Mgomo wa wafanyakazi tazara mbeya, wakwamisha abiria waliokuwa akienda zambia

bampami

JF-Expert Member
Nov 5, 2011
5,697
4,107
140827134132_mgomo_wa_wafanyikazi_wa_tazara__wawahangaisha_abiria_512x288_bbc_nocredit.jpg

Mgomo wa wafanyakazi wa Tazara wawahangaisha abiria

Sehemu kubwa ya wafanyakazi wa mamlaka ya reli ya Tanzania na Zambia TAZARA Stesheni ya Mbeya nchini Tanzania, wamegoma kufanya kazi tangu leo asubuhi.

Mgomo huo ambao wenyewe wameuita kuwa ni mgomo baridi umesababishwa na mamlaka hiyo kushindwa kuwalipa mishahara yao kwa miezi mitano sasa.

Kwa majibu wa mwandishi wa BBC Baruan Muhuza ambaye yupo safarini kuelekea Kapiri Mposhi Zambia akitumia train ya TAZARA, mgomo huo umesababishwa kukwama kwa train hiyo kuendelea na safari yake hadi kufikia jioni hii.
MSIMAMO WAO
Amesema train ya abiria kutoka Dar es Salaam ilifika mjini Mbeya saa 4.30 asubuhi na hapo wafanyakazi hao waliipokea train hiyo kwa wimbo wa Solidarity forever.
Wafanyakazi hao wameiambia BBC kuwa wanailalamikia Serikali ya Tanzania kwa kuwapuuza madai yao huku serikali ya Zambia ikiwalipa wenzao wa upande wa pili.
Kwa muda mrefu TAZARA imekuwa katika kipindi kigumu cha uendeshaji wa shughuli zake kutokana na kukosa ruzuku ya serikali zote mbili.
140827134322_mgomo_wa_wafanyikazi_wa_tazara__wawahangaisha_abiria_512x288_bbc_nocredit.jpg

Wafanyikazi wanasema kuwa hawajalipwa mishahara yao miezi 5 sasa

Baada ya mivutano na mikakati ya kuboresha shughuli za kabiashara ya mamlaka hiyo, iliamuliwa kuwa kila nchi iendeshe train yake na iishie mpakani kwenye miji midogo ya Tunduma (Tanzania) na Nakonde (Zambia).
TRENI KUISHIA MPAKANI
Mpango huo ndiyo kwanza umeanza kwa train ya abiria iliyoondoka jana Jumanne Dar es Salaam na nyingine ikitoka New Kapiri Mposhi na zitakutana mpakani baadae leo jioni.
Kwa mpango huo wasafiri wanaokwenda upande wa pili wa nchi nyingine watalazimika kushuka na kuingia kwenye train nyingine.
BBC inafuatilia kuona mchakato wa kuhamisha wasafiri hao utakavyokuwa, kwa kuzingatia miongoni mwa wanaosafiri kuna watoto, wazee vikongwe, wajawazito, Lakini pia kunakuwa na walemavu na wenye mizigo mingi.

SOURCE;Bampami: MGOMO WA WAFANYAKAZI TAZARA MBEYA, WAKWAMISHA ABIRIA WALIOKUWA AKIENDA ZAMBIA
 
Nimeona kwenye TV Mid hii Azam Two
Dereve anakuambia mie naendesha train nabebea roho za watu huku mie mwenye nina njaa.

Hii Issue mwakiembe imemshinda,maana kila siku porojo tu.
Kuna siku watakuja kufanya kama walioyafanya reli ya kati na kuuwa watu ndio hapo tutatia akili.
Sehem kama hizi ikiingia hujma basi ni ngum sana kuirejesha hali kuwa ya kawaida.

Wafanyakazi wa Zambia wanalipwa kwa Dollar wa kwetu Shilingi na hata hivyo haufiki kwa wakati.
Acha wagome,maana tumeishazoea hii hali,ila wajue ni hasara kwa upande wetu.
Maana migo hii ya tazara imesababisha hasara ya mabilioni ya pesa,sasa sijui serikali inashidwa vipi kuafikiana na wafanyakazi wakati wanadai haki zao.
Na Maofisa wa Tazara ndio wanaongoza kwa kukimbia kutoa habari.Hii Tazara ni kama ATC tu,sema yenyewe ilinusurika kuchakachuliwa maana wachina walitia mkono,lakini shombo zake ndio hizi.
Acha watie hasara serikali
 
Hali ni Mbayaaaaa.....
 
Miezi mitano bila mshahara!!!? Huu utakuwa ni ukatili wa hali ya juu, wanaishi vipi hao wafanyakazi, ili hali wana watoto wanahitaji ada, kodi ya nyumba na mahitaji mengine ya msingi. Ni wazi kwa kitendo hicho cha kutolipwa mshahara kwa miezi mitano ni ukatili na unyanyasaji wa hali ya juu na haki yao ya kikatiba ya kulipwa ujira kwa kazi uliyofanya imevunjwa. Wizara husika yenye dhamana ya kusimamia TAZARA inapaswa kuwajibika.
 
Kuna siku wataliingiza kwenye Korongo hili ndio wata watajua hasara kubwa ipo wapi.
Maana reli ya kati waliteswaa eee,wakaanza kufanya yao,lamba watu sana tia hasara mpaka wakasikilizwa.
 
Back
Top Bottom