Mgomo wa madaktari unachochewa na chama Pinzani-Gazeti RAIA MWEMA

Sidhan kama hilo ni sahii kila mtu anaomba maslahi yake. Yawe juu sidhan kama kuna shinikizo la wapinzani

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Acha UONGO wewe, uzushi haukusaidii hapa jukwaani,

Elewe kuwa mtu yeyote kuwepo jf amepitia mengi, haina tofauti na kumuona nyani mjini ujue kuwa kakwepa mishale mingi!

Gazeti hilo mimi ninalo hapa tangu saa kumi na mbili asubuhi na nimesoma mpaka matangazo yoooooote hakuna habari hiyo!

Danganya wajinga wenzio wa ccm sio wanajf waliofuzu manuvazi yote!

Mods Ondoeni hii habari ni yakizushi tu!

Vema kabisa!

Sijui watu wengine kusoma wanafikiri ni kuweza kutamka a e i o u Tu!!

Hakuna mahali gazeti limechukua jukumu la kusema kama gazeti kuwa linaona na linachukulia kuwa kuna chama pinzani kinachochea Mgomo. Kuona na kufikiri hivyo ni Utovu wa nidhamu na kutokujua kusoma kwa mantiki na uewlewa.

Kamwe huwezi kusingizia Gazeti kitu kama hicho!!!

Inawezekana kuna makundi ya watu na taasisi mabalimbali zinaona hivyo na kuripotiwa na Gazeti hilo ... lakini Huo si mtizamo wa gazeti na wala huwezi kulibebesha mzigo huo wala kulinyooshea kidole.
 
Huo ni ukweli mtupu Chadema wako nyuma ya mgomo huo. Wanataka nchi isitawalike na wananchi waichukie serikali ya CCM na Chadema ipande chati. Lakini sasa watanzania wamejua kwamba chadema ni hatari kuliko sumu.
 
tuweke mbele maslahi ya watanzania kwanza,tuache ushabiki wa kisiasa
 
Huo ni ukweli mtupu Chadema wako nyuma ya mgomo huo. Wanataka nchi isitawalike na wananchi waichukie serikali ya CCM na Chadema ipande chati. Lakini sasa watanzania wamejua kwamba chadema ni hatari kuliko sumu.

Tena ni hatari kupitiliza. Kina Mnyika wameacha kupigania kero za wananchi wako bize kuendesha harakati zisizo na tija. Ningekuwa mkazi wa Ubungo angenitambua
 
Walio wengi CCM ni wagonjwa wa akili na wako dhaifu hata kwenye hoja ! Nashukuru Mungu sijawahi kuwa na kadi ya CCM wala UAMSHO

Kwani una sifa za kuwa mwanachama wewe? Unakataa kitu ambacho huna sifa wala uwezo nacho!
 
wanamtafutaje mchawi? wakati wao wenyewe ndio WANGA?? TENA WAZANDIKI??
 
Walio wengi CCM ni wagonjwa wa akili na wako dhaifu hata kwenye hoja ! Nashukuru Mungu sijawahi kuwa na kadi ya CCM wala UAMSHO

Hatukushangai sana maana toka umezaliwa mwaka '91 unazeeka kwa kasi ya ajabu.
Kule CCM huhitajiki na kwa vyovyote vile umelaaniwa na kuendele kuwa na huo utapiamlo wa akili pamoja na kudumaa kimwili.
Endelea kuwadhihaki baba zako waliokulea na waliokuleta duniani pamoja na kukujengea nchi unayoitukana ukiwa mbali.
 
Vema kabisa!

Sijui watu wengine kusoma wanafikiri ni kuweza kutamka a e i o u Tu!!

Hakuna mahali gazeti limechukua jukumu la kusema kama gazeti kuwa linaona na linachukulia kuwa kuna chama pinzani kinachochea Mgomo. Kuona na kufikiri hivyo ni Utovu wa nidhamu na kutokujua kusoma kwa mantiki na uewlewa.

Kamwe huwezi kusingizia Gazeti kitu kama hicho!!!

Inawezekana kuna makundi ya watu na taasisi mabalimbali zinaona hivyo na kuripotiwa na Gazeti hilo ... lakini Huo si mtizamo wa gazeti na wala huwezi kulibebesha mzigo huo wala kulinyooshea kidole.

Mkuu nadhani hujui unachokisema.Hili gazeti lina malengo na agenda maalum kwa watu wanaoweza kusoma katikati ya mistari.Hilo gazeti limetoa hiyo taarifa na mwandishi wa hiyo habari amejificha na kujiita NA MWANDISHI WETU.Narudia tena kwa mtu makini lazima atilie shaka hiyo habari.
 
Acha UONGO wewe, uzushi haukusaidii hapa jukwaani,

Elewe kuwa mtu yeyote kuwepo jf amepitia mengi, haina tofauti na kumuona nyani mjini ujue kuwa kakwepa mishale mingi!

Gazeti hilo mimi ninalo hapa tangu saa kumi na mbili asubuhi na nimesoma mpaka matangazo yoooooote hakuna habari hiyo!

Danganya wajinga wenzio wa ccm sio wanajf waliofuzu manuvazi yote!

Mods Ondoeni hii habari ni yakizushi tu!
Duh leo Molemo kawa CCM! Hii inaweza kuwa friendly fire nzito tu! Mkuu Molemo unaambiwa unaleta uzushi jukwaani na bahati mbaya mimi sijalisoma hilo gazeti. Tufafanulie mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Walio wengi CCM ni wagonjwa wa akili na wako dhaifu hata kwenye hoja ! Nashukuru Mungu sijawahi kuwa na kadi ya CCM wala UAMSHO

Mkuu hata ile ya lazima ili ujiunge chuo ilikupita?
 
viongozi wasijaribu kukumbia majukumu yake kwa kujidai kuzusha chadema ndiye chanzo ya mgomo wa madaktari.jukumu la serekali ni kuhakikisha mgomo wa madaktari unapatiwa ufumbuzi na kuwa huduma mahospitalini zinapatikana kama kawaida basi.ndicho wananchi wanachotaka.suala la nani mchawi liongelewe baada ya ufumbuzi kupatikana.muhusika wa mgomo ni nani sio muhimu kwasasa.kwanini viongozi wetu wanaendelea kututreat kama watoto wadogo?
 
Back to the Topic please ili tuelewe kama Raia Mwema nao siku hizi wametugeuka ama la.Hiyo habari imo kwenye gazeti la Raia Mwema ama haimo? Na kama Imo Raia Mwema mwema ndio wanadai kuwa mgomo umesababishwa na Chadema ama wamemnukuu mtu maana tokea wiki ya Juzi walipokuja na kichwa cha habari kinachosema kuwa Mnyika amefukuzwa bungeni kwa kusema kuwa wabunge wa ccm ni wapuuzi wakati magazeti mengine yote yaliandika kuwa amefukuzwa bungeni kutokana na kusema Raisi Kikwete ni dhaifu, mbali na kupata sasa matangazo kibao kutoka Serikalini, nimeanza kuwa na wasiwasi nalo...
 
Back
Top Bottom