Mgomo utapita kama ilivyopita mingine, na huu sio wa kwanza wala wa mwisho.
Ndugu yangu si kweli mgomo huu utapita bure, mgomo huu unapita na roho za watanzania maskini. Migomo mingine kweli ilipita, kwa kuwa kama shule zilifungwa kisha zikafunguliwa na watoto wakaendelea na masomo, vituo vya dala dala na vya treni vilifungwa kisha vilifunguliwa na abiria wakaendelea na safari zao. Lakini mtu aliyepatwa na mstuko wa moyo (Cardiac Arrest) na kukosa huduma ya daktari, hawezi kuamka tena na ndo maana leo Mhe. Rais amekutana na viongozi wa madaktari kuangalia jinsi gani ya kumaliza mgomo huu. Natumaini Mhe. Rais atatumia busara tena, kama kwenye Mswada wa Katiba mpya.
Mungu ibariki Tanzani.