai wao.
Wakati mwandishi wa habari hizi akiwa maeneo ya hospitali hiyo, alishuhudia wagonjwa zaidi ya watatu wakipoteza maisha bila kupewa msaada wa aina yeyote.

Akizungumza kwa niaba ya wauguzi wa hospitali hiyo, John Alex, alisema kuwa uongozi wa hospitali umekuwa ukiwatendea mambo mengi ya kudhalilisha na kushindwa kuwalipa haki yao iliyotolewa na Serikali kwa lengo la kuboresha huduma ya afya jambo ambalo linaonyesha dharau ya hali ya juu.

Alex alisema kuwa walikuwa wakinyanyaswa kwa kipindi kirefu lakini wamekuwa wakivumilia ambapo alisema kwa zaidi ya miaka saba sasa hawajawahi kupewa sare za kazi wala hawalipwi muda wa ziada wa kazi, na pia hawapewi likizo kama watumishi wa sekta zingine
“Fedha hizo zilikuja zikiwa zimeainishwa kila idara itapataje lakini cha kushangaza sisi wauguzi tuliotakiwa kupewa kiasi cha shilingi 10,000 unapewa shilingi 5,000 aliyetakiwa kupewa 15,000 amepewa 10,000 na waliotakiwa kulipwa 5,000 hakulipwa kabisa,”alisema Alex.

Muuguzi Ntunia Machibura, alisema kuwa kufuatia viwango hivyo kuzua utata, walichukua uamuzi wa kufuatilia moja kwa moja kwa uongozi husika ambapo majibu waliyopewa hayakuwaridhisha hatua iliyowasababisha kuanzisha mgomo hadi hapo haki yao itakapokamilishwa.

Hata hivyo, Mganga Mkuu wa mkoa, Samson Winani, alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusiana na mgomo huo hakutaka kujibu chochote bali alisema yeye sio msemaji.Hadi tunakwenda mitamboni, mazungumzo kati ya wauguzi hao na uongozi yalishindwa kufikia muafaka na kusababisha mgomo huo kuendelea huku kazi ya kutoa huduma kwa wagonjwa ikifanywa na madaktari wa hospitali hiyo.
 
Haya waziri Mwinyi kazi ndo umeanza na Mara ndio wa kwanza kukukaribisha kablsa hujavuta kiti kukalia.
 
Kuna utafiti wa kisayansi kuwa hawa watumishi wasingegoma hao wagonjwa wasingefariki? Siku ambazo hawa watumishi wako kazi vifo havitokei hospitalini?
 
Devastating news for Mara Region inhabitants where already health facilities are stretched and the poorest in the nation. The Government Hospital is the only place that handles the sick at night in Musoma Municipality. Dr Mwinyi has to intervene very quickly and rescue the Municipality and its neighbouring areas.
 
Back
Top Bottom