Mzee wa Gumzo
Senior Member
- Apr 21, 2008
- 197
- 5
jumamosi tulimsikia waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Prof.Jumanne Maghembe na waziri wa utumishi Hawa Ghasia wakitoa msimamo wa serikali kuhusu sakata la waalimu kutokulipwa malimbikizo yao yanayofikia bilioni 16.
Katika maelezo ya serikali kwa umma mawaziri hao walidai kuwa waalimu wanaidai serikali bilioni saba na ushee tu kwa maana kuwa walishaanza kulipwa malimbikizo yao na serikali ingali inaendelea kulipa.Serikali ilitumia nafasi hiyo kuwataadharisha waalimu kutokugoma kwa madai kuwa mgomo utakuwa batili.
Kwa upande mwingine, jana jumapili CWT imetoa tamko kuwa taarifa ya seriklali siyo ya kweli kuhusu mkataba unaodaiwa kufikiwa kati ya pande hizo mbili mapema mwezi huu.Vilevile CWT imepinga takwimu zilizotolewa kuhusu malimbikizo ya waalimu.
Nia yangu hasa ni kutaka tufanye tafakari ya kina juu ya sakata hili na staili ya serikali yetu kuyashughulikia matatizo ya wafanyakazi wa umma nchini.Hii siyo mara ya kwanza kwa serikali kutoa vitisho kwa waalimu kuhusu kugoma kwao.Mara zote waalumu wamekuwa wakilalamikia hali iliyopo na wakati waot serikali imekuwa ikitoa ahadi kuwa inahakiki majina na madai yao kabla ya kuwalipa.
Hali hii ya kuwapiga waalimu danadana kila wakati inapaswa kufika ukomo na waalimu wapewe heshima na umuhimu stahili.Serikali inaona njia ya kutatua matatizo ya waalimu ni kuwatishia kuwa watachukuliwa hatua za kinidhamu.Huu siyo mfumo mzuri wa uongozi.Kwa miaka siyo chini ya kumi sasa waalimu hawajaonja utamu wa fani yao na malimbikizo ya madai yao hayalipiki kwa urahisi.
Mfano mzuri ni malipo yaliyofanywa mwezi wa nane mwaka huu.Serikali ilidhamiria kuwaficha ukweli waalimun kwa hazina kuchelewesha salary slip za waalimu mpaka leo lakini chakustaajabisha zile za septemba zilishatolewa.
Kwa ujumla waalimu wanpaswa kufika pahala wakasema YATOSHA.Kama wazazi na walezi wanajukumu zito sana na kugoma kwao kuna athari kwa watoto wa taif hili lakini hawawezi kuendelea kufundisha wakati mioyo yao imejaa ukiungu wa sononeko na kukata tamaa.
Vitisho haviwezi kuwa suluhisho, muhimu kwa waalumu kufikia azma yao ya kugoma na wasiwepo watakaowasaliti wenzao.Tanzania lazima tujifunze kudai haki zetu hata kama ni kwa kulala njaa na kuonekana wabaya.
Haki ya mtu haiombwi inakuwepo tu.Usipoiona basi ujue kuna mtu kaificha na anataka umpigie magoti.Kataa kufanya hivyo.